Umeshawahi kusaidiwa nini na mganga ukaona kabisa mganga wako fundi?

Umeshawahi kusaidiwa nini na mganga ukaona kabisa mganga wako fundi?

Baada ya kuona biashara yangu imekwama nikaongea na wenyeji wa mji, nikapelekwa kwa mganga mwanamke,

Kwanza mganga huyo akikaa anaogea kama anapokea simu au anapokea maelekezo kutoka sehemu,

Nilikutana na watu wa hadhi tofauti wanamiliki mabasi mapya na magari mengine mapya wamepeleka yakafanyiwe uchawi,

Zoezi la kwanza baada ya kujieleza akanituma nikachote maji kwenye kisima chake, hiki kisima ni maalum kwa kazi hiyo ya kiganga, kipo umbali kama wa kilometer moja kutoka mji ulipo,

Hivyo nilipewa mashariti nisigeuke hadi nikifika nyumbani kwa mganga kupeleka maji na endapo nikigeuka napaswa kurudia zoezi upya.... ila nikajikuta nimegeuka nikiwa nakaribia kufika... niling'atwa na nyuki kwelikweli,

Nikaona uvivu kurudi tena kisimani nikaamua kwenda kwa mganga na maji yale yale .. nilipofika tu akaniamba usikae wewe umegeuka (umekosea mashariti) rudia zoezi, ikanibidi nirudie[emoji23]

Tulishindwana alipoanza kuniuliza
Kabila langu, Wazazi wangu kama wapo hai, idadi ya watoto na mke, pia nichague nani nataka afahamu ninachokifanya endapo nakufa ataendeleza mali.

Nikamwambia nimegailisha zoezi kwa leo ngoja nikajitafakari upya, akanigundua namkimbia akanipa adhabu kabla sijaondoka nikanunue jogoo mkubwa zaidi ya wote nitakaemkuta kwenye cage ya wauzaji sokoni nimpelekee,

Kufika sokoni nikakuta bei mbaya nika bargain nikachukua mdogo kati ya yule mkubwa zaidi, ile kurudi kwa mganga akasema sio huyo, kamlete yule mweupe uliyemuacha[emoji23] tulisumbuana zoezi hilo mara 3 ikabidi nikubali kumnunua na kumpelekea.

Nikatoka nduki hata nyuma sikutazama tena.
🤣😅😂 ila wee mtu ni msumbufu na mkorofi... Ungemkuta kavurugwa angekugeuza bata
 
Habari wadau Kwa wakazi wa mzizima wenye changamoto ya uzazi magonywa ya watoto ngiri pumu Niko mkoa Kwa bibi mnaweza kuniagiza dawa wale wenye changamoto. Za uzazi mimba kutoka bibi anatibu hii wale niliowapa namba naamini watakua mashahid
 
Ilikuwa Ujiji. Nimepigika kinyama mimi na mwanangu Q. Ghafla mbele yangu naona bango la Uganga, kwa maelekezo hakukuwa mbali na pale. Tunafika tunapisha na wateja ( kama sikosei ni mtu na wakeze ).
Yule Mganga alikuwa ni mwanamke! Basi baada ya salam akaanza makeke yake, shida zetu akazipatia Mule mule toka mwanzo wa Safari yetu mpaka ile siku tunafika kwake! Shida ikawa moja tu! Anataka 40000, sasa nikajiuliza yaani huyu Bazazi ameona yoote lakini kashindwa kujua kama hatuna ata mia? Nikamwambia fresh Mmama we tufanyie kazi sisi tutakupa 60000 sio hiyo 40000, basi ile kainuka tu kuingia ndani kuchukua madubwana yake, mimi nikakusanya pesa 45000 zilikuwa pale kwenye ungo na kinokia Obama nikamwambia Q mwanangu hii nauli tusepe. Tukatokomea hivyo yaani mpaka Mwaloni. Tukauza kale kanokia 15000 jumla tukawa na 60, tukala 7000, tukalipia boti 6000 kwa kila mmoja. Kufika mbele mbele huko kuna kijiji kipo ndani ya Gombe, mida ya saa 1:30 ile Boti inazama, tunatumbukia kwenye lile ziwa, maji naanza kuyaona meusi mwanangu hajui kuogelea anakaba shingoni anaogopa kufa, hali inazidi kuwa tete kila nikijitahid anishike japo ukosi wa shati yule maaluni kakaza kabali......sitosahau. yule mama alitupiga kitu kizoto. Siiendelezi naishia hapa.
Ha ha haaaaa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Naomba hapa wale watembea kwa sangoma mtoe shuhuda zenu mliyokutana nayo kwa waganga na toka umeanza kwenda Mganga.

Alikusaidia nini ukaona kabisa shida yako imetatuliwa kwa nguvu ya mganga.

Ikiwezekana mtaje mganga alipo na wengine wakauone uwezo wake.
Naona hili ungewapelekea wabunge wetu moja kwa moja....watakusaidia kabisa.

cc: @BungeTanzania
 
alinipa mafuta ya mvuto huyu jamaa, nikiongea na hizi pisi hazichomoi, nikamfuata tena nikamwambia nipe ya biashara akanambia ni hyohyo dogo we unachotakiwa ni kunuia tu unachotaka, aisee we acha tu hii dunia ina maajabu mengi sana
Mm nilipew ya mvuto na mganga wa Mtwara nikagombana na rafiki zangu wote. Haya amambo ya ushirikina sio ya kuyazoeazoea walahi
 
sijawai kusikia ana mizimu wala majini
Yeye hutuambia ni dawa za asili alifundishwa akiwa mdogo kusaidia kupata mifungo iliopotea , kuikinga mifugo dhidi ya wanyama wakali
na kujua mtu aliekwenda safari ya mbali kama bado yupo hai ama alishakufa

Dawa hizo pia hutumika kuwaita watoto waliokwenda mjini kutafta maisha na kusahau kurudi kijijn kusalmia wazee ,unambiwa ukifanyiwa hizo dawa utatafta kila njia urudi kwenu hata kwa mkopo ama kutembea kwa mguu

Na kuna ingine alinambia ikitokea hataki mtoto wake aende kutafuta maisha mbali na nyumban anachota unyayo wake anamix dawa na kwenda kuufunika na chungu
kuanzia hapo aliefunikwa hawez hata kufikiria kusafiri wala kwenda kuishi mbali na nyumbani.
Kuna vitu vikubwa viwili vinafuana. Usasa na ukale.. maisha ya sasa yako mjini miji ilikojengeka. Vijana wanaopenda sana kwenda kuyaishi haya. Wanatoka makwao huko nchimbilimbi kwenda mjini kuyatafta. Ukale nao unataka watu wake.. Babu zetu wanaona kale yenye thaman mnoo. Wazaz hawataki watoto waende mjini. Uchawi pia nia sayansi kale ndio mana umefungamana sana na kupinga maendeleo ya kisasa (husda).
Kuna movie Moja hiv ya Amerindian inazungmzia hili. Mzaz hataki mwanae aende mjini ili ameithishe uchawi dogo anaondoka Kwa kutoroka kutafta maisha. Anafanikiwa na kuwa mtu mmoja mkubwa sana kwenye kampeni ya Sheria huko. Siku anayaorudi kutembelea kwao anaanza kukumbana na uchawi unaomsubiri arudi.
 
Baada ya kuona biashara yangu imekwama nikaongea na wenyeji wa mji, nikapelekwa kwa mganga mwanamke,

Kwanza mganga huyo akikaa anaogea kama anapokea simu au anapokea maelekezo kutoka sehemu,

Nilikutana na watu wa hadhi tofauti wanamiliki mabasi mapya na magari mengine mapya wamepeleka yakafanyiwe uchawi,

Zoezi la kwanza baada ya kujieleza akanituma nikachote maji kwenye kisima chake, hiki kisima ni maalum kwa kazi hiyo ya kiganga, kipo umbali kama wa kilometer moja kutoka mji ulipo,

Hivyo nilipewa mashariti nisigeuke hadi nikifika nyumbani kwa mganga kupeleka maji na endapo nikigeuka napaswa kurudia zoezi upya.... ila nikajikuta nimegeuka nikiwa nakaribia kufika... niling'atwa na nyuki kwelikweli,

Nikaona uvivu kurudi tena kisimani nikaamua kwenda kwa mganga na maji yale yale .. nilipofika tu akaniamba usikae wewe umegeuka (umekosea mashariti) rudia zoezi, ikanibidi nirudie[emoji23]

Tulishindwana alipoanza kuniuliza
Kabila langu, Wazazi wangu kama wapo hai, idadi ya watoto na mke, pia nichague nani nataka afahamu ninachokifanya endapo nakufa ataendeleza mali.

Nikamwambia nimegailisha zoezi kwa leo ngoja nikajitafakari upya, akanigundua namkimbia akanipa adhabu kabla sijaondoka nikanunue jogoo mkubwa zaidi ya wote nitakaemkuta kwenye cage ya wauzaji sokoni nimpelekee,

Kufika sokoni nikakuta bei mbaya nika bargain nikachukua mdogo kati ya yule mkubwa zaidi, ile kurudi kwa mganga akasema sio huyo, kamlete yule mweupe uliyemuacha[emoji23] tulisumbuana zoezi hilo mara 3 ikabidi nikubali kumnunua na kumpelekea.

Nikatoka nduki hata nyuma sikutazama tena.
Wapi huko uelekeze hapa mana mwakan na mm naanza kampeni za kugombea ubunge
 
Mwamba alitoka na Bangi ndoo mbili na nusu moro vijijini,njia za ndichindichi akatokea chalize.
Mwamba akadaka abood pale sheli kona ya kwenda tanga pale.
Kitu ikatupiwa kwenye buti wayaaa to dar.
Akashuka ubungo,mwamba akapita njia ya juu mpaka kwenye mwendo kasi.
Wayaaa mpaka posta,dah pale akakuta askari kibaoo na mbwa moyo paaap akakumbuka babu alimwambia :
"utakuta mbwa sehemu usitikisike wewe nyoosha tuu".....
Wale askari walikuwa busy kubishana kuhusu mpira huku jibwa liko mbele yao likiwatizama na ulimi nje mwamba akapita kati yao wayaaa mpaka feri akavuka maji to kigamboni.
Akadaka daladala kwenda gheto kwa wakuu wa kazi kisha akashukia hichi kituo kiko nyuma kidogo pale kuna njia pacha huyo akaanza kunyata mdogo mdogo akafika geto mlangoni akasikia kuna raia ndichi wanapiga story,akajisemea itakuwa wana wako ndichi kisha akagonga mlango.......
Niendelee ama nisiendelee......................................
 
Nilivunjika mguu mbeya mjini nikaenda hospital wakadai inabidi niukate nikatonywa na waja wema niende ILEJE nikaenda nikaungwa mguu kienyeji mpaka leo natembea.

VIPI NIMUITE MGANGA MSHIRIKINA?!

Kwamba ningemuomba huyo Mwenyez Mungu nisingekatwa mguu.

Mungu hadhihakiwi, utavunjika kiuno na usiungike!!
 
Mwamba alitoka na Bangi ndoo mbili na nusu moro vijijini,njia za ndichindichi akatokea chalize.
Mwamba akadaka abood pale sheli kona ya kwenda tanga pale.
Kitu ikatupiwa kwenye buti wayaaa to dar.
Akashuka ubungo,mwamba akapita njia ya juu mpaka kwenye mwendo kasi.
Wayaaa mpaka posta,dah pale akakuta askari kibaoo na mbwa moyo paaap akakumbuka babu alimwambia :
"utakuta mbwa sehemu usitikisike wewe nyoosha tuu".....
Wale askari walikuwa busy kubishana kuhusu mpira huku jibwa liko mbele yao likiwatizama na ulimi nje mwamba akapita kati yao wayaaa mpaka feri akavuka maji to kigamboni.
Akadaka daladala kwenda gheto kwa wakuu wa kazi kisha akashukia hichi kituo kiko nyuma kidogo pale kuna njia pacha huyo akaanza kunyata mdogo mdogo akafika geto mlangoni akasikia kuna raia ndichi wanapiga story,akajisemea itakuwa wana wako ndichi kisha akagonga mlango.......
Niendelee ama nisiendelee......................................
Endelea
 
Back
Top Bottom