Umewahi kuswekwa lockup(selo), Unakumbuka nini?

Umewahi kuswekwa lockup(selo), Unakumbuka nini?

Binafsi ni moja wa watu niliowahi kuexperience kufungiwa selo, Niliwekwa lock up Police central pale Arusha, Nlivyofika niliingia chumba kidogo cha kutoa maelezo ya kesi na kuhifadhi vitu nlivyonavyo na kuamrishwa nichuchumae (ukiwa mbishi unakula makofi ya kutosha)nakumbuka nilikuwa na simu na elf 22, nlkakabidhi vitu vyangu nikapewa kijikaratasi cha vitu nlivyoweka.

Nlivyotoka hapo kilichofata nliamrishwa(sio kuombwa) kuvua mkanda na viatu nikasachiwa fasta fasta kama kuna vitu nimeficha then nikaingizwa ndani selo(hapo ilikuwa kipindi cha baridi kungekuwa na joto ningeingia na boksa peke yake), Aisee ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia mule nliwahi kuskia masela wa mule ukiingia wanakupiga lakini wala sikuguswa na tulisalimiana vizuri na story ziliendelea, Jion kuna roll call unaitwa jina la kwanza sasa ole wako useme "Nipo" utakiona, inabidi useme jina lako la ukoo unahamia uoande wa watu waliohesabiwa, Ikifika usiku utaratibu ni huo huo, Mule ndani sio mahala pazuri mpasikiage tu, Ikifika usiku mnalala chini kwenye sakafu hakuna cha mkeka wala nini na mnalalia ubavu ili wote mlale mana mnakuwa wengi sana huwezi kulala kama upo kitanda cha 6x6, Nashukuri mungu kesho yake nlipewa dhamana nikarudishiwa vitu vyangu na nikaondoka na kilichofata ilibidi niripoti polisi wiki nzima asubuhi saa mbili na nilifanya hivyo.

Kosa langu lilikuwa ni dogo sana na ushauri naowapa mtii sheria mana hata ukimwaga taka sehem isiyotakiwa, kukojoa sehemu zisizotakiwa kunaweza kukupeleka mule ndani.
Pole mkuu ila naamini mtu yeyote anaweza kupitia sekeseke hyo ktk maisha aidha kwa kuteleza kidogo au hata kwa kusingiziwa. Ni muhim sometimes tukajiandaa kwa vitu km hivi
 
Nshalala Central Arusha Kituo Kidogo Kaloleni Pia Arusha Ilifika Kipindi Police Wakiniona Wananiacha Tu Mitaa Ya Shivaz Sikosekani Wakikamatwa Nami Nimo Maromboso Nililala Siku Moja Ila Saivi Nshakua Yashapita Sitaki Hata Kukumbuka.
Inabid weekend ijayo tuende shivaz mkuu, show zote nitalipia-si buku 10 tu per show?😀😀😀
 
Kesi kubwa useme alikula tigo kinguvu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mkuu hyo ilikuja coz plc walisema hii kesi ni madai,kufika kwa pilato hana ushahid bwana pilato akashauri myamalize kindgu, nikakataa maana alishanijaza gesi balaa, plto kauliza kwann unamuacha nikamjb ananilazimisha kula ndogo[emoji57] [emoji57] [emoji57] na kesi ikaishia hpo!!!!!!!!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] hyu jmaa vyeeeepe ametumwa mnarefusha uzi kwenda wp??[emoji57] [emoji57] [emoji57]
Sijui juu sijui chini..hii chitchat sijui kwanini watu wanashindwa elewa.

Ukinikuta jukwaa la siasa au MMU nakuwa serious kuchangia mada ila mkuu angalia maana ya chit-chat
 
Nikisikia ninatafutwa na polisi ninahama mji kabisa, nilikaa masaa 8 nilichoka kulala, kukaa na hata kusimama nilikosa uhuru wa kufanya ninachotaka nilijutia kosa na sitaki kurudi tena selo
 
Back
Top Bottom