Umeshawahi kupotea Kariakoo? Juzi ilibaki nukta nipige mayowe

Unadhani ishu ni kujua majina, sio ishu hiyo
Mimi nina experience ya kupotea pia na nilikaa karikoo miaka miwili

Yani siku ya kwanza nilimsindikiza mama mitaa ya aggrey kununua vyombo kwaa jili ya biashara aliyoanza
Huwezi a mini pamoja na uwenyeki wangu niliojikuta ninao baada ya kufanya manunuzi maduka kama saba na zaidi, muda wa kukusanya tulishindwa kukumbuka baadhi ya maduka yalipo, hadi jamaa mmoja wa kampuni ya usafirishaji ambaye ndio awali aliyupeleka kila duka ili kununua alipokuja na kutupeleka mote tulipopita maana yeye tulikuwa nae hiyo awali na alikumbuka hayo maduka na alifahamiana na wauzaji

Kumbuka maduka mengi ya kariakoo yana majina ila mengi pia haya a vibao vya majina ama, hayo majina yapo kwa maandishi madogo

Bado hujaijua kariakoo mkuu, kariakoo mimi hunipotezi kabisaaa mkuu
 
Kweli kabisa. Nilikuwa Bandarini pale nje ya ofisi ghafla sikujua niliko. Miaka hiyo wala hakuna pilika nyingi na siku zote tunazurura kuangalia meli na kwenda kula Babana Split maeneo ya Mkwepu. Nilijihisi niko mji mwingine kabisa nikawa natetemeka. St Joseph church naiona sielewi niko wapi. bahati akatokea mtu ananifahamu akaniuliza unakwenda cinema Avalon? ndio akili ikarudi .
Dah! Mkuu menikumbusha mbali sana enzi za Avalon cinema.
 
Dah nakumbuka kabla ya mwendokasi madaladala ya Mbezi tulikua tunapandia hapa msimbazi karibu na sheli ya big bon, kuna siku nimezunguka madukani wee! Kurudi kituo cha daladala nimesahau wala sheli siioni[emoji23] nilizunguka siku ile na kuuliza watu naogopa wasijekua vibaka wakanipora so naitafuta ile sheli siioni kumbe nazidi kuelekea mnazi mmoja huko. Nikaona basi sasa kama ntaibiwa kwa kuuliza basi! Nikamfata machinga mmoja ndiyo akaniambia huku mbali rudi na njia ileee nikafata nikaona big bon hii hapa nilifurahii fasta nikaingia kwa bus[emoji23][emoji23][emoji23]

Siku nyingine ndugu yangu katoka mkoani kaja kununua mzigo kariakoo akaniomba nimsindikize yeye ni mgeni, tumeenda tumenunua kurudi tupande bus tena sioni kituo dah alinikejeli eti "nilidhani wewe ni mwenyeji kumbe mshamba tu kama mimi"[emoji23][emoji23] hadi tukaulizia kituo kilipo ndiyo tukaoneshwa.

Siku nyingine naenda kariakoo huku congo, hilo bus linaenda Machinga complex! Tumeshushwa hapo sielewi nimeuliza naambiwa nenda njia ile dah naendaa hata sifiki aah nikachukua boda kumbe nilikua nimevuka congo bila kujua naenda mnazi mmoja hivooo[emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] aisee hii nouma sanaa
 
Hapo k.koo majuzi tu mwezi wa sita nimepotea nilipopaki kigari changu

Ilikuwa hivi nimetoka uelekeo wa fire pale kituo cha mafuta nikaja mpk kwnye mataa ya msikiti pale magari ya muhimbili-Kiwalani yanapoingilia nikaingia kama naenda jangwani vuup mpk mtaa wa nyuma kidogo ya China plaza nikapark pale.
Nilikuwa na shida ya kutengeneza Pc nikamaliza shida zangu fresh njaa ikauma nikaenda kula sehemu flani karibu na Kanisa la KKT lile nadhani.

Sasa nikasema acha niondoke nirudi nyumbani eee bwana eeh tafuta mtaa niliopark gari naona hola. Kila nikienda mtaa huu naona mbona kama nilipita hapa nafuata mtaa mpk barabara ya mwendokasi kule hola narudi tena mtaa wa pili hola.

Nilipoteza kama masaa mawili kila nikienda nakuta gari si yenyewe mpk nikasema nimeibiwa gari mana nilipark hapa na siioni.

Ubaya ni kwamba wakati naingia kuna jamaa alinipigia simu hivyo akili ilikuwa kwenye simu badala ya kukariri sehemu mpk nashuka nilikuwa bado naongea na simu tu.

Mungu si athumani mida ya saa kumi hivi nikapata hiyo sehemu ndio naenda kuikuta gari na dada wa parking anasubiri chake nimpe.
Hapo nimechoka mpk akili majasho kama yote sitaki kukumbuka.
[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Hii mada inawalenga sana wale wenye mishe misheza manunuzi kariakoo.

Aisee kama huna uzoefu na ile mitaa, hasa ile ya nguo, nakushauri ukinunua mzigo wako ukiona huwezi tembea nayo bora utafute hoteli ulipie uwe unakusanyia mizigo yako hapo.

Mimi sio mgeni wa k.koo hata kidogo, ila juzi ni kama ndio nimefika kwa mara ya kwanza,

Ipo hivi
Nimefanya manunuzi yangu ya nguo za jumla, Ikawa kila ninapochukua mzigo sababu ni mkubwa na bado naendelea basi naufunga namwachia mwenye duka mpaka nitakapo maliza nazungukia kote nabeba.

Pasipo kuelewa jinsi ninavyoiacha ndio nazidi kuchanganya mambo, imefika saa 9 hivi nikawa nishamaliza, ni kuanza ku kusanya sasa.

Nilikua na location 9, nikaanza moja baada ya nyingine, Zikabaki 3, hizi sasa ndio kimbembeee.

Siku za nyuma ilikua kila nikiacha mzigo basi na kalili ule mtaa na duka ili iwe rahisi baadae, Sasa juzi kwa haraka niliyokua nayo na huku nikiamini sijawahi potea na nishakua mzoefu nika ignore hilo swala,

Aloo, Nilizunguka ile mitaaa huku machozi yakinilenga kadiri mda unavyopita,

Duka la kwanza kati ya yale matatu nililipata baada ya 2hrs, kumbuka hizo 2hrs zote nilikua natafuta bila kupumzika,
Na sio kama nililiona mwenywe ila nilikua napita lesi ndio jamaa akaniita akaniuliza "bro vipi bado sana maana ndio tunakaribia kufunga"?

Nikajifanya "Ahaaa basi poa ngoja tuu nitembee nao" nikachukua mzigo huku moyo ukiruka ruka kwa kushukuru, yaani pale ndio kabisaa nilikua sipawazi kama nilifanya manunuzi.

Sikutaka hata kuchelewa nikaupeleka guest, inshu ni hayo maduka mawili, Kazi ikaanza tena, hapo mda umeenda, watu washaanza kufunga, kila nikisikia wanashusha yale ma milango yao ya bati, napanick natoka nduki.

Nikatafutaweeeeee, inafika saa 12, nimechoka, nimepanick, nimekata tamaa, Jasho na kiu haviniishii Nishanunua maji kama katoni nzima na henganjifu za kutosha ila vyote kila ninapo simama nikiondoka nimesahau.

Ikafika saa moja, Hapo sasa wengi washafunga, nikawa natembea kinyonge, machozi yananilenga nikiona magrili yanashushwa tuu, nikakaa sehemu ilibakia nukta nipige mayoweee.

Sikua na la kufanya zaidi ya kusubiri kesho yake ambayo ni jana, Akili ilikua ishachoka, nikampigia Rafiki yangu aje tuu anitoe pale nilipokuwepo, maana niliona kabisa mwendokasi ikinivaa.

Asubuhi, nikaingia tena, Inafika saa 6, bila bila, hapa nikaanza kupiga hesabu namna ya ku compensate hasara ya kama 900k na usheee(almost 1M kasoro).

Nikakaa tena sehemu, hapa ndipo nikagundua kweli akili ya binadamu kuna mzingira inafanya kazi baadae ukikaa ukijiuliza ni wewe huamini.

Nilianza kuvuta kumbukumbu za kuanzia Mwanzo naingia k.koo ile jana asubuhi, nini nilianza nacho, wapi nilianzia, basi kuanzi hapo mtiririko wa mazingira ya nje ya kuanzia duka la kwanza mpaka la 9 ukanijia.

Hayo ni mazingira ya pale dukani, inshu ni mtaa na njia gani? Kwa kumbukumbu hivyo hivyo nikaja nikajua ni duka la ngapi na la ngapi katika ule mtiririko ndio nimeyapoteza.

Njia kila nikivuta kumbukumbu haziji, nikaona best option ni kwenda kuanzia duka la kwanza kutembea huku nikivuta kumbukumbu, ile ndio ilikua pona yangu, Mzigo wa kwanza nikaupata duka namba 4 mtaa wa Congo na agrrey, mzigo wa pili duka namba 7 Mchikichi na Nyamwezi.

Bahati nzuri ni waaminifu, nikakuta mizigo yangu salama, nikabeba, huyoooo.

Mpaka nikakumbukaga kale ka meme, watu wanakatumaga kiutani ila kumbe inaonesha wao yalishakuta.

"Ulishawahi kupotea kariakoo mpaka ukapita sehemu ukawauliza watu, mliniona nikipita hapa?"
Hatreeeee umepambana hta hvy
 
Siku moja natoka tegeta na lift ya gari la mshikaji mida ya saa moja usiku,tulipofika k/koo jamaa kanishusha akaelekea zake ferry anaenda kigamboni mm ikabidi nichukue usafiri wa home kule gerezani..nikikumbuka Ile siku kilichotokea nachekaga tu maana jamaa tulipofika k koo aliniamsha Tu oya mwanangu kariakoo hii km vp tomorrow basi..nikashuka!!

usingizi jumlisha usiku sikujua kbs nimeshuka mtaa gani. Akili iliganda km nusu saa najiuliza jamaa kanishusha wapi hapa? Ikanibidi nitembee Tu mm mtoto wa mjini bn siwezi potea k/koo lkn bado akili haisomi kbs ninakoenda ni wapi

Nikasema isije nikatokezea kusikojulikana maana nimetembea kishenzi sifiki gerezani ngoja niulize.Nikamcheki muuza mayai kumuuliza asee naelekea iliko stend ya mwendo Kasi akanijibu sasa huku unakoenda mbona unakaribia kufika mnazi mmoja[emoji1787] ..nikamwambia niitie bodaboda akanijibu labda bajaji.Nikakodi bajaji Kwa buku 4 Hadi gerezani..nikikumbuka najiuliza hivi ilikuwaje nikapotea k/koo siku ile.Sipati jibu
Umetishaaa
 
Nimewahi potea kkoo ila usiku[emoji23][emoji23]
Day time ni poa maana tumekua kkoo zaidi ya 20 years. Ila hutaamini, kkoo usiku ni sehemu nyingine kabisaa. Yaani nilikikuta nimefika karume[emoji23][emoji23] hapo ndo nilianzia moja. Sehemu napoteaga day time sometimes ni posta kuanzia mnazi mmoja mpaka posta hapa katikati. Yaan na kusoma kwangu posta 4 years haijawa msaada. Yaani napoteza mwelekeo kabisaa[emoji23][emoji23] kuna siku nikasema nitoke mnazi mpk posta vinjia vya kati lwa mguu. Nilikikuta mara 2 narudi mnazi palepale. Niliumiaaaa[emoji119][emoji119] sikutaka tena nikapanda daladala. Halaf nakua nimefika kamtaa ka posta kabisa hivi viroundabout vya ndani huko kama hindu mandal etc. Dar pa kijinga sana
[emoji28][emoji28][emoji28] hadi Karume, baada ya kuona hamna maghorofa mengi ndo ukashtuka
 
Kariakoo buana[emoji846], ukifika huwa mishale ya usiku inakuwaga kama sehemu nyingine kabisa, japo me nadhani ni kutokuwa na mazoea, Nilipofika DSM kwa mara ya kwanza, nilitamani nifahamu sehemu mbalimbali, Mungu si Athumani nikawa nimezifahamu sehemu nyingi,
One day nmefika Kariakoo kutoka mkoani,mida ya saa tatu usiku[emoji38] nilizunguka kutafuta stend ya daladala hadi saa tano usiku[emoji28], Just imagine masaa mawili, na begi lilikuwa zito kinouma nouma, mara nitokelezee mnazi moja, mara kama naenda Posta, mara nitokee hadi ilipo stend ya sahivi magerezani[emoji28][emoji28] Nikawa najiuliza hivi nipo siriaz kweli, [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hata mie nilipotea,harafu nikawa nasubiliwa na watoto wa kike wachukue mzigo,mm nazunguka tu ,wao wanauliza upo wapi ??,mie nakujaaaa,unaanzaje kumwambia mtoto wa kike umepotea mchana kweupe? Walikuwa askari fulani, wananiambia tupo hapa sheli ,mm sheli naifaham ila siku hiyo niliitafuta bila kuiona

hadi wakakata tamaa ,wife ananipgia cm kuuliza nipo wapi ,si nikaanza kumlaum ,mnakaa mnanituma tuma tu,mm nimepotea ,ndo kuniulizia nipo maeneo yenye mwonekano gani ,nikamtajia ndo kuniambie nishike welekeo gani ndo pona yangu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nilishaacha kwenda kusali mara mbili ajili ya kupotea hapo stone town... Kila nikizunguka nione kanisa silioni hadi muda wa kusali unaisha. Kama unataka kupotea vizuri wewe tokea sokoni darajani halafu nenda kaitafute kanisa katoliki mbona utakoma.
 
Hata mie nilipotea,harafu nikawa nasubiliwa na watoto wa kike wachukue mzigo,mm nazunguka tu ,wao wanauliza upo wapi ??,mie nakujaaaa,unaanzaje kumwambia mtoto wa kike umepotea mchana kweupe? Walikuwa askari fulani, wananiambia tupo hapa sheli ,mm sheli naifaham ila siku hiyo niliitafuta bila kuiona

hadi wakakata tamaa ,wife ananipgia cm kuuliza nipo wapi ,si nikaanza kumlaum ,mnakaa mnanituma tuma tu,mm nimepotea ,ndo kuniulizia nipo maeneo yenye mwonekano gani ,nikamtajia ndo kuniambie nishike welekeo gani ndo pona yangu.
Wewe utakuwa mgeni wa jiji
 
Kama kisehemu kidogo tu kama Kariakoo unapotea, utaweza kuishi kwenye miji mikubwa kama Paris au New York kweli ?

Hii ni dharau sasa,kwani wanaoishi hizo sehemu hawawezi potea wakienda sehemu nyingine?! Hata hivyo Paris na NY pamepangika vizuri na data zake za location ni rahisi sana.Huyu unaemdharau Yes anaweza ishi hizo sehemu vizuri tu na asipotee.
 
Hata mie nilipotea,harafu nikawa nasubiliwa na watoto wa kike wachukue mzigo,mm nazunguka tu ,wao wanauliza upo wapi ??,mie nakujaaaa,unaanzaje kumwambia mtoto wa kike umepotea mchana kweupe? Walikuwa askari fulani, wananiambia tupo hapa sheli ,mm sheli naifaham ila siku hiyo niliitafuta bila kuiona

hadi wakakata tamaa ,wife ananipgia cm kuuliza nipo wapi ,si nikaanza kumlaum ,mnakaa mnanituma tuma tu,mm nimepotea ,ndo kuniulizia nipo maeneo yenye mwonekano gani ,nikamtajia ndo kuniambie nishike welekeo gani ndo pona yangu.

Hapo mwisho pa kumlaumu Wife [emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23]
 
Nilishaacha kwenda kusali mara mbili ajili ya kupotea hapo stone town... Kila nikizunguka nione kanisa silioni hadi muda wa kusali unaisha. Kama unataka kupotea vizuri wewe tokea sokoni darajani halafu nenda kaitafute kanisa katoliki mbona utakoma.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii mada inawalenga sana wale wenye mishe misheza manunuzi kariakoo.

Aisee kama huna uzoefu na ile mitaa, hasa ile ya nguo, nakushauri ukinunua mzigo wako ukiona huwezi tembea nayo bora utafute hoteli ulipie uwe unakusanyia mizigo yako hapo.

Mimi sio mgeni wa k.koo hata kidogo, ila juzi ni kama ndio nimefika kwa mara ya kwanza,

Ipo hivi
Nimefanya manunuzi yangu ya nguo za jumla, Ikawa kila ninapochukua mzigo sababu ni mkubwa na bado naendelea basi naufunga namwachia mwenye duka mpaka nitakapo maliza nazungukia kote nabeba.

Pasipo kuelewa jinsi ninavyoiacha ndio nazidi kuchanganya mambo, imefika saa 9 hivi nikawa nishamaliza, ni kuanza ku kusanya sasa.

Nilikua na location 9, nikaanza moja baada ya nyingine, Zikabaki 3, hizi sasa ndio kimbembeee.

Siku za nyuma ilikua kila nikiacha mzigo basi na kalili ule mtaa na duka ili iwe rahisi baadae, Sasa juzi kwa haraka niliyokua nayo na huku nikiamini sijawahi potea na nishakua mzoefu nika ignore hilo swala,

Aloo, Nilizunguka ile mitaaa huku machozi yakinilenga kadiri mda unavyopita,

Duka la kwanza kati ya yale matatu nililipata baada ya 2hrs, kumbuka hizo 2hrs zote nilikua natafuta bila kupumzika,
Na sio kama nililiona mwenywe ila nilikua napita lesi ndio jamaa akaniita akaniuliza "bro vipi bado sana maana ndio tunakaribia kufunga"?

Nikajifanya "Ahaaa basi poa ngoja tuu nitembee nao" nikachukua mzigo huku moyo ukiruka ruka kwa kushukuru, yaani pale ndio kabisaa nilikua sipawazi kama nilifanya manunuzi.

Sikutaka hata kuchelewa nikaupeleka guest, inshu ni hayo maduka mawili, Kazi ikaanza tena, hapo mda umeenda, watu washaanza kufunga, kila nikisikia wanashusha yale ma milango yao ya bati, napanick natoka nduki.

Nikatafutaweeeeee, inafika saa 12, nimechoka, nimepanick, nimekata tamaa, Jasho na kiu haviniishii Nishanunua maji kama katoni nzima na henganjifu za kutosha ila vyote kila ninapo simama nikiondoka nimesahau.

Ikafika saa moja, Hapo sasa wengi washafunga, nikawa natembea kinyonge, machozi yananilenga nikiona magrili yanashushwa tuu, nikakaa sehemu ilibakia nukta nipige mayoweee.

Sikua na la kufanya zaidi ya kusubiri kesho yake ambayo ni jana, Akili ilikua ishachoka, nikampigia Rafiki yangu aje tuu anitoe pale nilipokuwepo, maana niliona kabisa mwendokasi ikinivaa.

Asubuhi, nikaingia tena, Inafika saa 6, bila bila, hapa nikaanza kupiga hesabu namna ya ku compensate hasara ya kama 900k na usheee(almost 1M kasoro).

Nikakaa tena sehemu, hapa ndipo nikagundua kweli akili ya binadamu kuna mzingira inafanya kazi baadae ukikaa ukijiuliza ni wewe huamini.

Nilianza kuvuta kumbukumbu za kuanzia Mwanzo naingia k.koo ile jana asubuhi, nini nilianza nacho, wapi nilianzia, basi kuanzi hapo mtiririko wa mazingira ya nje ya kuanzia duka la kwanza mpaka la 9 ukanijia.

Hayo ni mazingira ya pale dukani, inshu ni mtaa na njia gani? Kwa kumbukumbu hivyo hivyo nikaja nikajua ni duka la ngapi na la ngapi katika ule mtiririko ndio nimeyapoteza.

Njia kila nikivuta kumbukumbu haziji, nikaona best option ni kwenda kuanzia duka la kwanza kutembea huku nikivuta kumbukumbu, ile ndio ilikua pona yangu, Mzigo wa kwanza nikaupata duka namba 4 mtaa wa Congo na agrrey, mzigo wa pili duka namba 7 Mchikichi na Nyamwezi.

Bahati nzuri ni waaminifu, nikakuta mizigo yangu salama, nikabeba, huyoooo.

Mpaka nikakumbukaga kale ka meme, watu wanakatumaga kiutani ila kumbe inaonesha wao yalishakuta.

"Ulishawahi kupotea kariakoo mpaka ukapita sehemu ukawauliza watu, mliniona nikipita hapa?"
Ungechukua hata risiti angalau majina ya maduka ungekua nayo au nambari za simu. BTW Pole.
 
Nilipotea mtaa nilipo-park gari.
Baada ya kuswampa sana nikamuona dada wa parking aliyenipa risiti ya EFD yuleeee nikamfata.

Ndio akanionesha "gari ile pale... Next time unapo park uliza jina la mtaa ndio uende kwa mizunguko yako"

Nikamtoa buku nikamshukuru sana.
 
Hii ni dharau sasa,kwani wanaoishi hizo sehemu hawawezi potea wakienda sehemu nyingine?! Hata hivyo Paris na NY pamepangika vizuri na data zake za location ni rahisi sana.Huyu unaemdharau Yes anaweza ishi hizo sehemu vizuri tu na asipotee.
Why are you offended so easily my dwag ?
 
Nimewahi potea kkoo ila usiku[emoji23][emoji23]
Day time ni poa maana tumekua kkoo zaidi ya 20 years. Ila hutaamini, kkoo usiku ni sehemu nyingine kabisaa. Yaani nilikikuta nimefika karume[emoji23][emoji23] hapo ndo nilianzia moja. Sehemu napoteaga day time sometimes ni posta kuanzia mnazi mmoja mpaka posta hapa katikati. Yaan na kusoma kwangu posta 4 years haijawa msaada. Yaani napoteza mwelekeo kabisaa[emoji23][emoji23] kuna siku nikasema nitoke mnazi mpk posta vinjia vya kati lwa mguu. Nilikikuta mara 2 narudi mnazi palepale. Niliumiaaaa[emoji119][emoji119] sikutaka tena nikapanda daladala. Halaf nakua nimefika kamtaa ka posta kabisa hivi viroundabout vya ndani huko kama hindu mandal etc. Dar pa kijinga sana
Posta balaaa[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom