Umewahi kuwa kwenye uhusiano na Mtu Mchoyo? Ilikuwaje?

Kwa haraka haraka atakuwa ni KE!
Na Mwanaume anaweza kuwa LastBorn,na uwezekano wa wote kuwa last borns ni mkubwa sana!
Kaeni chini mzungumze--hakuna mtu perfect,hata ukimzaa wewe mwenyewe hatokuwa kamili.
 
Usitegemee furaha ya mwenzio ndipo ufurahi.

Jamaa hakutaka kujiweka mateka chini yako siku ukiondoka unaondoka na furaha yake.

Nadhani ulivyoondoka jamaa alibaki na furaha yake.

Ni kati ya wanaume wachache sana wanaojitambua na kutambua thamani ya maisha yao
 
Wewe ni KE au ME?
 
Maisha ya ndoa ni changamoto saana.
Kuja jamaa liniwahi msikia alisema kwann mungu asitonyeshe yule mwandani wako kabisa?

Ambae atakuwa sambamba nawew kwenye Kila kitu? Ili tuhangaike tu kwenye kutafuta pesa.

Kwanamna flani niliiwaza sana hii kauli yako nikaona Kuna ukweli ndani yake.
 
Mimi nili date namdada fln eti yeye alikuwa anataka nitoke nyumbani nimekula nikienda kulala hata kama akipika hakuwa akijiskia vizuri nikila
 
Mwanamke anataka muda wako,pesa yako,mapenzi yako na roho yako. "Wiki za mwanzo zilikuwa tamu, zawadi ndogo dogo, vimeseji vya asubuhi" mwanamke mwema aliyeandikwa kwenye biblia ni mpambanaji,mwenye upendo Kwa mumewe na wa jamaa zake, huyu mwanamke hapatikani karne hii na zijazo.

Leo nimeenda kanisani kupunguza mzigo wa dhambi, baada ya kumwambiya Padre nimefanya uasherati Mara nyingi akaniuliza, Umeoa? Nikamjibu sijaoa, akaniuliza Kwanini? Sikumjibu, alichonisisitiza ni kwamba nioe! Wanawake wa kuoa ni Hawa wanaodhani upendo wa kweli ni mwanaume kujitoa zaidi kuliko mwanamke.

Niliwahi kukutana na mwanamke wa Aina yako, nilijinyima sana kwaajili yake, lakini sikuambulia chochote zaidi ya ukimya na Hisia mbaya juu yake. Bora hata wewe ulikuwa unaelezea Hisia zako. Wanawake wamekuja kuiharibu hii Dunia.
 
Atakukumbuka sana
 
ndani ya siku moja uliomba
1.akuunge bando
2.akusaidie nauli ukaone mjomba wako anaumwa
3. akupe pesa ya 40 ya mtoto wa kaka yako
4.hela ya dinner
 
Mimi nilikuwa nakaa mitaa jirani na aliyekuwa dem wangu,siku moja nimeumwa nikahitaji niandae dawa ya kunywa kwa kutumia blenda,,sikuwa na blenda ikabidi niombe aniazime,,Cha kushangaza alisema ile blenda haitoki kwake kuja kwangu labda nikatengenezee kwake kwa sababu anadai alipewaga na mzazi mwenzake ili awe anamuandalia juice mtoto wake,na mda huo ukizingatia haishia tena na mtoto kashampeleka kwa bibi yake ,Yuko peke yake geto.
Ikabidi nikubali kwenda kutengenezea kwake, nikamuomba anipe funguo zake nikatengeneze haf ataijia funguo zake kwangu,,lakini akasema hawezi kunipa funguo labda nikatengenezee kwake huku yeye mwenyewe akiwepo , ukizingatia Mimi nimeshampa funguo moja ya geto kwangu anakuja mda wowote anaotaka
#kwakweli iliniuma Sana na nikasema Kuna wanawake wabinafsi Sana duniani kama huyo dem
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…