Umewahi kuchapwa/kupigwa na mzazi/mlezi?

Me kuna siku nimemsindikiza mama yangu mdogo kwa bwanaake bila kujua,sasa akaniacha sehemu akaniambia nimsubiri anakuja muda si mrefu,then ni mbali na tunapoishi(sie tunakaa kigamboni then tumeenda mtoni kwa azizi ally)sasa bhana nikamuona anakatiza vichochoro tu mwishowe kapotea hapo sina hata mia ya nauli wala maji nikakaa kwenye hicho kibaraza toka saa sita mchana mpaka saa kumi jioni njaa iliuma wee mpaka ikapoa,nililia wee mpaka nikapoa,nikawa nawaza muda wa mama kurudi kazini ndo umewadia na sie tuko huko,sasa mamdogo kaja kuchomoka hiyo saa kumi yuko hoi tukaondoka kurudi home mpaka tunafika ni saa 12 maza kesharudi saa nyingi,swali la kwanza lilikuwa tulikuwa wapi me nikaropoka mtoni loh!tulipigwa haifai kusimulia tena tulipigwa mpk na wajomba tulipopata upenyo tukatoroka kwenda kujificha nyumba ya tatu kutoka home tukaletwa asubuhi yake kuombewa msamaha.....tangu siku hiyo sijawahi rudia kumsindikiza mtu sehemu nisiyoijua.
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Mimi nilikua na tabia ya kuiba sadaka kanisani pale chang'ombe machinjioni katoliki jamani..nilikua natumikia kanisani kwa hiyo nilikua najua sadaka inapowekwa mimi nilikua najiseviaga ile miatano yenye pundamilia.nilipobambwa nilikula kichapo mwake na kuzomewa kinoma.kurudi home ilikua ndio msala zaidi hakuna wa kunitetea na taarifa zilishafikishwa home.ikabidi nijisalimishe kwa mjumbe lakini haikusadia kitu jamani nilipigwa mpaka nikaomba bia badala ya maji.
 
😀😀😀😀😀😀😀
 
😀😀😀😀😀😀😀
Hataree sana.Siku ingine nikabandua kabati la nguo la chumbani kwa nyuma alafu nakwapua then nalirudishia ukutani kwa kulisogeza tu.nadhani ilipokuja kubumburuka ilibidi nikaombe hifadhi kanisani lakini haikusaidia maana na kwenyewe nilishaharibu.ikabidi niache tabia ya udokozi mpaka leo hii sisubutu kwa vipigo vile.
 
Siku hiyo sikupigwa ila alinifanyia ukatili sana mzee.

Tulienda kucheza ngoma fulani za asili zilikuwa zinapita toka saa tisa hadi saa moja jioni tunacheza ngoma, tuliporudi nyumbani mzee kauliza mlikuwa wapi ? Tukaanza kudanganya na maneno mengi kama wazaramo.

Nilikuwa na dada zangu wawili basi tukapika na kula ila baada ya msosi nikaenda kulala ile nafika chumbani nakuta hakuna godoro kitandani nikawa nashangaa shangaa tu hapo chumbani.

Akaja mzee akaniambia leo Hakuna kulalia godoro naomba vua nguo ulale.....[emoji26][emoji26][emoji26][emoji26] mzee ntalalaje juu ya kitanda bila godoro tena kitanda chenyewe cha chuma hakina chaga ni minyororo tupu.

Aisee mwanaume nikasema na mimi sipangiwi nikavua nguo na kakifua kangu kama ka erick omondi nikalala kwenye vyuma chini ya usimamizi wa mzee had usingizi ukanipitia.

Nilipoamka asbh nimechorwa mwili na vile vyuma hadi nakahisi kulia.

Asante mzee kama uko humu najua umesahau ila nilikomaa sana UNA DUME SIO UTANI.
 
Ukichunguza kwa makini wengi walikuwa abuse...kwenye jamii yetu tunaona kama ni kitu cha kawaida ila ni abuse. Kama wewe ulipigwa na mzazi wako sio lazima na wewe umfanyie hivyo mwanao.
Kweli kabisa mkuu. Kuna Mzee jirani yetu alikuwa analaani watoto Wa miaka 10. Eti umelaaniwa wewe na kizazi chako.[emoji15] [emoji15] yaani ajabu,maneno yote mabaya anawaambia wanae Wa kuwazaa kabisa
 
Mimi nilipokuwa darasa la kwanza nilimtundika mimba mdada wa form 2. Aisee. Kile kipigo, hata kuhadithia siwezi!
Darasa la kwanza jamani!!!! Au ulianza ukiwa na miaka 15!!!
 
Pole sana
 
Ulizidi utundu mkuu!!! Yaani wazazi wanasema kabisa katafute fimbo... Ukileta ndogo sana eti usiumie ndo wanaenda kuleta komoa, bora ata ulete fimbo ya kweli [emoji4][emoji4]
 
Mzee wangu ni toluuu haswaaa!!! Ko anakukamata mikono yote pamoja na kushughulikia matako!!! Daaah!!! Ukikosea eti uzuie fimbo kwa mkono P.O.P itakuhusu!!! Viboko vyake vilikua vya haja tena vya kuhesabu... Unajua kabisa nachapwa vinne lakini sikalii matako siku mbili
 
Duuh!!! Mama yako atakua alikua na hasira sana
 
Kabisa jamani!!! Mzazi kumpiga mtoto kama mwizi si vizuri kabisa... Wazazi wa siku izi wa kidijitali... Juzi kuna mama amekasirika anataka kumchapa mwanae wa miaka minne, ile kanyanyua fimbo mtoto akaangua kilio cha haja... Mama si akatupa fimbo na kuanza kumbembeleza mtoto, wote tulicheka aisee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hakika huo ni uponyaji endelea kumshukuru Mungu kwa yote aliyokutendea maishani mwako.
 
Mie mama mdogo tulikua tunaishi nae... Sasa kumbe yeye usiku wazee wanavyoenda kulala yeye anatoroka kwenda kwa wanaume na kurudi kabla hakujapambazuka mbaya zaidi anaacha mlango wazi... Baba akastukia mchezo, sa nne binti katoka baba akaweka stuli nje na kumsubiri mpaka alivyorudi... Jamani sijawai ona mzee anahasira kiasi kile... Mama mdogo alitundikwa kwenye mti kichwa chini tena uchi wa mnyama... Mzee alitembeza viboko mpaka mikono ikaanza muuma.
mama mdogo kaolewa na familia yake lakini mpaka kesho anamuogopa baba na hajakanyaga kwetu teena!
 
Hahahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…