Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

Hahaha jomba[emoji23][emoji23]
 
Dar moro siku mbili usiku na mchana. Barabara hiyo ina vibwengo kama wote. Sitaweza kusahau.
Acha uongo mwamba.
Wale tembo pale Ubena mpaka Bwawani walikukosa kweli!
 
Aiseee.
Nawe umetisha
 
Ulimaliza pea ngapi za viatu kwa mwezi/mwaka?
 
road to road mzee mpaka tandika, hapo nikapata shortcut moja nikatokea stendi ya shamba mbele ya mtongani kidogo, baada ya hapo ni kunyooka mpaka mbagala.

safari ilianza saa 12 jioni nikafika saa 6 usiku nilikuwa napumzika pumzika njiani umo
Kipande cha Vetinari, Tandika Majaribio, Tandika kaburi moja, Kizinga mpaka msikitini hukupata bahati ya kukabwa?
Maana muda huo na maeneo hayo ni "Tuwa tugawe"
 
Kwenye njia unazopita muda huo hali ya usalama inakuwaje ?
 
Mwaka 2018 kila jtano saa 12:00 asbh natoka pugu shule ya msingi hadi kivukoni. Kurud nilikuwa narud na bus. Nilijiwekea utaratibu huo kwa miezi 6
 
Naona Wanaume wa Dar mkilalamika kutembea km 5..... lol
 
2015 Lowasa
Buguruni hadi Biafra kupitia Posta
 
Kawe adi mnazi mmoja Via Old bagamoyo road, Ali Hassan Mwinyi Rd na Bibi titi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…