Umewahi kukutana na usumbufu unaosababishwa na huu mmea

Umewahi kukutana na usumbufu unaosababishwa na huu mmea

sijawahi kukamatwa hata siku moja.
Wala sijawahi kubanwa.ila nilimuona tapeli mmoja alimtapeli kiwanja mwanajeshi.
Yule mwanajeshi akaenda kuwaita wenzake wawili wakamkamata yule tapeli wakamuingiza ndani ya gari lake wakaanza kumbana mbupu.yule tapeli alitaja alipoficha hela kwenye gari lake.
Nipe uzoefu wako wa kuminywa goroli mkuu
 
Ni mmea ambao unaweza kukusababishia usumbufu mpaka ukajuta kuzaliwa.Watoto ambao wamekulia ndani ya mageti watakuwa hawajui.Unaweza kuwaadhibu watu na huu mmea
View attachment 1732173
Mjinga mmoja alikung'utia kwenye dawati la mwalimu mmoja mnoko sana, pamoja na rundo lake la bakora ilibidi asaliku amri na kurudi ofcn huku akitelekeza mzigo wake wa fimbo darasani.

Ofisini hakukukalika akaomba ruhusa kutejea nyumbani ambako alikaa kama siku mbili pasipo kuonekana shule.

Upupu heshima!!
 
Nakumbuka wakati nipo Shule ya Msingi wanafunzi watundu walivipaka viti na meza za Walimu hii kitu. Shule nzima ililambwa bakora za haja!
Sasa kulikuwa na upupu halafu na majani fulani hivi ukiyafinyanga yananuka kuliko kinyesi...
 
Kwanini polisi wasiwe wanautumia huu wanapokuwa wanataka information kwa lijambazi halafu lenyewe halitaki kutoa taarifa

Huu ushauri unaowapa unaweza kuanza na wewe au ukakukuta kwa namna fulani.

Polisi ni kwetu sote, tuepuke kuwapa mbinu za kutuumiza.
 
Huo sio upupu, majani hutumika kuogeshea mifugo kama mbwa, mbuzi, n.k...
Kwa watu wa Kyela majani yake hutwangwa kisha humwagwa mtoni, samaki hukosa nguvu na kufa, inakuwa rahisi kuvua. Kwa kilugha huitwa NKONDO
Kisukuma tunaita MLUKU Mwaka jana tulinunu debe la majani tukatwanga, tukaenda mtoni kuweka kwenye vidimbwi tuliokota kambare + sato gunia tatu.
 
Kuna Day Nilienda Kiparang'wanda kuchukua mzigo wa Mkulima mmoja wa Machungwa pick up tukaisogeza Shambani machungwa yalipokusanyiwa so kuna kakichaka cha kiaina fulani ile kusogea nakutana nao unanisubiri niuguse kabla tu nilishaanza kuwashwa nilipouona niligeuza kama nimeona Nyoka nduki! hiyo kitu inawasha hatari yaani tulijikuna wote tuliokuwa tumevaa kaptura nikasema siwezi uacha nikachukua karatasi nikaubeba niende nao shule ya Mkalimani nikamkomeshe
 
Nakumbuka wakati nipo Shule ya Msingi wanafunzi watundu walivipaka viti na meza za Walimu hii kitu. Shule nzima ililambwa bakora za haja!


Inanikumbusha vijana wa kihuni walimwaga upupu juu ya kitanda cha Mwendawazimu mmoja,----- looo, siku hiyo huyo mwendawazimu alifunga mtaa wote.🤣
 
Back
Top Bottom