Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 38,657
- 44,759
Tulikuwa ukumbi wa cenema, nikaenda toilet, wakati narudi umeme ukakatika nikapapasa seat mpaka nikaikuta moja blank nikidhani ni pale nilipokuwa nimekaa kumbe nimekaa na female Dean of students, nikawa naendeleza story nikijuwa niko na mdau wangu, umeme uliporudi 🙃😷🥵Katika harakati za kusaka elimu vyuoni wanafunzi wanakutana na kashikashi nyingi sana zinazosababisha wakati mwingine mpaka mtu kuachana na mambo elimu, mfano kujikuta uko kwenye mgogoro na mwalimu wako sababu wote mnamfukuzia binti fulani, kufanya starehe kwa kupitiliza mpaka unasahau kilichokupeleka ni baadhi ya kati ya mengi.
Je ulishawahi kukutana na kisanga gani mpaka ukapaona chuoni kama uwanja wa vita? Uliweza kurudi kwenye mstari au mpaka leo bado ni majuto tu?