Umewahi kuchapwa/kupigwa na mzazi/mlezi?

Mi baba aliwah nipiga mpaka kuhisi kuzimia ,hadi nikawa namuambia baba nataka kuzimia ,,tokea hapo hakunipiga tena ,nimekumbuka nimejisikia vibaya lo
Ujue umenifanya nicheke kwa nguvu sana..eti nataka kuzimia[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Dah... Mie kosa nililofanya sisemi.....ila mshua alinipa kipondo cha kufa mtu... Magumi, mateke na vibao....kisha akanining'iniza mtini kichwa chini miguu juu siku2 bila kunywa wala kula [emoji13] [emoji13]
Duh!!bora utuambie tu. I'm curious,ulifanya nn[emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Maskini,pole sana. Ni kweli muda mwingine watoto wanapigwa kwa sababu ya stress za wazazi..wanatafuta kwa kumalizia hasira. Nmehuzunika sana[emoji20]
 
Jamaniiii.
Mimi nakumbuka kisa changu,nilivyokuwa mtoto age ya miaka 7-10 nilikuwa nasumbuliwa sana na kifua cha kikohozi. Yaani nilikuwa nikipigwa na kaubaridi kidogo tu naanza kukohoa. Sasa nikawa Nina Tabia ya kuogelea mvua zikinyesha. Siku moja bimkubwa akanibamba akaniambia wewe una tatzo la kifua,haifai uogelee mvua. Na nilikuwa nikiogelea mvua tu mpaka naumwa kabisa siku zingine ila nikawa sisemi tatzo la homa ni nini. A couple of days baada ya kupewa warning nikarudia kuogelea halafu mama alikuwa anatoka kazini,kapita na mwavuli wake si akanibamba nipo kwenye mvua tena kwenye vidimbwi vya maji machafu pia,jamani nilivyorudi nyumbani,alinizabua maana nikisema kupigwa haitoshi. Alinizabua vya kutosha sana mpaka akaanza kulia yeye mwenyewe. Duh!!! Sitokaa nisahau kile kipigo a.k.a mkong'oto heavy
 
Enzi hizo nipo la tano napenda sana Mpiraa bhanaa.. Nyumbani nachelewa kurudi!! Yakaja matokeo nimekuwa mtu wa 9 akati kawaida ni 1 mpak 4 mwisho...khaaa Nadhani siku ilee Hata Baba wa mbinguni alisikia kilio changu...Nilikula kibanoooo toka kwa bi maza mpka mkono wake ulivimba..!! Tulipofungua shule uwanja wa mpira ulikuwa kituo cha Polisi yani....na ndoto za kuwa mcheza mpira zikafutika jumla.
 
Dah... Mie kosa nililofanya sisemi.....ila mshua alinipa kipondo cha kufa mtu... Magumi, mateke na vibao....kisha akanining'iniza mtini kichwa chini miguu juu siku2 bila kunywa wala kula [emoji13] [emoji13]
Pole sana Mkuu, nimecheka sana. Kwa adhabu hiyo hilo kosa lilikuwa ni kali sana.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mimi nilichapwa na baba tena kwenye zizi LA ng'ombe dada alikuwa mtoro shuleni tulikuwa tukisoma shule Moja Alf mimi sikuwa nasema nilikuwa namtunzia siri waalimu wakiniuliza namtetea lbd anaumwa au anauguza,,,, sasa siku mama alipoitwa shuleni mmmh nilijuta kuzaliwa makosa ya mtu mwingine nikachapwa mm
 
dah mkuu ulikua na roho mbaya sana.
 
Dah... Mie kosa nililofanya sisemi.....ila mshua alinipa kipondo cha kufa mtu... Magumi, mateke na vibao....kisha akanining'iniza mtini kichwa chini miguu juu siku2 bila kunywa wala kula [emoji13] [emoji13]
Inaonekana ww ulikuwa zaid ya mafia jina lako tu ni jibu tosha
 
Daah!!! Poleni sana!
 
Hahaha! Pole!!!
Kuzabua na kukong'otwa ndo inaeleze vizuri vipigo vingine.
 
Jamani!!! Waliziua ndoto zako kwa kibanooo!!!
 
Nilipigwa mara ya mwisho na baba nikiwa la tano.

Kaondoka zake mjini kaniambia nifanye kazi za nyumbani, nioshe vyombo na kufanya usafi ikiwa ni pamoja na kuteka maji.

Kidume nikapiga chai nikaaenda misele ile narudi nakuta mzee kafika alikuwa na boot moja imeandikwa chini ya unyayo BASE basi bhna nikasalimia mzee na kuingia ndani.

Ile naingia ndani naona giza la ghafla kumbe milango imefungwa nipo na mzee ndani hakuna kazi imefanyika, stiki zikaanza za rejareja hadi shingoni.

Duh BASE ikanikalia shingoni nikapewa stiki za kutosha ili kujiokoa nikavunga nimezimia anapiga silii wala kutikisika.

Mzee anahisi ameua akafungua milango wee nilitoka nduki kama Hamorapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…