totlo masire
JF-Expert Member
- Nov 7, 2021
- 868
- 1,398
mbona wako sio mtumbwi wa vibwengo,wangu ni mtumbwi wa majini[emoji23][emoji23].
sipendi ugomvi mpaka umri huu kisa nilipigwa na mwanamke"mwanamke" nikiwa darasa la tatu tu.
shuleni nilikuwa mpenda sifa sana,halafu maarufu shule nzima nikiwa la kwanza tu.natongoza mpaka wadada wa darasa la saba wengine wanaambizana wanacheka nikipita,hwaelewi huo ujasiri nautolea wapi!!!!
tukiwa darasani nakumbuka demu mmoja ambaye niko naye darasani alikuja akanambia nini sijui??vile namwona mshamba sio hadhi yangu maana namingo na wakubwa nikamjibu mbovu,darsa zima likacheka wakaanza kumzomea,nisijue ana kinyongo na mimi nikaja kumuuliza nini sijui'akaninyooshea kidole nikakiputa kwamba aache dharau mimi sio wa kunyooshewa kidole,aisee kilikuja kibao hicho[emoji28][emoji28],sikutegemea kwakweli.
kujaribu kujibu mashambulizi aaah wapi!!nilichelewa akanikamata mikono,nyanyua juu akanishusha kama gunia juu ya dawati,mademu huwezi pigana naye ukiwa karibu atakuaibisha.
halafu yeye ni kama aliishaanza kuvunja ungo alinizidi pound kiasi fulani.
nilichapika kweli shati vifungo vyote kuleee,nakuja kuamuliwa sina hamu.
saa nne mapumziko napewa pole tu na warembo wangu wa madarasa mengine maana nilikuwa sitamaniki[emoji23].
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]