Umewahi kupigwa roba mtaani? Weka kisa chako

Fainali ya UCL kati ya Arsenal na Barcelona ilichezwa mwaka 2006, fainali ya mwaka 2010 ilikuwa kati ya Inter Milan ya Jose Morinho na Bayern Munich ya Lois Van Gaal.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ulienda maisha plus nini kupata na matunda [emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongeraa pale kwenye ile sehemu ilikuwa hatari sanaa ziku zote
 
Kuvua shati na kutembea bega juu bega chini hizo ni code mkuu kuna mitaa ukipita hvyo hata iwe sa tisa usiku uwezi kukabwa
 
Mitaa yangu hiyo mkuu, dah way back nimesizi sana malapa hapo. Umenikumbusha mbali sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ghwandike kinyakyusa khitupu nkamu,,,,,huu mwandiko una lafudhi ya Kinyakyusa mkuu...
 
Nilipigwa ROBA kichochoro cha Mbagala Kiburugwa....

Kanuni ya ROBA si kung'ang'ania uutoe mkono....bali bila ya kupoteza muda nilijikunja na kuweka mikono katika mkono wake ulio shingoni mwangu na "kuning'inia"....

Kama umecheza MARTIAL ARTS hii ndio salama yako....

Kikanuni.....hakuna mkono unaoweza kuhimili UZITO WA KILO 70 za mwanadamu....

Yuke Sakala hakuhimili UZITO WA MNING'INIO WA MWILI WANGU ,miguu nimeikunja pia ili niongeze uzito chini(gravity)....mkono wake ulichoka na akaniachia....Kama angeujua "mchezo" basi wakati NILIPOJIKUNJA NA KUINAMA angekwenda nami chini(naye angeinama).....angefanya hivyo NISINGEWEZA KUJIOKOA....

Baada ya kuchoka mkono wake ,nilimgeukia kwa haraka na KUMTIA VIDOLE VYA MACHO....huku nikikamata "MBUPU"zake na kuzivuta.... Alitoa ukelele mmoja matata....SIKUMSUBIRI NIKAKIMBIA MBIO ZA USAIN BOLT....🤣🤣
 
Kilimanjaro,Moshi vijijini,Kibosho mtaa wa Kombo, Tumekaa kwenye gogo tunakula "kaya" na wanangu wawili mmoja mtoto wa Tandika (M'bongo) na (Nzige) huyu kwao Chunya-Mbeya , majira ya saa 12 jioni ghafla bin vuu ikatokea njemba moja hivi mbavu sana ikachomoa panga, hapo mi ndo nilikuwa naroli kitu, Nzige akataka kukimbia kwa uoga "oya chini ya ulinzi, kaa chini" mimi na huyo dogo wa Dsm ndo tulikuwa hatuna kitete, mi kwanza nikalipua "kitu" punde si punde zikaibuka njemba mbili kwa mtindo ule ule wa mapanga , sasa kati ya wale wawili waliokuja mmoja wao nilikuwa nakutana nae kwa pusha mara ingine namnunulia ganja au namuachia fegi, alivoniona tu akaja akatoa "tano" wale wenzake wawili wakakosa nguvu ya kutukaba, alafu mi hapo nishasizi siogopi chochote, nikamtembezea ganja yule mbavu nikawasha na fegi wakashusha mapanga yao tukaanza kupiga nao na stori nikawapa na ganja wakanyonga....

Wahuni hatukabwi kizembe, labda ukosee code
 
Vaa buti LA kihuni,jins mtumba mnyonyo,kunja suruali mguu mmoja na mwingine achia kawaida,vua shati au T-shirt kisha tupia begani ubaki na vest kisha badili Mwendo na bega moja bonyeza chini,dundika km mla ngada,nunua sigara hata 3 vuta hadi uvuke sehemu hiyo Mbaya na puliza moshi Wa kutosha hewani,hakuna kibaka atakugusa
 
Ulikabwa mara 2 wakati mmoja ? Hawana huruma 😀
 
Miaka ya 2013 naishi kigamboni ferry.
Nilikuwa nafanya shughuli za umeme Goba.
Siku Moja nimerudi ghetto mida ya night huku nimeweka tester (Screwdriver) flat mfuko wa shati.
Sasa wakati nakatizq chochoro za magenge ya urasa, mara ghafla , kibaka akanipiga roba matata. Pasipo kupoteza muda nikawahi ile pisipisi yangu iliyo mfuko wa shati. Nikamdunga nayo mitaa ya Mbavu. Ile anashituka kuniachia, mie nikakurupuka kukimbilia huku sokoni chini, kibaka akakimbilia kule juu.
Pisipisi nayo ilipotelea pale pale.
Tangu siku hiyo, mtaani wananiogopa , kwa kitendo kile. Nilichomfanya yule kibaka.

Mara zote Jaribu kuwa na zana shirikishi. Pindi inapofika usiku.
 
Hawa wajinga wa Mbagala wasijichanganye kwangu nitawaua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…