Umetafuta Fundi wa gari yako? Uliza chochote kuhusu gari lako

Hivi ikitokea gari ikaongeza fuel consumption huwa shida ni nini? Before 14-15km/hr now around 12 km/hr.. Toyota belta 2006 model

Sent using Jamii Forums mobile app
.
Sababu ya kwanza inaweza kuwa ni tatizo la emission.

Inaweza kua 'fuel filter' imeziba, kama haujabadilisha fanya hivyo. Pia 'throttle body' inaweza kuwa chafu na inatakiwa kusafishwa. Air cleaner au MAF (mass air flow sensor) pia inaweza kua chafu. Kuna 'spray can' ya kuisafisha MAF au unaweza tumia 'rubbin alcohol'. Ukaiweka (rubbing alcohol) kwenye spray bottle halafu unapulizia kwenye MAF kwa ndani kuisafisha, rubbing alcohol ita dissolve dust particles zote na kuzi-evaporate.

Pia inaweza kuwa kuna tatizo la 'vacuum leaks', ile mipira inayozunguka kwenye engine inasaidia kuiambia 'computer ya gari' kiasi cha air/fuel mixture inayotakiwa. kama imetoboka/imakatika mahali basi 'computer ya gari' inaweza fikiri engine inahitaji mafuta mengi kuliko kawaida.

Sababu ya pili inaweza kuwa ni 'compression'.

Hili ni tatizo la ndani ya engine. kunatakiwa kuwe kumezibwa vizuri. kama kuna sehemu ina 'leaks' basi nguvu ya engine itapungua kiasi fulani na hii itasababisha utumie mafuta mengi kuliko kawaida.

Sababu ya tatu inaweza kutokana na auto transmission (kama unatumia) kuwa mbovu ambapo gari haibadili gear inavyotakiwa kwa kuishia kwenye low gears. Hii hufanya engine itumie mzunguko mkubwa (high revolutions) kuliko kawaida ambapo husababisha mafuta mengi kuchomwa.

Vile vile Kuna baadhi ya magari yanakuwa na 'sports mode' ambapo ukibonyeza ki-button inazuia 'tranny' ku shift kwenda 'overdrive' na hivyo kufanya iishie kwenye low gears (zinakula mafuta). Jaribu kuangalia 'owners manual' ya gari lako kama ina 'sports mode option'.
 
Gari yangu INA kimbia sana seemu ya speed 50 natembelea 40 nikipigwa tochi inaonyesha speed 55

Sent using Jamii Forums mobile app
.
Inawezakana speedometer inamatatizo, inabidi iwe calibrated vizuri, ule mshale wa kuoneshea hauko kwenye zero mark wakati gari imesimama.

Haukutaja aina ya gari/mwaka, lakini inaweza kuwa ni speed sensor imeharibika (hii ni kwa magari ya zamani, 80's, 90's). Kama ni gari mpya 2000's basi ABS (Antilock brake system) imeharibika.
 
Overdrive ni nini na inamanufaa gani?

.
Katika magari yanayotumia 'automatic transmition', inapokuwa kwenye mwedokasi fulani, ili kuwe na 'efficiency' (kutumia mafuta kidogo), overdrive gear hutumika. Hii inasaidia engine kuwa na mzunguko ndogo sana na hivyo kuondoa mitetemo na makelele.
 
Gari kutoa moshi mweusi ni kiashiria cha nini.?

Na moshi mweusi je?

Piston rings ndio mdudu gani huyu?

NAWASILISHA NA KUTANGULIZA SHUKRANI.

.
Moshi mweusi ni viashiria vya kuwepo kwa 'carbon deposits' ambayo hutokana na 'incomplete combustion'. Piston rings hizi ni valves zinazozuia oil isiingie kwenye chemba.
 
Ilimradi iwe ndani ya ile range kwenye deep stick, haina shida isipokuwa kama unauliza nini kinasababisha oil kupungua kidogo.
.
Engine (piston rings) inapozeeka, huwa inabeba kiwango fulani cha oil kutoka chini ya engine (block) na kuipeleka mpaka kwenye chemba wakati piston inapopanda na kushuka (mzunguko wa engine). Kiasi hicho cha oil huunguzwa kwenye chemba kila wakati gari inapowaka. Baada ya muda 'oil level' hupungua kwa kiasi kikubwa.
 
Overdrive ni nini na inamanufaa gani?
Nadhani Overdrive ni kwa magari ya kizamani tu, siku hizi hamna kitu kama hicho. Overdrive ilikuwa ni design ya transmission (greabox) ya gari kusudi kuiwezesha kwende spidi za juu bila kuwa stress kwenye engine na transmission yenyewe. design za siku hizi zinajitosheleza wala hazihitaji hiyo kitu tena.
 
Yangu horn na radio zimegoma shida nini mkuu? Kingine, hata nikilock gari kwa funguo, inanyonya betri.
 
Naomba kuuliza fundi....

Gari yangu ni Suzuki Vitara 2.6D i/c Turbo, Automatic Petrol engine. Lakini nilishabadilisha engine yake kutoka ile ya Six Cylinders na kuweka ya four cylinders...

Naomba kufahamu matumizi ya kawaida na halisi ya mafuta ya gari aina hii iwapo kila kitu kipo ktk order kwa maana ya mechanically iko okay, hakuna dosari mahali
 
Huwezi kipata hicho unachokitaka mkuu coz gari yenyewe ushaifanyia mkorogo
 
Gari yangu inagonga sana mbele nikikata kona,inavuma na nikiingiza gia inastuka kwa sauti gu,gu,gu ni injini ya RAV 4 3S gearbox ua 4wheel
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…