Umewahi kufika mikoa mingapi Tanzania na ipi uliipenda zaidi?

Umewahi kufika mikoa mingapi Tanzania na ipi uliipenda zaidi?

Mkoa wa Dar es Salaam ndio baba lao ila, nilikaa Kigoma ni pazuri sana tatizo wenyeji wana mambo ya kiwaki!
Wanakuloga huku wanakupa pole.

Tanga napo ni pazuri ila mzunguko wa hela ni mdogo... Kilimanjaro napo mzunguko ni mdogo... Arusha hadi usome ramani kwa muda mrefu alafu uwe na mtaji wa uhakika... Manyara napo hapaeleweki ila ukipata chimbo lako unabeba mali hadi unakinai.
fungua PM mkuu
 
Kg, Ar,Shy, Simiyu, Mara, mwanza, Tanga Dar Kilimnjaro Manyara

Dodoma Singida
 
1. Kilimanjaro ni home pazuri sana.
2. Arusha ni ujuaji mwingi na unakaa kwa tahadhari muda wote beto ni anytime saa mbili ikukute nyumbani au lodge yenye usalama [emoji16]
3. Manyara pakawaida sana mzunguko wa pesa upo shambani ila amani ipo kiasi. Tatizo kuna mafisi sana, kuliwa na fisi ni anytime ukizubaa usiku hasa nje ya mji [emoji16]
4. Tanga ni pazuri sana kuliko sehemu zote ila tatizo ni mzunguko wa pesa hakuna kabisa.
5.Dar es salaam mitikasi ni mingi.
6.dodoma pakawaida.
7.singida pamezubaa tu
8.morogoro pazuri ila pesa ipo.
9.Iringa pamepoa sana.
10. Kahama pesa ipo ila hali ya hewa chenga.
Nilifika tanga kilichonishangaza ni kuona wachaga ndio wanao i run tanga...sasa nikajiuliza sehemu mpaka ma mamangi wameamua kupiga kambi ina maana pesa ipo au niaje?
 
Arusha
Mwanza
Daresalaam.

Nilipapenda zaidi dar es salaam kwasababu Kuna mzunguko mkubwa WA pesa , hivyo ni jiji zuri kwaajili ya biashara ,masoko yapo kwasababu ya wingi wa watu ....

Lakin pia napenda Hali ya hewa ya Joto ndiyo maana nilipapenda ...

Lakin daresalaam huwezi kukosa vibarua hatakama ulikuwa unafanya Kaz ikaishia njian kupata vibarua ni rahisi ...

Napenda Daresalaam ni jiji la kibiashara Yan pamechangamka Sanaa ,
na MZUNGUKO WA PESA NI MKUBWA .

Arusha Ni mji Wa Gharama Sanaa kuishi
Na Kuna baridi Sanaa
Lakin pia Arusha biashara unafanya strategical hauanzishi tu gafla gafla hivyo sipendelei Sanaa .

Mwanza ni pana Hali ya hewa nzuri lakin pia watu wake ni wakarimu mnoo , watu wenye Upendo Sanaa ,
Shida yake ni kwamba mzunguko Wa pesa ni mdogo Sanaa na pia hata kwenye swala la biashara hakujachangamka kabisa kabisa .... Hivyo sipapendelei Sana pia .
Mwanza mzunguko wa pesa upo tena mkubwa tu! Sijui kipi kilichofanya uone mzunguko wa pesa ni mdogo!
 
1. Kilimanjaro, (Moshi mjini, Same)
2. Mbeya, (Kyela na Mbeya mjini)
3. Iringa ( Mufindi na Iringa Mjini)
4. Morogoro, ( Morogoro Mjini)
5. Pwani, ( Bagamoyo, Mkuranga, Kibaha)
6. Dodoma (Dodoma Mjini)
7. Shinyanga (Kahama)
8. Mwanza. ( Mwanza mjini)
9. Dar es salaam ( Kinondoni, Ubungo)
10. Zanzibar. (Unguja)
11. Njombe. ( Makambako)
12. Arusha. ( Arusha Mjini)

Maeneo mazuri
1. Dar es salaam. ✔️
Huduma za kijamii, Hali ya hewa nzuri, biashara, attitude ya Watu wake, Burudani na starehe.

2. Morogoro. ✔️
Hali ya hewa nzur, Kilimo, na gharama za Maisha zipo Chini.

3. Pwani,
Hali ya hewa, Kilimo, pazuri ku-establish makazi.

4. Kilimanjaro.
Ni nyumbani. Pazuri Kwa kurudi kulia pension Baada ya mihangaiko ya Dunia. Na kusubiri Kifo.

Sipendi maeneo yenye baridi Kali kama Mafinga na njombe,

Sipendi maeneo yenye joto na jua Kali kama Dodoma, Kahama, Same n.k
 
Arusha
Mwanza
Daresalaam.

Nilipapenda zaidi dar es salaam kwasababu Kuna mzunguko mkubwa WA pesa , hivyo ni jiji zuri kwaajili ya biashara ,masoko yapo kwasababu ya wingi wa watu ....

Lakin pia napenda Hali ya hewa ya Joto ndiyo maana nilipapenda ...

Lakin daresalaam huwezi kukosa vibarua hatakama ulikuwa unafanya Kaz ikaishia njian kupata vibarua ni rahisi ...

Napenda Daresalaam ni jiji la kibiashara Yan pamechangamka Sanaa ,
na MZUNGUKO WA PESA NI MKUBWA .

Arusha Ni mji Wa Gharama Sanaa kuishi
Na Kuna baridi Sanaa
Lakin pia Arusha biashara unafanya strategical hauanzishi tu gafla gafla hivyo sipendelei Sanaa .

Mwanza ni pana Hali ya hewa nzuri lakin pia watu wake ni wakarimu mnoo , watu wenye Upendo Sanaa ,
Shida yake ni kwamba mzunguko Wa pesa ni mdogo Sanaa na pia hata kwenye swala la biashara hakujachangamka kabisa kabisa .... Hivyo sipapendelei Sana pia .
Hakuna sehemu yenye mzunguko mkubwa wa pesa na utajiri wa haraka kama Mwanza na Dar, na unaposema Mwanza hakuna mzunguko wa pesa labda ulienda Mwanza ya Namtumbo.
 
Kuna mikoa ambayo nimeishi (miezi 6 na kuendelea) halafu kuna ile ambayo nimetembelea tu nikakaa siku mbili tatu
Niombe - ndio nyumbani, napapenda kwa sababu hakuna njaa
Iringa - Naona kama pamepoa sana

Songwe - huku nako hakuna njaa, ardhi yake inakubali mazao mengi ya chakula na biashara...hali ya hewa pia sio mbaya

Songea - Hali ya hewa nzuri, mimi kule viazi tu [emoji4]

Dar - hata sijui nipaelezeeje, sipapendi kihivyo ila panaitwa mtakuja

Mbeya - ni pazuri kwa urahisi wa maisha ila hali ya hewa ile ya upepo siipendi

Mtwara - niliona kama pakame sana, pengine kwa sababu nilifika kwa muda mchache sikupata nafasi ya kuzunguka

Arusha - ni pazuri ila mimi siwezi kuishi

Morogoro -
 
Sumbawanga (Rukwa)
Songwe
Kigoma
Katavi
Tabora
Iringa
Dodoma
Singida
Shinyanga
Morogoro
Pwani
Dar
Njombe
Geita
Kati ya mikoa hiyo apo mkoa nilioupenda ni Rukwa mzunguko wa pesa ni mdogo ila kuna fursa kibao
 
Back
Top Bottom