Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🤣😅😂 ila wee mtu ni msumbufu na mkorofi... Ungemkuta kavurugwa angekugeuza bataBaada ya kuona biashara yangu imekwama nikaongea na wenyeji wa mji, nikapelekwa kwa mganga mwanamke,
Kwanza mganga huyo akikaa anaogea kama anapokea simu au anapokea maelekezo kutoka sehemu,
Nilikutana na watu wa hadhi tofauti wanamiliki mabasi mapya na magari mengine mapya wamepeleka yakafanyiwe uchawi,
Zoezi la kwanza baada ya kujieleza akanituma nikachote maji kwenye kisima chake, hiki kisima ni maalum kwa kazi hiyo ya kiganga, kipo umbali kama wa kilometer moja kutoka mji ulipo,
Hivyo nilipewa mashariti nisigeuke hadi nikifika nyumbani kwa mganga kupeleka maji na endapo nikigeuka napaswa kurudia zoezi upya.... ila nikajikuta nimegeuka nikiwa nakaribia kufika... niling'atwa na nyuki kwelikweli,
Nikaona uvivu kurudi tena kisimani nikaamua kwenda kwa mganga na maji yale yale .. nilipofika tu akaniamba usikae wewe umegeuka (umekosea mashariti) rudia zoezi, ikanibidi nirudie[emoji23]
Tulishindwana alipoanza kuniuliza
Kabila langu, Wazazi wangu kama wapo hai, idadi ya watoto na mke, pia nichague nani nataka afahamu ninachokifanya endapo nakufa ataendeleza mali.
Nikamwambia nimegailisha zoezi kwa leo ngoja nikajitafakari upya, akanigundua namkimbia akanipa adhabu kabla sijaondoka nikanunue jogoo mkubwa zaidi ya wote nitakaemkuta kwenye cage ya wauzaji sokoni nimpelekee,
Kufika sokoni nikakuta bei mbaya nika bargain nikachukua mdogo kati ya yule mkubwa zaidi, ile kurudi kwa mganga akasema sio huyo, kamlete yule mweupe uliyemuacha[emoji23] tulisumbuana zoezi hilo mara 3 ikabidi nikubali kumnunua na kumpelekea.
Nikatoka nduki hata nyuma sikutazama tena.
VP ulimpata bibi huyoMkuu pumu inanisumbua mno, nipe connection ya huyo mganga
Ha ha haaaaa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]Ilikuwa Ujiji. Nimepigika kinyama mimi na mwanangu Q. Ghafla mbele yangu naona bango la Uganga, kwa maelekezo hakukuwa mbali na pale. Tunafika tunapisha na wateja ( kama sikosei ni mtu na wakeze ).
Yule Mganga alikuwa ni mwanamke! Basi baada ya salam akaanza makeke yake, shida zetu akazipatia Mule mule toka mwanzo wa Safari yetu mpaka ile siku tunafika kwake! Shida ikawa moja tu! Anataka 40000, sasa nikajiuliza yaani huyu Bazazi ameona yoote lakini kashindwa kujua kama hatuna ata mia? Nikamwambia fresh Mmama we tufanyie kazi sisi tutakupa 60000 sio hiyo 40000, basi ile kainuka tu kuingia ndani kuchukua madubwana yake, mimi nikakusanya pesa 45000 zilikuwa pale kwenye ungo na kinokia Obama nikamwambia Q mwanangu hii nauli tusepe. Tukatokomea hivyo yaani mpaka Mwaloni. Tukauza kale kanokia 15000 jumla tukawa na 60, tukala 7000, tukalipia boti 6000 kwa kila mmoja. Kufika mbele mbele huko kuna kijiji kipo ndani ya Gombe, mida ya saa 1:30 ile Boti inazama, tunatumbukia kwenye lile ziwa, maji naanza kuyaona meusi mwanangu hajui kuogelea anakaba shingoni anaogopa kufa, hali inazidi kuwa tete kila nikijitahid anishike japo ukosi wa shati yule maaluni kakaza kabali......sitosahau. yule mama alitupiga kitu kizoto. Siiendelezi naishia hapa.
Naona hili ungewapelekea wabunge wetu moja kwa moja....watakusaidia kabisa.Naomba hapa wale watembea kwa sangoma mtoe shuhuda zenu mliyokutana nayo kwa waganga na toka umeanza kwenda Mganga.
Alikusaidia nini ukaona kabisa shida yako imetatuliwa kwa nguvu ya mganga.
Ikiwezekana mtaje mganga alipo na wengine wakauone uwezo wake.
Waganga hawa hawa waliambiwa atakeye toa Fununu ya Alipo Mo Dewj familia itampa kitita cha 1bilnlion na wote wakala nduki[emoji1787][emoji1787]
Matapeli hawa hawana msaada wowote.
Acha banaKwa taarifa yako namjua mganga aliyemrudisha mo!
Nina matatizo mtu anisaidie na contakt za watsaap nataka mgangaSasa boss mimi huwa najuulizaga mbona sasa watu wengi hawana yale mafanikio makubwa ya kutisha. Au ndo mpaka umwage damu?
Anzisha uzi ndugu, mm hayo mambo tofauti wapo watakusaudia wanaojuaNina matatizo mtu anisaidie na contakt za watsaap nataka mganga
Mm nilipew ya mvuto na mganga wa Mtwara nikagombana na rafiki zangu wote. Haya amambo ya ushirikina sio ya kuyazoeazoea walahialinipa mafuta ya mvuto huyu jamaa, nikiongea na hizi pisi hazichomoi, nikamfuata tena nikamwambia nipe ya biashara akanambia ni hyohyo dogo we unachotakiwa ni kunuia tu unachotaka, aisee we acha tu hii dunia ina maajabu mengi sana
Husein yule ni mtaalam wa nyota astrologyIlikuwaje Bakwata ikamtambua sheikh yahya hussein
Kuna vitu vikubwa viwili vinafuana. Usasa na ukale.. maisha ya sasa yako mjini miji ilikojengeka. Vijana wanaopenda sana kwenda kuyaishi haya. Wanatoka makwao huko nchimbilimbi kwenda mjini kuyatafta. Ukale nao unataka watu wake.. Babu zetu wanaona kale yenye thaman mnoo. Wazaz hawataki watoto waende mjini. Uchawi pia nia sayansi kale ndio mana umefungamana sana na kupinga maendeleo ya kisasa (husda).sijawai kusikia ana mizimu wala majini
Yeye hutuambia ni dawa za asili alifundishwa akiwa mdogo kusaidia kupata mifungo iliopotea , kuikinga mifugo dhidi ya wanyama wakali
na kujua mtu aliekwenda safari ya mbali kama bado yupo hai ama alishakufa
Dawa hizo pia hutumika kuwaita watoto waliokwenda mjini kutafta maisha na kusahau kurudi kijijn kusalmia wazee ,unambiwa ukifanyiwa hizo dawa utatafta kila njia urudi kwenu hata kwa mkopo ama kutembea kwa mguu
Na kuna ingine alinambia ikitokea hataki mtoto wake aende kutafuta maisha mbali na nyumban anachota unyayo wake anamix dawa na kwenda kuufunika na chungu
kuanzia hapo aliefunikwa hawez hata kufikiria kusafiri wala kwenda kuishi mbali na nyumbani.
Wapi huko uelekeze hapa mana mwakan na mm naanza kampeni za kugombea ubungeBaada ya kuona biashara yangu imekwama nikaongea na wenyeji wa mji, nikapelekwa kwa mganga mwanamke,
Kwanza mganga huyo akikaa anaogea kama anapokea simu au anapokea maelekezo kutoka sehemu,
Nilikutana na watu wa hadhi tofauti wanamiliki mabasi mapya na magari mengine mapya wamepeleka yakafanyiwe uchawi,
Zoezi la kwanza baada ya kujieleza akanituma nikachote maji kwenye kisima chake, hiki kisima ni maalum kwa kazi hiyo ya kiganga, kipo umbali kama wa kilometer moja kutoka mji ulipo,
Hivyo nilipewa mashariti nisigeuke hadi nikifika nyumbani kwa mganga kupeleka maji na endapo nikigeuka napaswa kurudia zoezi upya.... ila nikajikuta nimegeuka nikiwa nakaribia kufika... niling'atwa na nyuki kwelikweli,
Nikaona uvivu kurudi tena kisimani nikaamua kwenda kwa mganga na maji yale yale .. nilipofika tu akaniamba usikae wewe umegeuka (umekosea mashariti) rudia zoezi, ikanibidi nirudie[emoji23]
Tulishindwana alipoanza kuniuliza
Kabila langu, Wazazi wangu kama wapo hai, idadi ya watoto na mke, pia nichague nani nataka afahamu ninachokifanya endapo nakufa ataendeleza mali.
Nikamwambia nimegailisha zoezi kwa leo ngoja nikajitafakari upya, akanigundua namkimbia akanipa adhabu kabla sijaondoka nikanunue jogoo mkubwa zaidi ya wote nitakaemkuta kwenye cage ya wauzaji sokoni nimpelekee,
Kufika sokoni nikakuta bei mbaya nika bargain nikachukua mdogo kati ya yule mkubwa zaidi, ile kurudi kwa mganga akasema sio huyo, kamlete yule mweupe uliyemuacha[emoji23] tulisumbuana zoezi hilo mara 3 ikabidi nikubali kumnunua na kumpelekea.
Nikatoka nduki hata nyuma sikutazama tena.
Wenhe maduka mengi Kariakoo walozi. Kuja jamaa zangu rafiki yangu kabisa nampigia uwinga dukani kwake lakin hataki ukae zaid ya lisaa ndani ya duka. Lazima akutimueWatafuteni WAKINGA
Hivi mkuu mfano tu nikaenda kufungua yard kisarawe ya magari kule wanapolima mihogo sana alafu nimwambie mganga anipatie dawa ya kuvuta wateja wanaweza kunifata mpaka huko[emoji23][emoji23] mana nasikia hizi dawa hatari
Hahahah embu nisaidie wewe ndugu yanguQueen[emoji23][emoji23][emoji23]
Nilivunjika mguu mbeya mjini nikaenda hospital wakadai inabidi niukate nikatonywa na waja wema niende ILEJE nikaenda nikaungwa mguu kienyeji mpaka leo natembea.
VIPI NIMUITE MGANGA MSHIRIKINA?!
Kwamba ningemuomba huyo Mwenyez Mungu nisingekatwa mguu.
EndeleaMwamba alitoka na Bangi ndoo mbili na nusu moro vijijini,njia za ndichindichi akatokea chalize.
Mwamba akadaka abood pale sheli kona ya kwenda tanga pale.
Kitu ikatupiwa kwenye buti wayaaa to dar.
Akashuka ubungo,mwamba akapita njia ya juu mpaka kwenye mwendo kasi.
Wayaaa mpaka posta,dah pale akakuta askari kibaoo na mbwa moyo paaap akakumbuka babu alimwambia :
"utakuta mbwa sehemu usitikisike wewe nyoosha tuu".....
Wale askari walikuwa busy kubishana kuhusu mpira huku jibwa liko mbele yao likiwatizama na ulimi nje mwamba akapita kati yao wayaaa mpaka feri akavuka maji to kigamboni.
Akadaka daladala kwenda gheto kwa wakuu wa kazi kisha akashukia hichi kituo kiko nyuma kidogo pale kuna njia pacha huyo akaanza kunyata mdogo mdogo akafika geto mlangoni akasikia kuna raia ndichi wanapiga story,akajisemea itakuwa wana wako ndichi kisha akagonga mlango.......
Niendelee ama nisiendelee......................................