Umewahi kuingilia ugomvi usiokuhusu halafu yakakukuta makubwa?

Mi niliamulia ugomvi wa gelofriendi wangu na shosti yake enzi hizo. Baada ya wiki mbili shosti wa gelofriendi wangu akanizawadia papuchi kama shukrani ya wema wangu.

Tangu siku hiyo niko makini sana kufuatilia gomvi za jinsia KE. Huwezi jua mipango ya shetani, naweza nikalamba bingo tena

Mzigua90 na Shunie mtagombana lini nije niwaamulie?
 
Hahaha kwahiyo ugomvi wa Humble na CCNP kwako hauna faida?
 
Kuna mpangaji mwenzangu ana mke na mtoto mmoja nahisi ni wa miaka minne yule mtoto.

Jamaa shughuli zake ni ufundi, kwahiyo akitoka kurudi usiku sana. Siku hiyo kawahi kurudi akakuta mkewe kapakatwa na kinyozi mmoja hivi barabarani. Jamaa hakuongea kitu.

Alfajiri ya saa 10 kelele za 'Nakufaaaaa' zikaanza. Mimi nakaa chumba cha nje miongoni mwa vyumba vitatu vya nje hawa mke na mume wanakaa vyumba vya ndani.
Hadi uingie ni lazima ufunguliwe mlango.

Basi washkaji wa vyumba vitatu wote tumetoka tunamsihi jamaa amuache binti. Huku tukwapigia kelele wa vyumba vingine wafungue. Mmoja wetu akaenda dirisha la mwenye nyumba ili afungue mlango.

Nikaona wanachelewa nikaanza kupiga mateke mlango. Bwana muvi zinadanganya kumbe mlango ni mgumu baada ya mateke kama nane nikaona nitajivunja nisubiri kwanza.
Mwenye nyumba akafungua mlango nikatangulai kufika mlango wa chumba cha jamaa. Kama kawaida yangu mateke tu, nabadilisha miguu tu.

Yule jamaa alivyofungua mlango akatoka ni kisu akanichana kwenye triceps kidogo coz niliwahi kutoa mkono. Binti akapata upenyo wa kukimbia mi nikamtight mshkaji akanyang'anywa kisu.

Mchana nimelala nagongewa na watu kama wanne natoka askari kanzu watatu, mmoja ana sare na yule jamaa. Jamaa anadai nimempiga asubuhi. Nikabebwa hadi kituo kidogo.

Mwisho askari wakasema ok huna kosa unatuachaje? Ikanitoka 20K narudi nyumbani mwenye nyumba ananiambia mateke yangu yamemharibia milango hivyo natakiwa nigharamie ama milango mipya au ile iboreshwe.

Mie hoi.
 
nakumbuka mwaka 2013 life la chuo na ujana damu inachemka kila weekend club..

tulikuwa washkaj watatu mimi gatsby..bruno..na masai mmoja tulikuwa tunamuita pede

tumekula bia za kutosha pale Club Wantansh kwa nje mida ya saa saba na nusu usiku tukasema ngoja tuzame ndani kubambia na ikiwezekana kung'oa wadada wa masaki (maana kama mara mbili mimi na bruno tulitunukiwa na wadada wakubwa wakubwa kiumri baada ya kudance nao)

ile tumezama ndani tukaanza kucheza huku tunaendelea kula bia ikafika mida ya saa 8 na nusu yule mwenzetu masai pede akazima tukamuweka kwenye sofa sisi tukaendelea kula maisha

gafla tunaenda kumchek tunakuta anakula mate na lishoga jamaa hajielewi hapo anajua kaopoa demu nikamwita bruno tukaenda pale cha kwanza hatujauliza tukampa yule shoga vibao vya maana ..akasepa

gafla karudi na mashoga wenzake kama sita wametujalia pale kwenye sofa wanaanzisha utata mmoja akasema au mnamuonea gere mwenzenu na nyie mnataka au? gafla akamrukia bruno akambusu mdomon mamaaeee akaachia bonge la ngumi yule shoga chali

hata mabaunsa walipotokea wakaanza kutupa za chemba mimi na bruno wakatubeba juu juu wakaenda kututupa nje hapo tumechezea za uso tumevimba

kumbe bwana meneja wa pale wantanshi anapenda mashoga yawepo mule ndan ili kuvutia wazungu waje pale...

kesho yake hatukwenda chuo maana bado tulikuwa tumevimba yule maasai pede tunamsimulia kisa kilichofanya tupigwe anabisha eti kuwa ajaliwa mate na shoga 😂😂😂

anasema aseee nyie jamaa makorofii sana jana itakuwa mmepata wababe yenu imewaonesa kazi
 
Hahaha mngetoka nduki
 
Iyo inaitwa "KUNUNUA UGOMVI"
ebwana kuna jamaa alinunua ugomvi wa rafiki ake aliyekua anapata kichapo na raia wenye hasira kali...

Jamaa katokea from nowhere kanunua ugomvi...akitegemea ataungana na yule aliyekua anapigwa..

Basi bwana yule aliyekua anapigwa kapata lifetime chance akachomoka akamuacha mnunuzi......

Ebwana zile Raia zikamshuhulikia yule mnunuzi wa ugomvi kwa kipigo cha mbwa mwizi!

Akaapa kamwe hatakaa anunue ugomvi tena maana aliingia kwa nia njema ya kumuokoa rafiki ..rafiki akamkimbia..

Akazidi kusema kua ."......kwa kumsaidia mtu kama anapigwa eti ataenda kutoa taarifa nyumbani kwao kua ndugu yenu anakufa kule kaamueni.."

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu kipigo cha mtu anayeingilia hua kinakua cha mwana ukome ili siku nyingine usirudie
 
ilikuwa ambush kaka [emoji23][emoji23] sisi tupo bize tunawapiga wale mashoga gafla mbavu zimeingia bila hata kuuliza tukaanza kuchezea ...tulivyoona hawa hatuwawez tukajilaza chini ndio wakatubeba wakatutupa nje
[emoji23] [emoji23] [emoji23] hilo ambush si mchezo unaweza kuona unakimbia unawaponyoka kumbe ndo unaelekea upande wao
 
Ulikuwa mdoogo km piriton

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sele bujeeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…