Umewahi kufika mikoa mingapi Tanzania na ipi uliipenda zaidi?

fungua PM mkuu
 
Kg, Ar,Shy, Simiyu, Mara, mwanza, Tanga Dar Kilimnjaro Manyara

Dodoma Singida
 
Nilifika tanga kilichonishangaza ni kuona wachaga ndio wanao i run tanga...sasa nikajiuliza sehemu mpaka ma mamangi wameamua kupiga kambi ina maana pesa ipo au niaje?
 
Mwanza mzunguko wa pesa upo tena mkubwa tu! Sijui kipi kilichofanya uone mzunguko wa pesa ni mdogo!
 
Tanga kule korogwe milimani utafikiri uko Norway hali ya hewa safi kabisa
 
1. Kilimanjaro, (Moshi mjini, Same)
2. Mbeya, (Kyela na Mbeya mjini)
3. Iringa ( Mufindi na Iringa Mjini)
4. Morogoro, ( Morogoro Mjini)
5. Pwani, ( Bagamoyo, Mkuranga, Kibaha)
6. Dodoma (Dodoma Mjini)
7. Shinyanga (Kahama)
8. Mwanza. ( Mwanza mjini)
9. Dar es salaam ( Kinondoni, Ubungo)
10. Zanzibar. (Unguja)
11. Njombe. ( Makambako)
12. Arusha. ( Arusha Mjini)

Maeneo mazuri
1. Dar es salaam. ✔️
Huduma za kijamii, Hali ya hewa nzuri, biashara, attitude ya Watu wake, Burudani na starehe.

2. Morogoro. ✔️
Hali ya hewa nzur, Kilimo, na gharama za Maisha zipo Chini.

3. Pwani,
Hali ya hewa, Kilimo, pazuri ku-establish makazi.

4. Kilimanjaro.
Ni nyumbani. Pazuri Kwa kurudi kulia pension Baada ya mihangaiko ya Dunia. Na kusubiri Kifo.

Sipendi maeneo yenye baridi Kali kama Mafinga na njombe,

Sipendi maeneo yenye joto na jua Kali kama Dodoma, Kahama, Same n.k
 
Hakuna sehemu yenye mzunguko mkubwa wa pesa na utajiri wa haraka kama Mwanza na Dar, na unaposema Mwanza hakuna mzunguko wa pesa labda ulienda Mwanza ya Namtumbo.
 
Kuna mikoa ambayo nimeishi (miezi 6 na kuendelea) halafu kuna ile ambayo nimetembelea tu nikakaa siku mbili tatu
Niombe - ndio nyumbani, napapenda kwa sababu hakuna njaa
Iringa - Naona kama pamepoa sana

Songwe - huku nako hakuna njaa, ardhi yake inakubali mazao mengi ya chakula na biashara...hali ya hewa pia sio mbaya

Songea - Hali ya hewa nzuri, mimi kule viazi tu [emoji4]

Dar - hata sijui nipaelezeeje, sipapendi kihivyo ila panaitwa mtakuja

Mbeya - ni pazuri kwa urahisi wa maisha ila hali ya hewa ile ya upepo siipendi

Mtwara - niliona kama pakame sana, pengine kwa sababu nilifika kwa muda mchache sikupata nafasi ya kuzunguka

Arusha - ni pazuri ila mimi siwezi kuishi

Morogoro -
 
Sumbawanga (Rukwa)
Songwe
Kigoma
Katavi
Tabora
Iringa
Dodoma
Singida
Shinyanga
Morogoro
Pwani
Dar
Njombe
Geita
Kati ya mikoa hiyo apo mkoa nilioupenda ni Rukwa mzunguko wa pesa ni mdogo ila kuna fursa kibao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…