Umewahi kupigwa roba mtaani? Weka kisa chako

Umewahi kupigwa roba mtaani? Weka kisa chako

Mwaka 2004 natoka zangu mjini kuelekea home. Mjini daladala zikawa hakuna, bahati nikapata la Mabibo nikajisemea kimoyomoyo, ngoja nipande hili nitaunganisha Manzese la Kimara. Kufika manzese nikaona nikashukie CCM Kona ya Mabibo. Ile nashuka nikaona nipate bia mbili pale Rambo bar, wengi mtaikumbuka ilikua na Malaya wengii. Basi bwana nikapata siti pale nje na kuahiza safari ya baridi huku nikivizia daladala za Kimara. Nikipata bia za kutosha na simu yangu ya sony mlio polyphonic.
Ile nimelaza bia zangu nikaona pale kituoni Kuna watu Kama watano hivi. Nikaona na Mimi niungane nao tusubiri daladala. Kumbe wote vibaka. Aisee ilenafika kituoni sekunde nyingi nilijikuta nimelimwa mtama Niko chini Sina simu na mituko yoye iko nje.
Kipindi kile surualizilikuana mifuko ya Siri. Hivyo hakiba yangu nyingi hawakuiona. Baada ya kunipora huku mmoja amenikaba Koo wakaondoka. Nilivyo cheki hakiba yangu ipo nilirudi Tena Rambo na kuagiza beer nikiwa pale nje. Na wenyewe baadae walirudi kituoni wakaniona na gida bia. Naona Sasa walijiandaa kikamilifu. Nami nilitoa pesa na kuzihesabu nikiwa pale nje kwenye taa wazione Kisha nikaingia kwenye taxi.
Hahahaha ulikuwa unajiamini mkuu
 
Kipindi hiko maisha ya kuunga unga, 2015 baada ya dili zangu kufeli kkoo, nikaona niingie ilala, nikadaka daladala fasta hadi amana pale

Napo pale Amana mambo hayakua upande wangu, ilibidi safari ya kugeuka ubungo geto ianze rasmi
Daladala za kutokea mnazi mmoja zinazoenda ubungo (hii route ina daladala chache sana) zimejaza kiasi cha kwamba mimi ni masikini lakini wale ni masikini zaidi[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Nikaona hapa kubalance hesabu inabidi niue winga hadi buguruni then nipande dalala pale hadi ubungo
Tena naweza nikalia nikapanda kwa 300/=

Safari ikaanza, kutoka ilala nikaona hapa niitafute buguruni kwa kuprint mokomoko (kutembea kwa miguu) hiyo mishale ya saa 4

Katika kula mitaa hapa na pale hatua kama 40 nikapata company ya watu kama 3 "vibaka"

Sijakaa sawa raia hawa hapa, mmoja akaja kwa mbele mwingine akaniwai roba aisee. Nikawa mpole
Mwingine anajifanya kama father hivi huku anavuta fegi, "dogo tulia atutaki kuuza gazet hapa"
Akanipiga search akapata buku, hapo nimewapa ushirikiano 90%

Wakaniacha wao wanatembea na mimi natembea uelekeo tofauti, ila niliwachana
Nikawaambia wanangu sio fresh haya maisha tu,

Nikaona Kwa usalama wangu sasa ngoja nikatembee along the road, hapo nipo malapa napandisha kimwinuko upande wa kulia opposite yangu kuna makaburi around za saa 5 kasoro
Mara nashangaa miguu haigusi chini alafu upumuaji haupo kama unavyotakiwa
Nikagundua nipo kwenye kitanzi cha wahuni hapa
Mikiki mikiki nikapate ahueni ya kupumua,
alafu walikua machalii tu
Nikaona hawa acha niwapange kishikaji, nikawaambia wanangu nimetoka kukabwa mtaa wa nyuma hapa sina kitu, mtaniua bure kamanda wenu
Kumbuka bado nipo kwenye roba [emoji3][emoji3]

Madogo wamevuta mibangi hawana ata time ya kucheka, walivyomaliza inspection bila kupata kitu wakaniacha

Pale kinyonge hadi buguruni chama, nikaingia mifuko ya siri, hii mifuko ya kibahari zaidi nikatoka na buku 8000, nikanunua soda takeaway huku nawashangaa wazarendo pale "KAMBOKI"
Huku najisemea moyoni, oneday tutafurahi pamoja[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]


Sasa ntakuja kuelezea nusura Niue mtu kwenye haya haya mambo ya kukabwa[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Juzi Kati nimerudi kitaa kwetu kusalimia kwa muda maana longtime sijafika huko .

Kuna madogo niliwaacha shule za msingi wamekua kua wameota vindevu na kuanza kuvuta fegi .

Kwa habari nilizopata kwamba mtaani kwetu Kuna madogo wamekuja Kama vibaka japo mtaani sio uswazi kivile mtaa kishua kidogo.

Kumbe navyotaka kila kuelekea mjini wananipigia hesabu .

Kwakwaida huwa nikitembea natembea kibabe hivi mwendo wangu wa kijeshi jeshi nikipita karibu yako lazima usikie kishindo[emoji1] madogo wakawa wanawaz wataniingia vipi wanikwapua simu na hela .

Maana wananiona asubuhi na usiku mtanii nikipata halafu Mimi siwajui.sina habari nao.

Sasa kuna mwana mmoja mwanagu Sana wakamfuata wakaanza kuniuliza "oya Yule bro anaepita hapa Ni Kaka yako Nini " Jamaa anawajua Tabia akawaambia Kama mnataka kumkaba acheni mtakufa anapiga kipigo kubaya sana

Jamaa wakaa abort mission Yao

Jamaa anakuja nihadithia nilicheka Sana nikamwambia ungewaacha waje kwanza tuondoa hii Tabia mbovu mtaani wanageuza mtaa kuwa kishenzi.
 
Humu JF hata wapiga roba za mbao wamo humu.

Waje na wao wachangie
 
😂😂😂😂😂😂😂

Picha linaanza, kipindi nikiwa KCMC nimetoka zangu hostel za TATCOT kupiga story na washkaji zangu huko, ilikuwa mida ya saa 2 kasoro robo hivi nikatoka zangu kuelekea magetoni (nilikuwa nakaa maeneo ya makutini). Basi, kwa sababu haikuwa giza sana na kuna watu wachache wanapitapita, nikaamuo ngoja nipitie njia ya kutoka school of nursing halafu nikatize cha school of Physiotherapy then nitokee school of Optometry then nikatize uwanjani ili nitokee kwenye mashamba ya KCMC ambapo itakuwa karibu kutokea makutini, aisee kufika katikati nikaanza kuhisi harufu ya bangi kumbe kuna raia walikuwa wanapiga vitu vyao hapo

Nikasikia sauti ikinitaka kusimama, nikawa mbishi, nikaendelea kutembea zangu, mara kwa mbele wakatokea wawili, nikaanza sasa kukimbia, mara nikadondoka wakanishika wakanirudisha pale kwenye kijiwe chao nikiwa nimekabwa na matusi mengi, bahati nzuri siku hiyo sikua na vitu vingi, walichukua saa, simu pamoja na hela 12,700

Walivyoniachia niliona kama muujiza, nilifunguka balaa, sikurudia tena kupita hiyo njia usiku wala asubuhi sana mpaka naondoka hapo KCMC
 
Nilitaka kukabwa ila sio mtaani kwangu Ni kule jangwani nilikuwa natoka kwenye mkutano wa injili enzi zileee.....Bado Niko kijana nilikuwa mlokole wa nguvuuu

Basi bwana, Kuna siku nilienda hapo mahubiri tukashangweka weee mpka mida ya Kama saa 4 hivindio tukajongea kituoni kutafuta usafiri, Sasa usafiri wenyewe ulikuwa mgumu balaa na MIJITU nayo ilikuwa nyomiii
Basi mi nilivyoona pale sipaelewi nikaamua nitembee hadi kariakoo nikachukue usafiri
Basi bwana, nikachapa mwendo fasta nikifuata barabara ya lami ya kwenda kariakoo, nikafika sehemu Kuna km kidaraja hv halafu kumepoaa hamna watembea kwa miguu kauoga flani hv kaliniingia ghafla na akili ikaniambia geukaaa.....



Itaendelea kesho:'[emoji2][emoji2]
 
Yes 2010
Fainali uefa baina ya asernal na Barcelona kumbukumbu golikipa asernal alipata kadi nyekundu mapema sana alimgusa unyayo samueli eto akienda kufunga goli

Najamaa yangu tunasiku mbili panaitwa bagamoyo unaelekea stend kuu yatukuyu panadispensari na bar moja hivi nalakitano kwenye waleti ,simu Samsung

Kumbe kunajamaa ananiwinda mana natumia pombe balaa
Ukafika muda wamechi bwana ukumbini nilazima upite kaunta ,upande wakulia kunachoo unavoelekea ukumbini
Niliingia choo gent kama kawa kumbe kibaka alikuja nyumayangu akaingia cha ke ili ufike choo cha wanaume nilazima uvuke mlango wa ke
Natoka hivi nataka kukunja niingie baa niliguswa begani kugeuka nikasukumwa kidogo ukutani nikanata pale

Jamaa akatoa kisu vile vyakufyatua akaniambia unaona watu wanapita kuingia kuangalia mechi nikasema ndio
Ukipiga kelele wananiua naomba zilehela zote na simu kila kitu tumeona kwanza mgeni hapa tokajana unakunywa tu bia hapa ukikaa hata kuinuka huinuki

Nikasema nimekwisha ghafla akili ikija yule jamaa niponae alikua ametoka bwana mungu mwema akili ikaja nilegeze mwili na kauli hapo kichwani nipo nahisi damu inamwagika nimeloa mwiliwote
Watu wanapita nawanamwita jamaa jinalake(),anaitikia poa napiga stories na big yetu hapa

Basi ,nikamuangalia alivo nikipande cha MTU mweusi harufu pia yabangi kwambali nasikia toka kwake
Kimo chake urefu kidogo tunalingana

Nawaza nipige wapi huyu usoni jibu ikawahapa
Ghafla wazo likaja nitagonga kichwa changuvu eneo lapua nilazima ainame kidogo niifaidi pua yake
Nikamwambia naomba laini nitoe nikuachie simu napesa zote nakupa

Jibu likawa
Sawa brother nyie ndo mabrother tunawataka hamna bugdha
Nikatoa laini ingia mfuko wanyuma to a waleti

Wakati natoa waleti aliinama ili aifadhi kisu anavoinuka niligonga kichwa puani alilia kwasauti kubwa mamaaaaa nakufa akadondoka chini paaa

RAIA kwenye ukumbi na bar wakatoka wanauliza imekuaje nikawambia wakati mnapita hapa nilikua nimepigwa tero amesema nimpe simu napesa pia Mimi mgeni nakaaje sikumbili nakunywa tu pombe

ndo nikasikia najina lake anaitwa God ,dereva vigali beba mizigo soko LA tukuyu stend pale



Kutoka ilesiku sijawahi kusekana nyumbani sambili kamili usiku labda niwe safarini

Usiombee ukutwe au ubananishwe na kibaka sikiaga tu

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Mwaka 2010 natoka mlimani city kuangalia fainali world cup.Narudi zangu geto mitaa ya robert bar kwa nyuma nilikung'utwa ngumi ya sikio nikakosa kusikia kwa muda.Akili iliporudi sikuwa na simu yangu,wallet wala kofia.Nilibak na buku tu mfuko wa nyuma.
 
Enzi zile za kauli mbiu laki si pesa,awa shwain nilikua najihami sana na sikuwai wapata.
Nilikua nikipiga mipombe saa 7-10 ndo mida ya kurudi,napita chochoro lolote ili nifike home sikuwahi wapata.
Nilikua najiamini sana,nilikua na mbukta wa timberland una mifuko mikubwa,asa mida ya kurudi ikifika napasua chupa ya bia,moja au mbili.
Vipande ya chupa navitia mfukon kwa tahadhari kubwa,kulia na kushoto na nyuma kias.Simu natia kwny boxeeeeer.
Nikijua atakae nikaba na kuingiza mkono mfukoni atafurahia shoow.
.
Bht nzuri mby sikuwahi kukutana nao,
Kwa sasa silewi tena narudi home mapema tu.
 
Mimi nilipigwa ngwara 😂😂🤸enzi za chuo,njaa za usiku nikajifanya kutoka hostel kwenda kununua chips jomonii woiii mitaa ya bonanza area c Dom... ile ngwara siji isahau asee japo nilitoka mkuku ni Mungu tuu maana walikuwa vijana kama wanne na ndio kipindi ambacho matukio ya mauaji yalikuwa yamepamba moto hasa kwa wanafunzi....lile tukio ni moja wapo lilinifanya niokoke asee maana ukiniuliza nilivukaje nabaki kusema ni Mungu wa mbinguni tuu,daah!!!🙌🙌
Hawakukuumiza sana lakini?😅 Au ndio ulikubali ajali kazini tu
 
Back
Top Bottom