Umewahi kukumbwa na janga gani chuoni mpaka ukapaona chuoni kuchungu?

Umewahi kukumbwa na janga gani chuoni mpaka ukapaona chuoni kuchungu?

Sikulipa ela ya chakula, sasa wakati wa kusaini clearance form kuna pengo sehemu ya chief warden. Ilibidi niingie mtaani kufoji muhuri wa chief warden na saini yake. Bahati nzuri hawajastuka mpaka wakati wa graduation.

Hii ilinifanya hata caution money nisiifatilie kwa uoga wa kustukiwa kwenye huu msala wangu.
 
Nilikua na shida zangu hiyo siku nikapunguza laki nzima kwenye ada. Niliposoma sista angu alikua lecturer pale pipo kibao wananijua hii kitu ilikua inaniboa sana. Siku kaingia uhasibu wakamcheki bwana vipi mbona dogo hajalipa ada sista akanipandia hewan vipi umelipa ada nikamuambia ndio nshalipa akaniambia fresh.

Weee badae moto uliwaka hadi home maza nae kanipandia hewan kidogo mara broo nae kapanda hewan aah wee nilikoma hapo sina kabisa hiyo laki na sijui naitoa wapi na bado week 1 moja pepa nilikoma. Nilikua na kaboyfriend pale pale chuo ndio dk za mwisho akatafuta hiyo hela nikalipa.
 
Katika harakati za kusaka elimu vyuoni wanafunzi wanakutana na kashikashi nyingi sana zinazosababisha wakati mwingine mpaka mtu kuachana na mambo elimu, mfano kujikuta uko kwenye mgogoro na mwalimu wako sababu wote mnamfukuzia binti fulani, kufanya starehe kwa kupitiliza mpaka unasahau kilichokupeleka ni baadhi ya kati ya mengi.

Je ulishawahi kukutana na kisanga gani mpaka ukapaona chuoni kama uwanja wa vita? Uliweza kurudi kwenye mstari au mpaka leo bado ni majuto tu?
Nilipata maksi za umri wa mtoto kwenye EG106 ya Dr. Ishengoma wakati huo first year FoE ya UDSM na ME207 ya Warioba Second year ya FoE UDSM. Niliona chuo kichungu sana wallah..!!
 
Back
Top Bottom