Nyie usiombe kuachwa na Mabasi ya Mikoani hasa kipindi kile Stendi kuu ilikua Ubungo π
.
Kuna siku nilikua naenda Mbeya sasa nimefika ubungo kumbe nimesahau Tiketi, ikanibidi nirudi kufuata. Nimefika stendi Basi ndo kwanza linatoka nililia kama mtoto mdogo ikabidi watu wanisaidie kulisimamisha. Nilisemwa hadi nilijuta.
Vipi wewe umewahi kuachwa na mabasi au Treni?
Ni zamani kidogo, niliwahi kuachwa na bus la Exercutive, nilikuwa naenda Harare kwenye summit fulani. Bus lilikuwa linaondoka saa 11 alfajiri. Gari ya kwanza.
Nikapitiwa na usingizi, nikaamshwa na simu yao. Nikapiga hesabu nikaona siwezi kuwahi, nikadanganya kuwa niliahirisha safari na nilitoa taarifa ofisini kwao kwa simu.
Hiyo ilileta mgogoro wa kwenye simu na jamaa wao aliyenipigia, mimi nilishikilia msimamo wangu, hadi akakata simu kwa hasira.
Kulipokucha nikaenda ofisini kwao Kisutu, nikaenda kushikilia msimamo wangu. Huko nako ilikuwa balaa, nikashikilia kuwa nilipiga simu kuahirisha safari.
Wao waling'ang'ania kuuliza nilipiga namba ipi, nami nikawaambia sikumbuki, ila ni moja ya namba iliyo kwenye ticket.
Kitu kilichoniokoa ni kwamba ticket yangu ilikuwa na ya kurudi, maana waliniambia nina bahati nilikuwa na ticket ya kurudi. Wakanipa ticket nyingine, nikaondoka baada ya siku mbili.
Ova