Umewahi kufanyiwa kituko gani na Fundi Nguo (Cherehani) mpaka ukatamani msingefahamiana?

Wewe kumbe mgomvi alaaah
 
Mpuuzi sana yule fundi,miaka ya nyuma kidogo suruali za vitambaa za kushona zilikuwa dili,sasa nami nikaona nianze kuvaa za kushona baada ya kuelekezwa kwa fundi mmoja mzuri,nilipeleka kitambaa cha suruali moja akatoa suruali moja nzuri sana hivyo nikaamua kununua vitambaa vya suruali tano.Kumbe yule fundi akampa mwanafunzi wake kushona suruali zangu.Kwa namna zile suruali zilivyo ilinilazimu kuzigawa zote maana nilikuwa nakasirika kila ninapoziona.Ni zaidi ya miaka 25 sijawahi kushona suruali kwa fundi kwa sababu ya yule mpuuzi.
 
Sista aliambiwa na fhndinkushona nguo 25000. Akaenda kwa fundi kamseleleko akamabia kushona 12000.
Basi akampa advanve 10000 ibakie 2000. Siku anaenda kuichukua sound za kutosha akashona. Asubuhi anatest nguo ile zipu imetatuka pyaaa. Hahahahahaha na fundinhapatikani hewani hahahahahaha.
 
Fundi ambaye alikuwa ananishoneaa nguo Kwa zaidi ya miaka kumi hatimayeee nimemwaga rasmi...dharau alizonionesha zilinitoshaa nikasemaa no enough is enough 🙌 imagine nguo nguo nilimpa Kwa makubalioano ya one week na nguo ilikuwa nivae kwenye tukio na nisare...kabla ya siku ya kuchukuaa siku mbili kabla nikampigia cm akasema usijari sister naelewaa hiloo nguo itakuwa tayari,siku tayari...siku mojaa kabla nikampigia tenaa akaniambia sawaa usijali😅😅siku ya kwenda kuchukuaa kwanza sikumkutaaa kbsa ofisini nampigia cm akaniambia nashonea nyumbanii sister nikasemaa hiii... nikamwambia nguo naivaa keshoo kwenye tukiooo.. Akasema uwahii asubuhii itakuwaa tayari... asubuhii by saa nne nikawa tenaa hapoo ofisini sikumkutaa tenaaa nikampigia tenaa hakupokea cm tenaa na nguoo sikuvaa hiyooo..nilipanic hatarii nikaiziraa hiyoo nguooo nimemuamaa kbsaaaa...Im done na yeye🙌🙌🙌
 
🤣🤣
 
Mafundi wanazingua sana.
Kuna mahali nilikuwa napeleka nguo kushonewa, mmiliki wa ofisi alikuwa na mafundi wazuri sana kwa kushona nguo.

Nguo ya 1, ya 2 hakuna usumbufu, kuna siku nikapeleka vitambaa 2 na kumkuta fundi mwenyewe, boss wake hakuwepo (Mara zote ulikuwa ukipeleka nguo unafanya mawasiliano na boss). Nikawasiliana nae vizuri akampatia maelekezo fundi wake.

Siku ya kufuata nguo imefika nguo hazionekani wala vitambaa..😁
Tafuta tafuta wapi! Kapigiwa simu fundi kuulizwa fundi hapokei simu (Kumbe walikorofishana na boss wake akahama ofisi pamoja na vitambaa vya wateja alivyokuwa amekabidhiwa kushona.

Nikaona hapa nisipokuwa mkali hawa watanichukulia poa. Nikawaambia sitoki hapa ofisini mpaka nikabidhiwe nguo/vitambaa vyangu.

Mwisho wa siku nikapatiwa namba ya fundi nideal naye mwenyewe.
Aisee, nilideal nae kwa vitisho vingi sana mwisho wa siku akafunguka na kunielekeza mahali alipo. Kajichimbia Sinza, humo ndani huwezi kujua kama kuna ofisi. (Nyumba ofisi).

Muda wote huo hata nguo ilikuwa haijashonwa, zile heka heka ndo zikamfanya akate vitambaa. Nilikaa kusibiri amalize nikaondoka na nguo zangu.

Mafundi hawana tofauti na madalali.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 nimevuta picha lipensi nyanya afu lina marinda 🤣🤣🤣🤣🤣 bro umenivunja mbavu
 
Nakumbuka nilipokuwa form six niliibiwa suruali nikabakiwa na pea moja na kwenye mkoa niliokuwa nasoma kulikuwa na baridi Kali kiasi cha nguo kutokauka mapema ukiifua, niliamua kwenda kwa fundi akanishonee suruali nyingine nilimpa robo tatu ya hela yake akaniambia niende kuchukua baada ya siku tatu.
Basi siku ya tatu nilienda kuchukua mzigo wangu nilipofika sikumkuta funda bali nilimkuta rafiki yake mmoja ambaye kila siku anakuwa naye pale anakoshona, nilimwuliza huyo rafiki yake iwapo anafahamu aliko fundi akaniambia ametoka kidogo atarudi baada ya masaa mawili kwa hiyo nikaondoka. Siku ya pili nikarudi na mambo yalikuwa yale yale ya nne nikarudi sikumkuta tena ila nilianza kuchunguza nyumba aliyokuwa anafanyia kazi kama aliweka CCTV Camera ama la lakini nikagundua ameweka bonge la kioo mithili ya ile ya kwenye saluni. Kumbe kile kioo kinaonesha Kila anayekuja kuleta ama kuchukua nguo yake na akiona mtu anaenda kuchukua nguo anajificha.
Nilivyogundua hivyo siku nyingine nilienda ila nikabadili njia yeye kuja kugundua nimeshabisha hodi alipotambua sauti alikumbia chumbani akasimama, kama kawaida yangu nikamwuliza rafiki yake niliyemkuta pale.
MIMI:Fundi yuko wapi
RAFIKI WA FUNDI:Ametoka ila atarudi siyo mda mrefu.
(Kwa sababu jamaa nilimshtukiza hakujificha vizuri, miguu alikuwa inaonekana kupitia chini ya pazia la chumba.)
MIMI:Mwambie siku nyingine akiondoka asisahau kuondoka na miguu yake naona kayaacha pale chini ya pazia la chumba.
Nikaondoka zangu na siku nyingine niliporudi nikakuta ameshamaliza kushona na akanisamehe hela iliyobaki maana alijua nitamwaibisha zaidi.

NI ngori!
 
Mm nilipeleka kitenge anishonee suruali na blause.. siku nimeichukua ile suruali iliishia juu ya magoti haikupita..nikamwambia si ulinipima jamani vzr tuu sasa hiki kiuno kinachoishia miguuni ni kiuno cha nani...
Wanaboa sana..
 
😄😄😄😄
 
Kuna hao wa nguo halafu wengine wa furniture😁😁😁.

Dada yangu alikuwa fundi cherehani,siku moja amekusanya vitambaa vya watoto wa watu wa ubarikio awashonee wavae christmass,kajibaraguza weee,mpaka tareh 24 hajamaliza nguo 3,wale watoto wanazifata usiku nguo bado,waliangua kilio mpaka nikaanza kufeel namna wanavyojisikia,ilibidi akomae na mwanga wa torch ya simu mpaka saa sita usiku maana waligoma kabisa kuondoka..
 
Pole sana mkuu. Huyo fundi wako ni nyoko
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣huu uzi bana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…