Umesoma vitabu gani mwaka 2022 na wengine tuvisome?

Umesoma vitabu gani mwaka 2022 na wengine tuvisome?

Chuo Cha ustaarab tafsiri yake kwamba School of civilization hahaaaaa
Kwamba wakenya/ waafrika walikuwa hawajui kulima!
Pure whitewashing our history
Jamaa aliandika kiustaarabu sana. Alisema kuwa wazee wao walijua kulima, lakini hali na mahitaji yamebadilika hivyo wabadilike. Ila pi aliwaambia kuwa hawajui kupika na mahindi ni chakula cha mifugo🙂
 
Duuuh mna pata wapi muda wa kusoma vitabu vyote hivyo ..?

Naunga mkono hoja ya usomaji vitabu . ni chakula cha ubongo.
Muda wa kusoma ni mwingi sana mkuu. Mfano safari hii nimetumia sana muda ambao TANESCO wamekata umeme kusoma. Hata ukikaa unasubiri msosi unaweza soma pages kadhaa.
 
Acheni kuchosha watu akili. Maisha yalivyomagumu hivi huo mda wakusoma vitabu utatoa wapi? Wakati wengi wanakula mara moja kwa siku tatu na kuoga gizani mara moja kwa wiki.
unaweza tafuta kitabu juu ya kukabiliana na maisha magumu, au juu ya kula na kushiba, au namna ya kuishi bila kuoga.🙂🙂 Vitabu vina mambo mengi.
 
Kwa mwaka hu sijasoma. Ila nimejipangia 2023 nisome vitabu vingi na wanangu nijifunze mambo mengi kupitia vitabu. Nataka bint yangu mdogo aanze kusoma vitabu kuanzia mdogo
Pitia huu uzi upakue Nalutuesha na Adili na nduguze, mnaweza kuvienjoyhttps://www.jamiiforums.com/threads/tupeane-sofcopies-za-vitabu-vya-kiswahili-kwenye-huu-uzi.2049540/
 
Acheni kuchosha watu akili. Maisha yalivyomagumu hivi huo mda wakusoma vitabu utatoa wapi? Wakati wengi wanakula mara moja kwa siku tatu na kuoga gizani mara moja kwa wiki.
Correction....'acha kunichosha akili' na siyo ''acheni kuchosha watu akili''......na utaendelea sanaa tuuu kula mlo mmoja au usipokuwa makini utaishia nusu mlo kabisa haaaaa.....kusoma vitabu unaweza kupata maarifa humo hata ya kuboresha maisha yako. By the way huwa unapata muda wa masaa mangapi kuingia mitandaoni kusoma udaku na mambo yasiyo na tija??
 
🙂🙂🙂🙂🙂
 
Back
Top Bottom