Enzi hizo nipo kwenye ubora wangu, mechi haichezwi mpaka niwepo, tuna game saa 10, jana yake mazoezini kiatu kikazingua kidogo, asubuhi nikadamkia kwa fundi,
Mimi "fundi eeh, kiatu kinahitajika saa 9, si unajua leo ndio nusu fainali yetu"
Fundi" hapo 1000 tu, saa 7,8 njoo uchukue."
Nikampa buku 2 chenji hana, nikamwambia sio kesi, tufanye yote hiyo yake..
Saa 9 tupo kambini namtuma mtu akachukue kiatu, hajamkuta fundi, naenda mwenyewe fundi hayupo, jamaa wa pale wananijua, wakanipa ruksa ya kupekua, nakuta kiatu hakijashonwa..
Sipendi kumuwazia mtu mabaya, japo tayari nishaumuka, nikajisemea huenda kapata dharura kubwa.
Rudi kambini, tafuta sana kiatu cha kuazima, mie navaa 10.5 ama 11.. Tafuta saana, ikabidi apigiwe mtu simu alete toka karume.. Tukaingia gahara ya kununua kiatu kipya.
Yule kumer saa 5 usiku analeta viatu huku anafoka, nimeenda ofisini kwake nimemuharibia, kumsogelea ana kaharufu kapombe, namuelekeza kuwa nilifanya vile kwa sababu hivi na hivi haelewi yupo juu, namuuliza mbona hukufanya kama nilivyokuelekeza na badala ya buku nilikupa buku 2, mie nahangaikia viatu kumbe umeenda kwenye ulabu, akanijibu nisimpamgie...
Aisee kilinitoka kibao kimoja maridadi, nikapiga kelebu saafi kabisa, kuninuka nikamjaza na ndoo, hajakaa sawa nikalima mtama, kisha nikachukua fimbo ilikuwepo maeneo yale charaza sana, wati wakaja kuamua yakaisha..
Asubuhi polisi hawa hapa, kutizama namuona fundi na maaskari, fundi kavimba uso, alama za mikwaju kibao.
Tukaenda kituoni, kufika tunamkuta mkuu wa kituo, ambae ni number 1 fan wangu kwenye suala zima la kudananda soka.
Afande "Makaveli vipi tena kijana wangu,
Mimi. :sifahamu mkuu, nimeletwa na polisi, kwamba fundi kanisihtaki.
Akaniuliza ilikuwaje, nikamuelezea vizuri tu,
Jamaa akaulizwa ayasemayo makaveli yana ukweli, akajibu ndio yupo sahihi, akaambiwa umekosea wewe, na mimi kosa langu ni kushambulia, jamaa akakiri akasema yeye anataka elfu 30 tu kwenda jitibia, nikakubali ila pale sijabeba hela wala simu sijachukua, twende home nikampe, fundi akagoma, akiogopa ya jana yake, mkuu wa kituo akatoa elfu 10 pale, jamaa akasema hiyo inatosha.
Akaondoka zake, nikabaki na mkuu wa kituo, tukiongea na kunipongeza kwa kiwango kizuri cha jana, akaniambia alipanga kuwa atanipa zawadi yangu na ilikuwa ni 30, sasa pale kaishatoa 10, basi ananipa 20, akanipa 20.
Akaniahidi fainali ikiwa fresh kwa kiwango kile basi kuna 50 yangu, fainali ikawa nyepesi zaidi kuliko nusu fainali, nikajaga kupata 50 yangu.
Yule fundi ikawa heshima na adabu.
Yule mkuu wa kituo alihamishwaga pale, na nikapata taarifa za umauti wake, apumzike kwa amani.