Suala la uongozi siyo kuvaa suti kali na kuongea maneno makubwa kubwa kama
"uchumi unakua kwa kishindo" huku mfukoni mwako panya anazalia. Uongozi ni heshima, ni akili, na zaidi ya yote... ni
mtindo wa maisha (lifestyle)
View attachment 3701076
Huwezi kuwa kiongozi aidha Mbunge ama Diwani halafu mtindo wako wa maisha unafanana na drama za kina
Chumvi nyingi ama
Ngoma Nangwa. Sidhani kama kuna jamii ambayo inataka kuwa na viongozi wajinga wajinga.
View attachment 3701077
1. Akili Kubwa, Sio Akili Kisoda!
Kiongozi wa ukweli anatakiwa kuwa na
maono (vision) na siyo kuamka asubuhi na kusema,
"Leo ngoja nikakate gogo kisha nichambie gazeti." Hakuna kitu kinachosikitisha kama kiongozi anayepelekwa na upepo wa mitandao ya tiktok na Instagram au yule anayeingia kwenye kikao bila kusoma taarifa. Tukitaka viongozi wajinga, tutaishia kuambiwa foleni za magari barabarani ni ishara kwamba wananchi wana pesa nyingi!
View attachment 3701081
2. Mtindo wa Maisha (Lifestyle) Uwe mtu timamu.
Mtindo wa maisha wa kiongozi sio tu kuhusu kuendesha gari la kifahari; ni kuhusu
nidhamu, muonekano, na ustaarabu:
View attachment 3701079
Muonekano na Nidhamu: Kiongozi hawezi kuonekana upo unalewa Club mpaka saa nane usiku ukiwa unapiga nduru halafu kesho yake upo na Mkutano na wananchi! Mtindo wako wa maisha lazima uakisi mtu mwenye kujitambua, anayejiheshimu na anayeheshimu muda wake.
View attachment 3701080
Afya na Akili Timamu: Unakula nini? Unasoma nini? Unajumuika na akili za aina gani? Kiongozi anayetumia muda wake mwingi kwenye uhuni na masuala ya kipuuzi ni mtu waa ajabu sana, yaani kuliko kujisomea namna ya kuwa bora yeye ndio anatuongoza kuelekea shimoni kwa tabasamu kabisa!
View attachment 3701078
3. Kauli na Staha (Sio domo Taka)
Mdomo wa kiongozi ni sawa na pressure ya ndege. Ukitukana au ukisema vitu vya ajabu ajabu, siyo wewe tu unaanguka—unaiangusha na jamii nzima! Kiongozi bora ana busara, anajua wakati wa kuongea na wakati wa kusikiliza. Sio mtu anayeingia kwenye mabishano ya kitoto kwenye magroup ya WhatsApp! Sio mtu wa kutafuta trend ili uonekane ni mtu wa maana.
View attachment 3701079
Tukubaliane kitu kimoja:
Uongozi siyo mchezo wa bahati nasibu. Tukiruhusu viongozi wajinga watualike kwenye maisha yao ya ovyo, tutaishia kupiga makofi huku nyumba yetu inateketea kwa moto!
View attachment 3701081