Umewahi kukaa sehemu na ukahisi kama hiyo sehemu uliwahi kukaa zamani 'DEJAVU' already seen?

Nilipofika Tanga Mabawa mara ya kwanza niliona nimeshawahi kufika na kwenda kwa mwenyeji wangu bila kuongozwa
Nastaajabu sana.
 
Hii nimewahi kuisoma Mara nyingi Ila Leo nilijaribu Ku-trace maisha yangu na kuiona hii Dejavu
Mkuu DR HAYA LAND DeJavu huiitrace ni Ile hisia ambayo inakuja gafla msome vizuri Minjingu Jingu hapa chini hii ndio maana halisi ya DeJavu.
 
mwisho wa siku unakuta watu kama hawa ndo wanashupashaza shingo kudai elimu ya kayumba ndo bora zaidi,,,nimepata shida sana kuelewa kinazungumzwa nn apa. naona tu neno dejevu dejevu dejevu kumbe unaunaongelea neno DEJA VU!?daah we jamaa😳 umeshindwa hata kufuatisha walivyoandika kwenye iyo karatasi apo?🚮
 

Hizo nafsi huwa zinasafiri muda gani tukiwa ktk utambuzi au tukiwa usingizini?
 
Hii kitu ni kweli aisee! Kuna siku unakuta kila unachofanya au kinachotokea unaona inafanana kabisa na siku fulani ambayo umeshaiishi hapo kabla. Yaani karibia kila kitu. Huwa inanishangaza sana.
 
Hii khali huwa inanitokea mara moja moja.
Kinaweza kufanyika kitendo lakini kumbukumbu zangu zinanijulisha kuwa haya ni marudio, hiki kitu umewahi kukishuhudia kabla.
Kweli kabisa. Huwa inanishangaza sana Aisee!
 
Mimi iliwahi kunitokea nilienda mkoa ambao sijawahi kwenda tangu nizaliwe lakini kuna mahali nilikuwa nikifika najihisi niliwahi kufika kabisa tena zaidi ya mara moja.
Nilikuja kugundua niliwahi kuiota hiyo sehemu zaidi ya mara moja kabla sijaenda mkoa huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…