Umewahi kuchekeshwa na MC Pilipili?

Umewahi kuchekeshwa na MC Pilipili?

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2010
Posts
4,830
Reaction score
4,729
Habari zenu, kwanza nianze kumpongeza MC Pilipili kwa kupambana, kwa ujumla ni MC mzuri sana tu, turudi kwenye mada.

Mimi ni mdau mkubwa wa vichekesho vya ndani na nje ya nchi yetu. Kimsingi sikumbuki kama kuna siku nimewahi kuchekeshwa na MC Pilipili.

Huwa naangalia vipindi vyake vinavyoitwa vya ucheshi lakini hajawahi kunichekesha hata siku 1, huwezi mfananisha na mtu kama Joti au ile timu ya Mizengwe nk.

Kwa maoni yangu nadhani huyu bwana ni MC na si mchekeshaji au kuna wanao chekeshwa na MC Pilipili?
 
Habari zenu, kwanza nianze kumpongeza MC Pilipili kwa kupambana, kwa ujumla ni MC mzuri sana tu, turudi kwenye mada, mimi ni mdau mkubwa wa vichekesho vya ndani na nje ya nchi yetu. Kimsingi sikumbuki kama kuna siku nimewahi kuchekeshwa na MC Pilipili, hua naangalia vipindi vyake vinavyoitwa vya ucheshi lakini hajawahi kunichekesha hata siku 1, huwezi mfananisha na mtu kama Joti au ile timu ya Mizengwe nk.

Kwa maoni yangu nadhani huyu bwana ni MC na si mchekeshaji au kuna wanao chekeshwa na MC Pilipili?
Hivi aliacha ualimu? Msaidieni arudi kwenye taaluma yake. Anapiga tu makelele.
 
Hakuna kitu anafanya pale, naona anajikakamua tuu comedy ni talanta sio kila mtu anayo, kwaupande wa standup comedy wakenya wapo mbali sana sana tuu, sio kwamba napinga vitu vya kwetu lakini ukweli sijaona mtanzania mchekeshaji sio JOTI, MPOKI, MC PILIPILI, wote hakuna kitu
 
Back
Top Bottom