Umewahi kuwa kwenye uhusiano na Mtu Mchoyo? Ilikuwaje?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Tulikutana kwenye mkutano wa kikazi, na mara moja tukaclick. Alionekana mkarimu, mwenye malengo makubwa, na kila mara alinitia moyo kufuata ndoto zangu.

Wiki za mwanzo zilikuwa tamu—zawadi ndogo ndogo, meseji za asubuhi na ahadi zisizoisha za maisha bora ya pamoja. Nilihisi niko na mtu sahihi.

Lakini kadri muda ulivyopita, nilianza kuona upande mwingine wa sarafu.

Alikuwa mchoyo wa muda, hisia, hata maneno ya faraja. Kila kitu kilikuwa ni lazima kimpendelee yeye kwanza, maamuzi yote yawe ni kuhusu kazi yake, ratiba yake hata chakula tulichokula kilitegemea anachotaka yeye. Nilipojaribu kueleza hisia zangu, alinipuuza au kunigeuzia maneno, akinifanya nijihisi kama mzigo.

Mwisho wa siku, niligundua kuwa mapenzi si ya mtu mmoja tu. Nilipoondoka, nilihisi huzuni lakini pia wepesi wa ajabu nilikuwa huru.

Tangu hapo, nimejifunza kuwa ukarimu kwenye uhusiano hauhusishi pesa pekee, bali pia moyo wa kugawana kila kitu kuanzia furaha hadi majonzi
 
Kila point uliyoandika inaonyesha wewe ndo ulikua unahitaji kupokea kwa mwenzako hakuna sehemu uliyokua unatoa chochote sasa kati yako we na yeye nani mchoyo? We unataka ule unachotaka wewe ila yeye anataka ule anachotaka kwakua ndo uwezo wake ulipoishia sasa huo ni uchoyo mbona kajitoa sana?

Wewe ni mtu usie na shukrani, na ukiwa huna shukrani hutakaa uridhike kwa chochote kwenye maisha yako hata ukipewa utaishia kulaumu tu jirekebishe.
 
Wewe ulikuwa unatoa kipi kati ya hivyo ulivyotaka upewe wewe?

Kuna wakati wanawake wanakuwa wabinafsi. Mbali ya kuwa na mahitaji ya kifedha hujidai wanahitaji na muda wako vile vile, kusahau kuwa hitaji lao kuu ni fedha ambazo zinapatikana kwa mtu kufanya kazi; na ni ngumu kupata muda ikiwa unafanya kazi.

Mapenzi ya tamthilia ni maigizo, sio kweli ile.
 
Tulikutana kwenye mkutano wa kikazi, na mara moja tukaclick. Alionekana mkarimu, mwenye malengo makubwa, na kila mara alinitia moyo kufuata ndoto zangu.

Wiki za mwanzo zilikuwa tamu—zawadi ndogo ndogo, meseji za asubuhi na ahadi zisizoisha za maisha bora ya pamoja. Nilihisi niko na mtu sahihi.

Lakini kadri muda ulivyopita, nilianza kuona upande mwingine wa sarafu.

Alikuwa mchoyo wa muda, hisia, hata maneno ya faraja. Kila kitu kilikuwa ni lazima kimpendelee yeye kwanza, maamuzi yote yawe ni kuhusu kazi yake, ratiba yake hata chakula tulichokula kilitegemea anachotaka yeye. Nilipojaribu kueleza hisia zangu, alinipuuza au kunigeuzia maneno, akinifanya nijihisi kama mzigo.

Mwisho wa siku, niligundua kuwa mapenzi si ya mtu mmoja tu. Nilipoondoka, nilihisi huzuni lakini pia wepesi wa ajabu nilikuwa huru.

Tangu hapo, nimejifunza kuwa ukarimu kwenye uhusiano hauhusishi pesa pekee, bali pia moyo wa kugawana kila kitu kuanzia furaha hadi majonzi
Mtu macho hua anapoteza ladha kabisa hata kama ni rafiki, umenikumbusha nilikua na mpenzi miaka hio ya ujana alikua mchoyo wa kutupwa ananunua muhindi wa kuchoma akala na asikugaie na nimpo pamoja matembezini ,alikua mchoyo Hadi wa faraja,mapenzi,maneno matamu Yani ule uchoyo wake sijui ulimfikisha wapi sahv mana alikuja akaoa akaja kuachana na mkewe sababu ya huo huo uchoyo.
 
Tulikutana kwenye mkutano wa kikazi, na mara moja tukaclick. Alionekana mkarimu, mwenye malengo makubwa, na kila mara alinitia moyo kufuata ndoto zangu.

Wiki za mwanzo zilikuwa tamu—zawadi ndogo ndogo, meseji za asubuhi na ahadi zisizoisha za maisha bora ya pamoja. Nilihisi niko na mtu sahihi.

Lakini kadri muda ulivyopita, nilianza kuona upande mwingine wa sarafu.

Alikuwa mchoyo wa muda, hisia, hata maneno ya faraja. Kila kitu kilikuwa ni lazima kimpendelee yeye kwanza, maamuzi yote yawe ni kuhusu kazi yake, ratiba yake hata chakula tulichokula kilitegemea anachotaka yeye. Nilipojaribu kueleza hisia zangu, alinipuuza au kunigeuzia maneno, akinifanya nijihisi kama mzigo.

Mwisho wa siku, niligundua kuwa mapenzi si ya mtu mmoja tu. Nilipoondoka, nilihisi huzuni lakini pia wepesi wa ajabu nilikuwa huru.

Tangu hapo, nimejifunza kuwa ukarimu kwenye uhusiano hauhusishi pesa pekee, bali pia moyo wa kugawana kila kitu kuanzia furaha hadi majonzi
Ndivyo ilivyo utu,furaha na upendo,vipo tangu na tangu,pesa ni matokeo tu ya hivyo vitatu,kamwe pesa haitaweza kuchukua nafasi ya hivyo vitu vitatu.
 
Tulikutana kwenye mkutano wa kikazi, na mara moja tukaclick. Alionekana mkarimu, mwenye malengo makubwa, na kila mara alinitia moyo kufuata ndoto zangu.

Wiki za mwanzo zilikuwa tamu—zawadi ndogo ndogo, meseji za asubuhi na ahadi zisizoisha za maisha bora ya pamoja. Nilihisi niko na mtu sahihi.

Lakini kadri muda ulivyopita, nilianza kuona upande mwingine wa sarafu.

Alikuwa mchoyo wa muda, hisia, hata maneno ya faraja. Kila kitu kilikuwa ni lazima kimpendelee yeye kwanza, maamuzi yote yawe ni kuhusu kazi yake, ratiba yake hata chakula tulichokula kilitegemea anachotaka yeye. Nilipojaribu kueleza hisia zangu, alinipuuza au kunigeuzia maneno, akinifanya nijihisi kama mzigo.

Mwisho wa siku, niligundua kuwa mapenzi si ya mtu mmoja tu. Nilipoondoka, nilihisi huzuni lakini pia wepesi wa ajabu nilikuwa huru.

Tangu hapo, nimejifunza kuwa ukarimu kwenye uhusiano hauhusishi pesa pekee, bali pia moyo wa kugawana kila kitu kuanzia furaha hadi majonzi
Pole sana.Hukufa?Hebu jishike sehemu ulipo moyo uhakikishe mkuu.
 
Wanachokutendea watu au mtu ni uakiso wa kile unachowatendea watu wengine......
 
Back
Top Bottom