Umewahi kukumbwa na janga gani chuoni mpaka ukapaona chuoni kuchungu?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Katika harakati za kusaka elimu vyuoni wanafunzi wanakutana na kashikashi nyingi sana zinazosababisha wakati mwingine mpaka mtu kuachana na mambo elimu, mfano kujikuta uko kwenye mgogoro na mwalimu wako sababu wote mnamfukuzia binti fulani, kufanya starehe kwa kupitiliza mpaka unasahau kilichokupeleka ni baadhi ya kati ya mengi.

Je ulishawahi kukutana na kisanga gani mpaka ukapaona chuoni kama uwanja wa vita? Uliweza kurudi kwenye mstari au mpaka leo bado ni majuto tu?
 
Mimi nishawahi kula Ada na mtihani unakaribia.
 
Nasoma komenti

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Nilipata sup ya negotiation n mediation halafu mkufunzi mtata ukikata rufaa anaku mind mara 2

Mwamba nikakata rufaa, jamaa wakija kwangu wanasema mkufunzi haniachi aseeh lazima anile kichwa tena na tena

Nilikuja kuchomoka, tangu hapo nikaacha ubwege
 
Mimi nilikuwa mtu nisiependa kusoma tokea niko mdogo mpaka kufika chuo kikuu japo nilipokuwa mdogo nilikuwa sipendi kusoma na sikiwahi kufeli..

Nilivyofika chuo na ule u free mwingi Mimi ndio nilikuwa mtaalamu wa movie mpya mpya, nikapanga gheto nje yani habari za chuo sina quiz washikaji wananifanyia. Naenda chuo usiku kudownload movie tu.

Chuo niligraduate na GPA ya 1.9 hata sijutii.
 
Nilipata sup ya negotiation n mediation alafu mkufunzi mtata ukikata rufaa anaku mind mara 2

Mwamba nikakata rufaa, jamaa wakija kwangu wanasema mkufunzi haniachi aseeh lazima anile kichwa tena na tena

Nilikuja kuchomoka, tangu hapo nikaacha ubwege
Hongera kwa kuchomoka
 
Mimi tukio la chuo ambalo sitolisahau ni mwaka wa kwanza.

Hostel room tulipangwa wa 4. Sasa mambo ya kike tena roommates wangu watatu wakaungana wakaninunia halafu wakawa wananipiga vijembe live. Wakavuka mipaka wakawa wananiharibia vitu vyangu. Mfano, nikitanyika kitanda wanatoa shuka na kuvuruga nikiwa sipo.

Sasa hiyo siku kama Mungu. Naenda class nikawa nimesahau notes room. Nikarudi kabla hata sijamaliza kushuka ngazi. Nikavikuta vinavuruga vitu vyangu.

Hasira ilinipanda nikaona liwalo liwe. Nikakamata mmoja nikamtembezea kichapo wakaingilia wale wawili. Nikawachanganya wote. Nikawapiga wote. Yaani walinichangia watatu lakini walichapika haswa hadi vikakimbia nje vingine havijavaa hata nguo.

Baadae warden akatuita tukatakiwa tufukuzwe hostel.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚ wazee wa staki shule
 
Gpa ya 1.9 si umedisco?
 
Dah, pole sana
 
Tulipogundua kwamba chuoni hawana kawaida ya kufuatilia watu waliofeli(discontinue) tukaunda team ya watu kama saba na kutengeneza vitambulisho fake vya watu walifeli kuendelea na masomo mara tu baada ya orodha kutoka ubaoni kuonyesha kweli wamefeli.

Kweli tukafanikiwa kuchukua zile pesa dirishani (enzi hizo pesa haitumwi kwenye benki account) na kugawana kadri ya ushiriki wa kila mmoja wetu. Kasheshe ilikuja baada ya mmoja wa waliofeli kujitokeza kupinga kuwa hajafeli (kukata rufaa) na kukuta pesa yake imechukuliwa.....ilikuwa mbaya maana yule aliyechukua pesa alikuja kujulikana na kusimamishwa masomo na kutakiwa kuzirudisha pesa zote.
 
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ mjini mipango
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…