Raymanu KE
JF-Expert Member
- Jan 20, 2022
- 8,611
- 16,118
Duh! Hii hatarii!
Me walitaka kunipiga tukio ila Binti mwenyewe akaniambia nikaushie tu niachane nao
Nimelala nae kama leo kesho yake mama yake anatuma mjumbe eti nifanye utaratibu nipeleke posa laa sivyo akanishtaki kijiji (ofsini) maana namchezea mtoto wao
Sasa katika maongezi wakajichanganya eti Binti ana mchumba wake nimpe laki yule mama ili yaishe au kaka wa mtoto atakuja na ni mdeadly. Basi nikamchana vilivyo yule jamaa mjumbe nikamwambia mwambie huyu mama aache njaa Mimi sitishiwagi mwambie hata huyo kaka wa binti simwogopi na kama Binti ni kitega uchumi basi mwambie mama yake aje kesho achukue hiyo laki
Usiku yule Binti akajileta tena (alinielewa sana na hata mpaka kulala nae vile ni yeye ndo alinitega) tukazungumza sana nikawa nampasha na yeye basi akahuzunika sana akawa anasema "mama mbona Mimi namjua hiyo tabia anayo sana ila wewe usijali hatafanya lolote
Basi bwana Cha kushangaza yule mama alikuja kweli kufuata hela ila Binti yake akaniambia achana nao usimpe hata mia kwanza wamesema wanakuogopa huoni wameishia kule mbali (walifika kwenye kotaz zetu lakini wakakaa mbali kabisa). Basi Mimi nikawafuata hadi pale walipo nikawasalimia kisha nikawauliza "tuwasaidie Nini" wakajibu "tumekuja kumjulia Hali tu huyo Fulani" (yaani mtoto wao- maana alikuwa amekuja kama house girl kwa moja ya wenzangu katika kazi). Walivyojibu tu hivyo mimi nikawapita zangu moto! nikaishia
Stori ndefu ila kufupisha tu ni kwamba binti aliniganda sana na kuonesha ananipenda hajawahi kula hata mia mbovu yangu na mimi nikawa Sina mpango nae. Alikuwa tu akilalamika kwamba mama yake kamharibia. Siku kadhaa mbele akafukuzwa pale akarudi kwao mara nasikia kaolewa mbali kidogo na ndo hatujaonana hadi leo