Usile ADA HAILIPIKI. Mimi nilijaribu hapo ndipo nilijua nani rafiki na nani adui. Pia hapo nilijua nina ndugu wa namna gani. Chuo kilinicheleweshea bumu sasa hela ya kuongezea ada nikaila maana home wasingenielewa kuwaambia naomba hela ya kula. Mpaka inafika siku ya mitihani bado hela haijasoma so nikaenda kwa Dean of School akaniandikia barua nikapewa examination card nikafanya pepa. Hela ikatoka nipo home nikatumia kama laki nikijifariji hela ya field ikiingia nitalipa. September conference ikaniita nafika kigezo ni kuingia ni kulipa ada. Hapo sina nina laki nne na nusu tu we nilikoma. Piga simu zote watu hara hawapokei yani. Mshkaji mmoja rafiki yangu na yeye akashikwa akaja kufanya mtihani. Anakuja maza ake akamtumia hela ya kula kwenye simu nakumbuka tu alinipa simu akaniambia mwanangu kalipe ada. Nikatoa ada nikalipa ada halafu nikarudi tena bro sina hela ya kula. Mwana alinilisha wiki mbili. With that he became my brother. Hata leo alinipigia simu nina tatizo hili naomba msaada i don’t think twice maana hata ile hela hakuitoa yeye niliitoa mimi yani hata kuiona hakuiona. Huwa namwambia Mungu endelea kumbariki maana ndugu waligoma hata kunimbia hatukupi. Pia nimejifunza kutoa feedback kwa watu kuhusu mambo mbalimbali.