Umeshawahi kusaidiwa nini na mganga ukaona kabisa mganga wako fundi?

Naomba usinifuatane PM

Niliambiwa sema chochote unachotaka... Utapata

Nikashindwa kusema na ile chance ime-nicost mpaka leo maana wengine waliambiwa waseme wanachotaka wakasema kweli wamepata...

Kuna waliosema wanataka ndoa wameoa na wengine wameolewa mpaka sasa,

Kuna waliosema wanataka kazi wamepata kazi na wanafanya kazi mpaka sasa,

Kuna waliosema wanataka biashara wamepata biashara na wana biashara zao mpaka sasa,

Mimi sikusema chochote maana sikua naamini katika kile kinachofanyika Ila sasa daaah haya Mambo yapo na watu wanafanikiwa kweli.. ukipuuza unakuja kujilaumu mbele
 
Mkuu nipe huo mchongo basi mimi nikutane na huyo bibi anifundishe hizo dawa
 
Kwa kuwa ni shuhuda ntatoa yangu ,Ila staki pm au judgement, haya ni mambo yaliyopita tulifanya ,tusiaemane vibaya.

Kisa Cha kwanza kilitokea 2010 hapo, nlikuwa kijana Sana Ila mganga huyo yupo Ila jina wala namba sitoi. Nlikuwa nauza spare parts za Mercedes ,Faw ,Howo n.k kwa duka la jamaa kutoka turkey hapa dar,nenda keko uulize jina la Mchopa wa spare parts utapewa story ucheke uanguke .
Ss nlikuja kujua kazi nikataka kumpiku boss, mshkaji wangu akanieleza kuhusu mganga fulani Chipu, Sumbawanga mpaka namba nikapewa. Yule mshkaji alipofatlia nkajidai mambo ya mganga staki Ila kimya kimya weekend moja nlisepa kwenda kule mwenyewe .
Ikumbukwe mkoa wa rukwa wala sumbawanga nlikuwa sijawahi kanyaga, nliposhuka stendi nkaulizia kuulingana na maelezeo ya yule braza mpaka kijiji nkakipata , nikiwa almost kufika kwa yule mganga (sitaki kumtaja jina) nlipatana na mbwa alikaa Kama amechizika hvi ,aisee nlitoka mbio akinifukuza ,nliingia ndani ya compound nkihema nikipiga kelele ,kukatokea yule mganga akamfukuza tule mbwa Kisha kunipa karibu .
Kufupisha, Mzee aliniongoza kwa kichaka chake nkapata jiwe limeegemea mti kando Kuna kijumba kidogo na hapo tulipokaa nakumbuka kulikuwa na kisu kina damu Yaani kichafu ,dhahiri kuonyesha kafara watu walikuwa wanafnya pale.
Kimbunga kilianza pale Mzee aliponiuliza ntakacho nkamwambia nataka kumzidi boss niwe tajiri, akaongea mambo yake Kisha lile jiwe likageuka bibi kikongwe ,alinipa kile kisu akaniambia Kama mm ni jasiri na nataka Mali nichukue kisu kile kisha nifuate kinjia fulani kulikuwa hapo ,kile ntapata kife.
Kushika njia Ile nlipatana na kuku nkampita sikushkanisha ,nilipoendelea mbele bila kupata kitu nkakumbuka nliambiwa kile ntapatana nacho ,nilirudi faster Sana.
Mzee yule kuku tulikimbizana ktk ya nyasi ile kumshika nlikata bawa ila akapepea na hio moja mbali sikumpata ,hii tukio ilipita Kama 2 hours hvi nikimkimbiza kuku yule.
Kurudi nlipata kile kibibi kinacheka balaa,nlirudi nimeshika pande LA bawa nlilokata natoka jasho sana ,akaniambia mwanangu una roho ngumu ,nenda mambo yako yatakuwa sawa ,Ila nisiwai kula kitimoto.
Long story short pale keko nilichakata mbususu nyingi Sana Tena Sana ,yule bosi alipanda ndege na familia Yao hawajarudi mpaka leo aisee .
Aliyopo pale kwa ss nijamaa anaitwa shafa ,anauza matunda kando Kuna stationary ya jamaa anaitwa dula wananikumbuka Sana tu .
Nlikuja jisahau nkala sausage one day nkiwa na Dem fulani kisu ,wanawake Yaani wapuzi ,aliponilisha tu moyo ulipasuka nkakumbuka vile nliambiwa , kila kitu kilienda na hewa mpaka zile pisi nlizokuwa zanikimbiza ...Ila nlijenga nyumba moja kubwa Sana mpaka Leo wazazi na dada zangu wanaifaidi , ujana aisee stosahau .
Leo hii nishamaliza masomo nina Mali Ila sijafikia enzi zile .
Walioko keko nenda kwa dula , au Rick Ross bonge fulani anaendesha bajaji pale ,muulize jina Mzee wa mbususu au Mchopa wa spare utapewa bonge LA story kunihusu enzi hizo .
Kwa nliowakosea enzi zile ,nisameheni Bure ni kiburi cha pesa tu na ujana , uchawi upo Ila Kama unajua kuplay smart nao
 
Daaah very interesting wallah
Lakini maisha yana definition pana na fumbo gumu sana kulitambua yahitaji akili kubwa na hekima ya hali juu.

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 

Kuna siri gani kuhusu kitimoto,mana waganga wanaikataa na huku kwenye dini za wazungu na waarabu wanaikataa,
 
Ingejaribu ndio uanze kulalamika
 
Hujaendeleza kuwa mlipata au?...
 
Mimi nina sheikh wangu mmoja hapo Magomeni Mwembe Chai, ni noma kishenzi. Yeye hakopeshi, ukitaka kuua mtu au kumpa mtu laana ya kuokota makopo anakuambia niletee kuku tu au nyama kilo mbili ale na familia yake.....anadedisha mtu bila hata huruma.
Huruma itoke wapi kuna watu wanastaili kukutana na hasira ya mnyama na si hasira ya kibinadamu. Huyo mganga awadedishe tu kwakweli na tena awauwe sana kuna watu wanajikuta wao ni Mungu kumbe ni wapumbavu wakubwa
 
Kama ni kweli, Basi better late than never [emoji137][emoji137][emoji137][emoji1787][emoji1787]
 
Ni story kweli ya jamaa yangu wa karibu sana.

Mkewe alianza kuumwa pressure akiwa na ujauzito wa miezi 6.

Wiki nyumbani, wiki hospitali yalikuwa ndiyo maisha yake.

Tulifikia wakati tulishauri daktari atoe mimba mama apone. Daktari alikataa kabisa. BP ilikuwa inapanda hadi 180.

Huwezi amini, alijifungua salama japokuwa mtoto alikuwa njiti.

Cha ajabu, baada ya kujifungua tu, tumbo lilijaa mara mbili ya alipokuwa na mimba. Alivimba miguu kiasi cha kushindwa hata kusimama. Daktari anasema licha ya hali hiyo, hawaoni tatizo lolote katika kupima na hata BP imerudi hadi 110.

Ikawa mshikemshike, hali tete. Si mgonjwa wala watunzaji na daktari mwenyewe tumekata tamaa. Ndipo mmoja wa ndugu akasema nitatenda dhambi mgonjwa apone.

Alikuwa mkristo wa imani ya juu. Wale wa kusali na kulala kanisani. Alikwenda kwa witch doctor. Hakupewa chochote zaidi ya kuambiwa arudi hospitali na kwamba atajua yeye cha kufanya na mgonjwa baada ya saa 3 atasimama.

Alipofika hospitali mgonjwa alishazima. Anasubiriwa tu akate moto.

Baadaye akawa kama ameshtuka fulani, akafungua macho. Akaonekana kurejea uzimani.

Kweli baada ya saa 4 hivi, mgonjwa aliweza kusimama kwa kujitegemea. Akawa mzima tena.

Sote tulimwamini yule witch doctor. Shemeji yetu mzima hadi leo, tena kwa gharama ya sh. 30000/= tu.
 
Alimtibuje huyo jamaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…