Umewahi shuhudia mtu akifa mbele yako ghafla na hukuamini?

Umewahi shuhudia mtu akifa mbele yako ghafla na hukuamini?

Moshi miaka ya 1980s niliona vijana wawili wako kwenye bodaboda wanaongea kwa sauti kubwa tu, ile wamefika karibu na soko kuu wakauvaa mti, waliishia palepale

Miaka ya 1990s mbeya eneo la rrm kuna trafiki wawili walikuwa kwenye bodaboda wakaingia mtaroni, nilikuja sikia walifia palepale
 
Leo nimeona mtu akifa kama utani na mbele yangu.

Wakati nikivuka barabara ghafla mtu mwanaume aliyekuwa mbele yangu akaanguka kama kapigwa shoti ya umeme.

Akajibamiza vibaya sana chini na pote pakaanza kutapakaa damu, inatoka kila eneo la wazi la mwili.

Sababu ya butwaa nilikosa cha kusaidia ila wakaja wadau hapo wakasema ni kifafa huyo, jamaa keshameza ulimi n.k yaani kuna mzee akamgusa akasema huyo tayari kafa.

Basi ikawa ndio hata hatujui nini kifanyike

Ila ndio ikawa tayari amekufa. Nikaahirisha na safari nikarudi zangu nyumbani.

Umewahi shuhudia mtu kufa kimasihara?
Hakuna kufa kimasihara mkuu Mbwichichi huyo ndo tayari kafa.
 
Unaonaje ukituletea mambo uliyowahi kuyaona ambayo sio ya kawaida enzi ukifanya kazi mochwari, kufanya kazi mochwari kulianzaje, ulikuwa na hilo wazo kabla? au ilitokea tu kwenye harakati za maisha? vipi ile siku ya kwanza uliyoanza kazi, humo ndani palikalika?

Vituko vya mochwari
 
Umenikumbusha jambo moja lililotokea nikiwa na demu geto, ndani ya sekunde 5 nishapagawa.

Mwezi wa 7 nilikuwa na demu geto, baada ya kunyanduana tukawa tumelala. Sasa USIKU wa manane nilivyoshtuka, kumwangalia demu katulia tiiiii. Kumgusa kwenye mbavu akawa kama hapumui hivi! Oyaa, nilidata, nikajua ashavuta.

Basi nikamtikisa kwa nguvu sana ndo akashtuka anauliza NINI????

Nilivuta pumzi ndefu halafu nikalala Hata sikumsemesha
Demu alikuwa ameenda kuwanga
 
Mwezi wa tano mwaka huu mtoto wangu alikuwa kalazwa KCMC kwa shida ya moyo. Saa 7 usiku daktari akanipigia simu kuwa hali ya mtoto imebadilika ghafla. Niliwasha gari na kuelekea hospitali haraka na kufika tu dogo akanishika mkono akakata roho....

Natamani sana nisingepigiwa ile simu. Mzazi hapaswi kuzika mtoto bali mtoto ndio amzike mzazi
I can feel you,pole sana
 
Pole sana mkuu, imeniuma kama mimi ndio mzazi!!
 
Mwezi wa tano mwaka huu mtoto wangu alikuwa kalazwa KCMC kwa shida ya moyo. Saa 7 usiku daktari akanipigia simu kuwa hali ya mtoto imebadilika ghafla. Niliwasha gari na kuelekea hospitali haraka na kufika tu dogo akanishika mkono akakata roho....

Natamani sana nisingepigiwa ile simu. Mzazi hapaswi kuzika mtoto bali mtoto ndio amzike mzazi
Pole sana😭
 
Back
Top Bottom