Umewahi kuingilia ugomvi usiokuhusu halafu yakakukuta makubwa?

Wewe jamaaa umefanya j.mosi yangu iwe nzuri
Asantee kwa hadithi yako nzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha sele buje noma
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] mwanangu stor zako umenkumbusha stori za baba ubaya enz hzoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hahahahahaaa eti Sele Buje,,[emoji3] [emoji3] [emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hahahahah,, dah yan apo kwnye kubadilisha miguu kupiga mateke mlago km kwny muvi mm hoiiii[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2006 kuna mwanangu wa dhahabu (R.I.P hommie) alikua anapiga kazi kwenye supermarket ya wazungu sasa mazoea ya utoto wa mtaani mwanangu ikawa daily anakwara bidhaa fulani muhimu anatuletea wanae maskani iwe bure au kwa bei ya chini ikawa neema kwetu kuliko maelezo,kumbe kuna mkolombwe mmoja alikua anapiga nae kazi akashtukia mchezo,siku mwana kavusha mzigo yule jamaa na mwenzie wakamtaiti nje tu ya ofisi wakampa option ya kuachiwa mzigo au wakaseme kwa watasha mwana aka-surrender akawapa mzigo walivyo wakuda wakampa kibano kikali sana na vitisho juu.
Basi swahiba kaibuka uswazi akatupa mkasa huwezi amini watu 4 tukasema kesho tuna dili na uyo bwege kweli tukaibuka super-market tukasubiri anachomoka na sisi tukazama nae kwenye daladala iyo iyo basi kushtuka jamaa kashuka Mtogole pale nasi tukashuka hatukumsogeza mbali tukampa kibano tukiwa na swahiba wetu kumbe yule mbwee kwao sio mbali si akapiga kelele za wezi wananiua sijui maraia walitokea wapi ila nilijiona nina kundi la watu nyuma yangu wana jazba haswaaaa na mitaa siijui nikazama kwenye jumba bovu moja nikapokelewa na wahuni wanakula kaya uku wanacheza kamari ile wakanituliza tayari raia wako nje jamaa wakaniuliza kulikoni nikawapa mkasa basi mtabe 1 akatoka kuwasambaratisha raia nikatulizwa kama saa 1 mle ndani wakaniambia unaelekea wapi usindikizwe duh huwezi amini niliwacheulia wale jamaa mapene yangu yote nikabaki na nauli kwa shukrani wakanipitisha vichochoroni mpaka kituo kingine nakadandia chuma mpaka home,uwoga ukawa kusema kuhusu wale wenzangu ila nashukuru mpaka kufika usiku wote tulikua salama ingawa kila mtu alitimkia kwake.
 
Mkuu umenikumbusha miaka 8 iliyopita, ilikuwa mdogo wangu anapokea kipondo kutoka kwa baunsa flani kwa kumtusi mke wake basi mm kuona mdogo wangu anapokea kipondo nikaumia sana na kama ujuavyo "damu nzito kuliko maji" , si ndo nikajitosa ulingoni kumpiga tafu dogo ili baunsa tumchape kwa ushirika!! Ile napanda tu ulingoni kupiga tafu basi dogo akarudi benchi na kuniachia msala ulingoni.. Kipigo nilicho pokea anajua muumbaji. Ila sikujutia kumtetea dogo japo nae nilim-mind balaa.!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu Mwenyekiti,

Ilikua MARCH 2016 usiku wa kuamkia jumapili.

Wiki hiyo yote nilikua na misukosuko ya kutosha, basi kama zali weekend hiyo ikawa ni birthday ya shemeji yangu(mdogo wake wife)- halafu huyu shemeji yangu ni maarufu wengi humu wanamjua ila sitomtaja.

Sasa wao wakaamua birthday ikafanyiwe pale "Bulls" survey njia ya kwenda UDSM, sasa pale home kwenye friji nilimnunulia wife castlelager kama 6 hivi 1week before, ila hakunywa, tulikua tunaishi na dogo mmoja hivi anatusaidia kazi pale home, sasa hiyo jumamosi mida kama ya saa 11jioni kupitia kwenye friji nikakuta zile bia, wife akasema hana mzuka nazo(alikua na ujauzito wa kama wiki 6 hivi) nikaona siyo issue nikamwambia yule dogo anayetusaidia kazi azipige.. dogo akazifakamia akachangamka kichizi.

Mida ya saa tatu usiku safari ya kwenda Bulls kwenye birthday ikaanza, tulipofika pale kwakweli palikua "pamenoga sana", tukaendelea kuvesha, wakalishana cake pale mambo yakaendelea . Kipindi hicho mimi nilikua nakunywa " vikali" sasa pale nilikuta watu wanavesha "nyagi dry" mzee baba "nikaliunga", hapo tulienda na yule dogo wa kunisaidia kazi, kichwani alikua na castlelager 6 tayari, alipoiona nyagi akawehuka na yeye akaendelea kuvesha, alikua anahamu nazo sana maana alikua anakunywa kwa kujifichaficha pale home nisijue ila mimi nilikua nishajua huyu dogo nae ni mkata maji mzuri tu so nilipompa huo "uhuru wa manyani" akawa so excited.

Hapo kama siku mbili zilizopita wife aliniambia kuwa Boyfriend wa mdogo wake-huyu birthday girl wetu ambaye ni shemeji yangu ameoa. Yaani jamaa ni mume wa mtu ila hajamwambia ukweli huyu binti, so binti hajui lolote anajua huyo ndiye future husband wake, lakini daily walikua wanagombana binti anaforce apajue nyumbani kwa jamaa maana jamaa kajenga goba ila jamaa anamchomolea kumpeleka kwake wanaishia kwa binti tu, hapo jamaa anaprovide kila kitu kwa binti.

Sasa kumbe wife alifanikiwa kuijua hiyo siri kupitia "washakunaku" faster akamwambia mdogo wake ukweli wa mambo kuwa jamaa kaoa, ni mume wa mtu zaidi ya miaka miwili, mdogo mtu akatafuta perfect time ya kuanzisha ugomvi, na kwa timing zake akaona siku hiyo ya birthday ndo aliamshe dude.

Basi bwana turudi pale Bulls, shughuli ilikua inafanyikia ndani mule kuna club, Tulilewa, Tukalewa, Tukalewa- Yesu wangu! Ukafika muda wa kuondoka, ilikua kama saa tisa hivi usiku, tokatoka nje pale, tupo kama watu 10 hivi, wakati huo yule dogo niliyotoka nae home alikua kazima kama mida ya saa nane hivi so nikampeleka kwenye gari nikamlaza seat ya nyuma.

Tukiwa pale nje kwenye parking tunataka kuagana varangati likaanza! Plan yangu ilikua nimpakie shemeji na boyfriend wake nikawadrop kwake(sinza) halafu sisi turudi home Africana-mbezi. Hapo mimi nilikua sijajua kama kuna mkakati wa kuliamsha dude, mara naona wanajizungusha, nikamwambia wife twendeni basi muda unaenda tukapumzike nimechoka, mdogo mtu akadakia, akasema kwa sauti kubwa mbele ha madereva tax na bodaboda "Shem yaani leo nataka nikalale kwa mume wangu, nataka akanit.o.mbeeeeee mpaka nijisikie kuwa leo kweli nim.et.ombwaaa", DAH..!!! kusikia vile madereva tax wakalipuka kwa makelele oyooooooo.... noma ... noma !!
Nikageuka kumtazama yule boyfriend wake nikaona anatabasamu lakini ni kama anahofu sana, akili ika'click kwamba hapa wanataka kumletea jamaa zengwe waende kwake waka'prove kama kweli jamaa kaoa au la!

Nikasema ngoja nimuokoe mwanaume mwenzangu, hapo wote tumelewa isipokua huyu boyfriend-ake. Wakati huo yule dogo kwenye gari katapika nyongo seat za nyuma huwezi kuzitazama mara mbili.. Nikamwambia Shemeji yangu, " Shem skia, kwasasa ngoja niwapeleke sinza, pakikucha mtaenda home kwa jamaa" akajibu "hapana, haiwezekani kila siku yeye hataki nipajue kwake, sasa nasema hivi hapa kama tunaondoka safari ni goba, siendi popote zaidi ya kwake", hapo kuna nyomi lishatuzunguka, nikaona ngoja nimvute pembeni nimpige darasa atanielewa tu, ile kumshika mkono tu wife nae akadakia "unataka uk.a.mt.ombe wewe?, unaingilia nini wewe yanakuhusu?"

Nilimrukia nikamlima kofi moja akaanguka chini, akanyanyuka mzimamzima akaniparamia mzee baba nikajikuta chini akanikalia kifuani halafu sasa yeye ni "giant" nikajikuta nashindwa kunyanyuka, akaniparua na kucha + ngumi, mzee baba nikaona fedheha gani hii tena, nikajikaza kiume nikampindua nikainuka, sasa nikaamua ngoja niende kwenye gari nisepe niwaache, ile nashika kitasa cha gari nilivutwa mpama chini tena, tulibiringishana pale mpaka akanichania vifungo vyote vya shati nikabaki vest nje.

Akafanikiwa kunitight vizuri sana, kila nikijaribu nikaona hii issue inakua series sasa nikaanza kumvesha ngumi, lakini kwakua nilikua tungi kila ngumi ninayompiga nikaona haimuingii, nikamng'ata mkono akashtuka kidogo hajakaa sawa nikamtia meno ya mgongo tena halafu nikainuka yeye yupo chini analia, nikaenda kwenye gari nikaweka D safari, hapo yule shemeji yangu, mumewe na marafiki wengine wanahangaika hawajui cha kufanya,! kufika pale calabash roho ya huruma ikanijia nikakumbuka pale alipo mbuni kipande hana, atafikaje home, nikapiga u-turn kupitia ile service road nikawakuta wote kwa pamoja wanatembea mdogo mdogo, nikageuza gari nikamwambia panda twende, akagoma nikashuka kwa hasira nikaanza kumburuta washkaji wanania muache tu uaimfanyie hivyo nikawaambia kama kweli mnamuhurumia nisaidieni kumbeba tumuweke seat ya nyuma, nikaweka ile child rock ya milango ya nyuma maana alikuwa na tabia tukizinguana tukiwa kwenye gari anafungua mlango ili kuruka.Basi tukambeba pale tukamuweka nyuma na yule dogo, nikatia gia safari.. Mpaka leo wife ana alama ya meno mkononi, ya mgongoni ilishafutika.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Supavaiza [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…