Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Nimekumbuka Miaka kadhaa iliyopita Wiki mbili kabla ya Siku yangu ya Uchumba na kutolewa mahari nikapeleka kitambaa kwa fundi anitolee Gauni nzuri na mshono ulikuwa simple tu
Akanipa na siku ya kurudi kuchukua nguo bhana, me nikajiongeza nikasogeza siku kadhaa (akamilishe vizuri nguo) nikaenda siku 2 kabla ya uchumba, yoooh nimefika pale kuchukua nguo fundi ananiuliza ulileta kitambaa cha aina gani?
Heeeeeeee Jaman nilitamani kuzimia, nilimwangalia kama vile nimnyongeeeee, niliongea mpaka machozi yakanitoka mwenzenu. Nilikaa hapohapo kitambaa kikaanza kutafutwa kwenye manguo huko ndani ndio aanze kushona huku nasubiria, nguo ilikamilika saa 4 usiku aisee kuanzia saa 9 mchana
Kuna mwingine nilimpa Kitenge ashone koti, siku naenda kuchukua nakuta natoa Gauni, nikagundua Mafundi watakuwa sababu ya miye kwenda Jela aiseeee
Kuanzia hapo mzuka na Nguo za kushona uliisha, mimi na nguo za dukani mpaka Yesu arudi