Joseverest
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 52,812
- 71,392
Mh.!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]Me kuna siku nimemsindikiza mama yangu mdogo kwa bwanaake bila kujua,sasa akaniacha sehemu akaniambia nimsubiri anakuja muda si mrefu,then ni mbali na tunapoishi(sie tunakaa kigamboni then tumeenda mtoni kwa azizi ally)sasa bhana nikamuona anakatiza vichochoro tu mwishowe kapotea hapo sina hata mia ya nauli wala maji nikakaa kwenye hicho kibaraza toka saa sita mchana mpaka saa kumi jioni njaa iliuma wee mpaka ikapoa,nililia wee mpaka nikapoa,nikawa nawaza muda wa mama kurudi kazini ndo umewadia na sie tuko huko,sasa mamdogo kaja kuchomoka hiyo saa kumi yuko hoi tukaondoka kurudi home mpaka tunafika ni saa 12 maza kesharudi saa nyingi,swali la kwanza lilikuwa tulikuwa wapi me nikaropoka mtoni loh!tulipigwa haifai kusimulia tena tulipigwa mpk na wajomba tulipopata upenyo tukatoroka kwenda kujificha nyumba ya tatu kutoka home tukaletwa asubuhi yake kuombewa msamaha.....tangu siku hiyo sijawahi rudia kumsindikiza mtu sehemu nisiyoijua.
😀😀😀😀😀😀😀Mimi nilikua na tabia ya kuiba sadaka kanisani pale chang'ombe machinjioni katoliki jamani..nilikua natumikia kanisani kwa hiyo nilikua najua sadaka inapowekwa mimi nilikua najiseviaga ile miatano yenye pundamilia.nilipobambwa nilikula kichapo mwake na kuzomewa kinoma.kurudi home ilikua ndio msala zaidi hakuna wa kunitetea na taarifa zilishafikishwa home.ikabidi nijisalimishe kwa mjumbe lakini haikusadia kitu jamani nilipigwa mpaka nikaomba bia badala ya maji.
Hataree sana.Siku ingine nikabandua kabati la nguo la chumbani kwa nyuma alafu nakwapua then nalirudishia ukutani kwa kulisogeza tu.nadhani ilipokuja kubumburuka ilibidi nikaombe hifadhi kanisani lakini haikusaidia maana na kwenyewe nilishaharibu.ikabidi niache tabia ya udokozi mpaka leo hii sisubutu kwa vipigo vile.😀😀😀😀😀😀😀
tehe tehe tehe mnafananaWamama wote tuko hivyo
Kweli kabisa mkuu. Kuna Mzee jirani yetu alikuwa analaani watoto Wa miaka 10. Eti umelaaniwa wewe na kizazi chako.[emoji15] [emoji15] yaani ajabu,maneno yote mabaya anawaambia wanae Wa kuwazaa kabisaUkichunguza kwa makini wengi walikuwa abuse...kwenye jamii yetu tunaona kama ni kitu cha kawaida ila ni abuse. Kama wewe ulipigwa na mzazi wako sio lazima na wewe umfanyie hivyo mwanao.
Pole sananimepigwa na mama tabia ya kwenda kucheza kwa majirani tobo na wavulana na mpira wenyewe itakawa . pigwa mno mpaga nikampa mama a,k,a ya simba ........... mbaya zaidi wadogo zangu nao michezo wakaiga na mama hataki mtoto kwenda kwa jirani bila sababu .. tukawa tunapemana zamu ya kumchunga akitokea tu unasikia mtu ana sema huyo simbaaa wote tunarudi nyumbani unajifuta vumbi wewe mama anapiga sana aisee ..
Nilikuwa na 7.Darasa la kwanza jamani!!!! Au ulianza ukiwa na miaka 15!!!
Ulizidi utundu mkuu!!! Yaani wazazi wanasema kabisa katafute fimbo... Ukileta ndogo sana eti usiumie ndo wanaenda kuleta komoa, bora ata ulete fimbo ya kweli [emoji4][emoji4]Mama alikuwa master wa leather belt ass whooping,mdingi mpole so yeye alikuwa ni vifinyo tu.Kipigo cha mzazi shurti ulie na uonyeshe kuwa unaumia asa ww jifanye nunda.Uzuri wazazi wangu walikuwa hawachapi ovyo ovyo ni vile tu nlikuwa mtundu sana.walikuwa wanakuhesabia makosa tu ukifanya mara moja unakemewa tu ikifika mara ya tatu lazima uchezee kipondo cha kibabe.
Nakumbuka kichapo kikubwa nlichowahi chezea ilikuwa sababu ya kucheza msikitini wakati wa swala,ebana mzee aliniwamba balaa,tena fimbo nliambiwa nkachume mwenyewe.kuanzia siku hyo mpaka leo nikiingia msikitini nakuwa na utulivu wa ajabu(ushuiy).
Mzee wangu ni toluuu haswaaa!!! Ko anakukamata mikono yote pamoja na kushughulikia matako!!! Daaah!!! Ukikosea eti uzuie fimbo kwa mkono P.O.P itakuhusu!!! Viboko vyake vilikua vya haja tena vya kuhesabu... Unajua kabisa nachapwa vinne lakini sikalii matako siku mbiliWazazi wana aina tafauti tafauti za uchapaji
-Kuna ile anakuchap huku anakusema na kukutajia kosa ulilolifanya alafu mwishowe anakuuliza "utarudia tena?" huku kichapo kinaendelea ukisema sirudii anauliza tena kwa msisitizo "UTARUDIA?"mpka aridhike na jibu lako ushachezea nyingi
>Aina nyengine ni ile unapigwa huku uko kwenye movement(freestyle),unachapwa mkwaju wa mguu ukishika mguu unalambwa ya mgongo,ukirudi nyuma unayo,ukienda mbela imo mara mnaanza kuzunguka kama mduara huku mikwaju inaendelea alimradi tu mko kwenye motion.
>Nyengine ni ile ya kimya kimya,yaani anayekuchapa haongei kitu na hataki unayechapwa ulie,unachapwa kiafsa,hiiara nyingi ni kwa wale wanaokaa nyumba za kupanga au mzazi asiependa ijulikane kama anakuadhibu
Duuh!!! Mama yako atakua alikua na hasira sanaDaaa nakumbuk cku moja tumezngua mimi na kaka na dgo anaenifata,,,sas maza alivkua mtata akataft fimbo ote watatu, tukakimbia ,mimi kwa ujinga wangu hata kabla hasira hazijamuish bi mkubwa nikasema aaah ngja nirud kwan atanifanyej,,, mamaaaa!!!! nlikutana na jiwe usoni kiasi kwamba nikalal apoapo nilpokua huku damu zinamwagika usoni,,,ila damu ni nzito kuliko maji coz yy mama huyohuyo nd alini take care mpk nkarud kweny hali ya kawaida ,,,tangu cku ile mama akiwa amekasirka mimi nakaa mbaliiii yasije jirudia ya kipindi ichooo ,,,yote kwa yote nampenda sana mama yangu kunifundsh mengi
Kabisa jamani!!! Mzazi kumpiga mtoto kama mwizi si vizuri kabisa... Wazazi wa siku izi wa kidijitali... Juzi kuna mama amekasirika anataka kumchapa mwanae wa miaka minne, ile kanyanyua fimbo mtoto akaangua kilio cha haja... Mama si akatupa fimbo na kuanza kumbembeleza mtoto, wote tulicheka aisee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hivi wazazi wa kipindi hiki wanapiga watoto kama zamani? Mimi nimepigwa ila kuna rafiki wakati tupo shule ya msingi alipigwa na mzee wake sijawahi kuona kipigo kile ingekuwa leo yule mzee jela ingemuhusu kabisa jamaa aliletwa shule hawezi kutembea amekatwa sikio, alama za visu mgongoni na bado akampiga mbele ya mwalimu mkuu walimu wakamuombea msamaha jamaa angekufa. Wakati mwingine wazazi wetu walitumia vibaya nguvu zao kutuabuse. Mada imenigusa mno
Hakika huo ni uponyaji endelea kumshukuru Mungu kwa yote aliyokutendea maishani mwako.Asante ndugu, nilishasamehe na mungu amweke mahali pema peponi, kipigo wanaohadithia huku bado sana, Unasahau ilipo soap dish unapigwa bila nguo[emoji24] uchi kabisa, Wao bia mwendo mdundo Nyumbani ugali na mchicha aisee!! Nawashukuru sana kunisomesha mana nahisi nisingestarabika. Nimejiahidi kutouvunja moyo Wa mwanangu awae yote na hata Wa pembeni.
Mie mama mdogo tulikua tunaishi nae... Sasa kumbe yeye usiku wazee wanavyoenda kulala yeye anatoroka kwenda kwa wanaume na kurudi kabla hakujapambazuka mbaya zaidi anaacha mlango wazi... Baba akastukia mchezo, sa nne binti katoka baba akaweka stuli nje na kumsubiri mpaka alivyorudi... Jamani sijawai ona mzee anahasira kiasi kile... Mama mdogo alitundikwa kwenye mti kichwa chini tena uchi wa mnyama... Mzee alitembeza viboko mpaka mikono ikaanza muuma.Me kuna siku nimemsindikiza mama yangu mdogo kwa bwanaake bila kujua,sasa akaniacha sehemu akaniambia nimsubiri anakuja muda si mrefu,then ni mbali na tunapoishi(sie tunakaa kigamboni then tumeenda mtoni kwa azizi ally)sasa bhana nikamuona anakatiza vichochoro tu mwishowe kapotea hapo sina hata mia ya nauli wala maji nikakaa kwenye hicho kibaraza toka saa sita mchana mpaka saa kumi jioni njaa iliuma wee mpaka ikapoa,nililia wee mpaka nikapoa,nikawa nawaza muda wa mama kurudi kazini ndo umewadia na sie tuko huko,sasa mamdogo kaja kuchomoka hiyo saa kumi yuko hoi tukaondoka kurudi home mpaka tunafika ni saa 12 maza kesharudi saa nyingi,swali la kwanza lilikuwa tulikuwa wapi me nikaropoka mtoni loh!tulipigwa haifai kusimulia tena tulipigwa mpk na wajomba tulipopata upenyo tukatoroka kwenda kujificha nyumba ya tatu kutoka home tukaletwa asubuhi yake kuombewa msamaha.....tangu siku hiyo sijawahi rudia kumsindikiza mtu sehemu nisiyoijua.
HahahahaMimi nilikua na tabia ya kuiba sadaka kanisani pale chang'ombe machinjioni katoliki jamani..nilikua natumikia kanisani kwa hiyo nilikua najua sadaka inapowekwa mimi nilikua najiseviaga ile miatano yenye pundamilia.nilipobambwa nilikula kichapo mwake na kuzomewa kinoma.kurudi home ilikua ndio msala zaidi hakuna wa kunitetea na taarifa zilishafikishwa home.ikabidi nijisalimishe kwa mjumbe lakini haikusadia kitu jamani nilipigwa mpaka nikaomba bia badala ya maji.