moudgulf
JF-Expert Member
- Jan 23, 2017
- 142,674
- 743,909
Hahaha jomba[emoji23][emoji23]Tabata to Manzese, hizi ruti nimefanya sasa nilipokuwa nasoma shule ya msingi zile siku za weekend nikipewa nauli sipandi daladala. Ila kubwa kuliko nilitoka Kiwanda cha Cement cha Wazo kule Tegeta hadi Mwenge nikiwa na miaka 12 tu. Ilikuwaje... Nilikuwa naishi Tabata nasoma Manzese na enzi hizo daladala zinatoka Buguruni zinapitia Tabata zinaishia Ubungo halafu napanda la Ubungo kwenda Kariakoo nashukia Manzese. Hivyo natakiwa kupanda Mabasi mawili, ile usumbufu wa makonda kuwakataa wanafunzi na kubadilisha magari muda unakwenda ikawa nikipata gari la lift napanda kuepuka huo usumbufu. Nikajenga mazoea, siku hiyo likaja basi la kiwanda cha Cement cha wazo nikapanda, kumbe lile gari likichukua wafanyakazi halisimani ni moja kwa moja hadi kiwandani. Nashangaa kufika Ubungo basi limeshika njia ya kwenda Mwenge na kwa utoto wangu sikuwa na ujasiri wa kuuliza gari inakwenda wapi au lisimame wanishushe. Aisee moja kwa moja hadi Kiwandani. Nashangaa watu wanashuka na kutawanyika na mimi sikuwa na jinsi nikashuka. Bahati nzuri basi ilisimama nje ya geti la kuingia kiwandani. Nikafuata barabara ya basi ilipotoka hadi Tegeta, nilikuwa sipajui kabisa Tegeta na nikawa na hofu nisipange gari nyingine nisije kupotea tena. Nikatembea kwa Miguu hadi Mwenge nikasikia wanatangaza magari ya Kariakoo nikapanda hadi Kariakoo kisha nikapanda basi la kwenda ubungo nikarudi nyumbani Tabata. Siku nzima nilimaliza na ilikuwa ni kipindi cha mitihani ya kufunga muhula. Sikusema nyumbani niliogopa ila shuleni nilidanganya nimefiwa wakanipa mitihani ya siku nisiokuja nikafanya peke yangu. SITOSAHAU!!!