Umewahi kupigwa roba mtaani? Weka kisa chako

Hawa wajinga wa Mbagala wasijichanganye kwangu nitawaua.
Ha ha ha mkuu wangu👍...unaweza ukawa na black belt na wakakudhuru kwa kukuwahi vyema tu 🤣

Muhimu ni kujua mbinu za kujilinda wakikuvamia na kinachofuata ukimbie....laa kama wewe ni Jet Lee basi utawapelekea moto wa maana!

Mkuu huku uswahilini Kuna tatizo moja....ukikabwa jamii haisaidii kwani WAKABAJI NI WATOTO WAO....unaweza kuwatandika wakabaji halafu wahuni wote wa mtaa wakakumiminikia na silaha tofauti....Sasa ukitoka hapo shukuru Mungu...kama unatembea na "uchawi wa mzungu" basi Hilo ni jengine maana huo uchawi ni balaa 🤣🤣
 
[emoji1]
 
Taifa walinipora Camera,pesa na simu yangu wakati natoka taifa kuangalia mpira,then ile simu sikureneaw laini Kama wiki hivi,nikatuma message kwa namba nyingine chochote kibaya mikitokea wanitafute kwa namba hii,nikapanda Treni Hadi kigoma mjini,kuna eneo linaitwa Kitonga nikamtafuta mtaalam akafanya yake,huku wale vibaka walivimba vichwa kuja kunitafuta ,so far nilipata kahela kidogo..
 
Hahahah huu uZi nimecheka sana
Umenifanya nimekumbuka mbali
Sana

Ova
 
Kuna hii mbinu ya kuvua nguo zote, unaziweka kwenye mfuko, unabaki na boksa. Hii hutumika sehemu korofi sana!
Kuna mwana mmoja pande za mwembeyanga tmk ndio zake hzo wahuni huwa wanajua chizi kumbe mwana yupo timamu tuu hizo ni Teknik utumia afikapo sehemu zile korof huyo hadi anaokota makopo hajawah kukabwa kwa teknik zake
 
Hili la kutembea bila vitu vya thamani linaweza kukutokea puani. Wezi wengine wakikuta huna kitu wanakufanyia unyama mbaya sana.
 
Ilikuwa sagavodo, fukwe moja ya kidwanzi pembezoni mwa ziwa Tanganyika, eneo linaitwa kinindo Bujumbura Burundi.

Nilipata manzi wa kizungu, sasa kaja job kanibeba beba tu ka kifurushi, na nilikuwa nafungua PC nikawa na lile screw driver refu, nikalisunda mfuko wa nyuma, tukatoka, si mbali hapo kazini na hapo sagavodo, tumeenda fresh ile mida ya jioni viboko huwa wanatoka nje ufukweni, so manzi akawa anataka kupiga picha na upuuzi mwingine, ile siku sikufurahia kufuatwa job ghafla alafu mapenzi ya kizungu ya kifala sana, full kuburuzana, tumechill pale ufukweni mpaka saa moja moja hivi kigiza kinaanza sasa ndo tunaondoka, kuna kipande kina maboma, kipindi hicho. Alaf barabara imenyooka unaona tunaenda kulee alafu pembeni ni maporia ( vichaka vikubwa ) vya maana tu. Kwa mbali nikamuona mjuba kakatiza kwa kasi ya kicheche, kavuka toka kichaka A kapiga mbizi kichaka B. Dah nikamuuliza manzi, mbali na simu una nini kingine? Anauliza kwanini? Kabla sijajibu wanatokea kwa mbele Interahamwe kama wanne hivi na mapanga yanameremeta,

No Story, mzungu [emoji383], lete Money, dah, dem anaogopa, mi mwenyewe nikaona leo nimeingia anga za wajuba, sasa wakat najibizana nao, huku manzi nimemvuta kwa nyuma yangu yupo nyuma mgongoni huku, wale wasen** wako serious nikaona sasa hivi hapa tunapasuka, nikamwambia manzi anipe simu yake, wakati nataka kuwapa simu zote yangu na ya manzi wanataka na Ice alizovaa, silva alaf alikuwa na pete ina ki diamond na yenyewe wanataka pia na money, eeh nikaona hapana aisee huu unyonge, sasa wao wana zana alaf dizain kama hawajiamini, sasa manzi anasaula mavitu na mkojo ushamtoka, ndio nikakumbuka kumbe nna bisibisi mfukoni, dah lilikuwa kosa, nikaweka simu chini na cheni ili aokote, yule kiherehere masikini akaingia mkenge, alivyoinama tu yule kiongozi wao nilimsindikiza na bisibisi ya jicho, alitoa ukelele mmoja, panga likaanguka nikaliokota mbio zikaanza sasa wao ndio wakaanza kutoka nduki wanakimbilia vichakani huku mmoja analia haoni nikapeleka panga la bega lile lile panga alilotumia kuniharas nalo, alaf nikamuachia kama zawadi nikarudi kwa mzungu wangu( maana sikuwa na hakika kama kule walikokimbilia kama ni wao tu ama kuna kikosi kazi kingine ) nikaokota vitu vyetu, nikamuweka begani, mbio...sitosahau ile siku.

Alafu kama saa nne hivi usiku nikarudi lile eneo na wana. Walikuwa wamejenga kabisa kama vibanda vinne, wanauza pombe haram na misuba, hatukuuliza, kilichowakuta walijisalimisha Comine( Polisi ) ya Kinindo.
 

Aaah nmecheka apo umesema kinundu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Miezi kadhaa imepita ,mi nikishakulaga nyama choma na bia zangu huwa najiona Kama dume la nyani yaani confidence ya kutosha .Sasa baada ya kuchangamka nikapanda toyo kufika mitaa fulani nikamwambia dereva wa toyo nishushe njiani kwani dume la nyani haliwezi kupelekwa mpaka nyumbani bwana .Boda akaniambia mwanakwetu hii mitaa nishai Kuna watoto nuksi .Mi kwa kujiamini nikamwambia mwanakwetu siku nyingi sana sijacheza nao hao ndio haswa nawataka( ngumi zenyew sijawahi hata kuzijaribisha).Kutembea kidogo ghafla naona mkono ushazunguka kwenye shingo ,nikawaambia acheni utani wanangu,ngoma inazidi kutight tu .Ile roba ilikuwa kali mpaka nikayataja majina matatu ya bimkubwa wangu huku nikiwaambia madogo najuta kwanini sikusikiliza ushauri wake wa kuacha pombe.Madogo wakanilostisha mazaga na ngumi za uso za kutosha . Asubuhi naamka lips ya juu ndefuuu ya chini fupi.Sitasahau pia nilivyopigwa mpini wa jembe wa mgongo kwenye bodaboda mpaka nikashuka mwenyewe😀😀 mitaa hiyo hiyo.Acha nikamwagilie moyo ntarudi saa 9 lakin na bajaji.
 
Acha uongo UEFA 2010 final ilikuwa Inter Milan Vs Bayern.
 
Kuna mwana mmoja pande za mwembeyanga tmk ndio zake hzo wahuni huwa wanajua chizi kumbe mwana yupo timamu tuu hizo ni Teknik utumia afikapo sehemu zile korof huyo hadi anaokota makopo hajawah kukabwa kwa teknik zake
Shida yote hiyo ya nini?
 
Mimi nilkuwa na broo angu tumetoka kiwanja Cha Dar live kipindi imefunguliwa .tumetoka mida ya sa8 usiku tukakuta gari za kwenda chamazi hazipo na sisi tulikuwa twaenda saku. Ikabidi tutembee tulipofika mitaa ya magengeni almaarufu mahakama ya simu. Ikabidi tuanze kutembea kama wahuni , huku tunatoa maneno ya kihuni kwa sauti kubwaaa nakuombana bangi . Tulipo vuka hilo eneo tulicheka sanaaa. Maana hata bangi na fegi hatujawahi vuta.
 
NILIKABWA KIFALA SANA MCHANA TENA NYUMBANI NA MBELE YA WASHKAJI NA DOGO LANGU AKISHUHUDIA

Miaka ya nyuma nikiwa dodoma mitaa ya mailimbili hom tulikua na kimaskani nje ya nyumba yetu hapo nikiwa form 3

Siku moja tunapiga stori kama hizi za kwenye huu uzi bac kuna broo mmoja akatokea. Tulikua tunamfahamu tulisoma nae madrasa akaacha akawa anavuta mibangi cjui wapi uko

Baada ya kusikia stori tunazopiga akasogea karibu na mwendo wake wa kiteja teja

Akatwambia madogo mtu yyte akikupiga roba nawapa njia tatu za kutoa. Akanambia mimi nimpige roba nikawa nampiga bla kutumia nguvu lkn akawa anatoa mpaka style zote tatu zikaisha

Sasa akanambia anipige mimi then nitoe kutumia style alizotufundisha. Msenge c akanikamata roba matata sana mbwa yule. Tumia style zote pale waapi zinafeli msenge haniachii

Nikaona hapa sasa nakufa kweli jicho limenitoka na pumzi zinakata washkaji wao wanaona utani tu wanacheka

Basi yule boya akatumia mkono wake mwingine akanipiga sachi akakuta simu na buku mbili pesa akachukua simu akaniachia afu akaniacha nkaanguka huku nakohoa. Akasema "siwezi kufundisha mitoto misenge isiyoelewa bure bure"

Huyoo akasepa zake huku wana wakinicheka vbaya mno. Kwa hasira nikaingia ndani kulala

Popote ulipo Twalibu siku nkirudi Dom lazma nkutafte mbwa ww
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…