Mchakato wa kupata hati ya kusafiria ulinifanya nitembee kwa mguu kutoka
Kurasini hadi
Mlimani City mchana wa juakali.
Ilikua hivi:-
Tangu wakati niko chuo nilihangaikia sana suala la kuwa na passport ili niweze ku "access fursa za dunia." (Najichukulia kama mwananchi wa dunia, na sio mwananchi wa kipande kidogo cha dunia kiitwacho Tanzania pekee)
Kwangu mimi, kutokua na passport ilikua ni kama kifungo (nilijifananisha na mbuzi aliyefungwa kamba shingoni na kamba hiyo kufungwa kwenye mti). Hivyo kuwa na passport ingekua kama kuikata ile kamba na kuweza "kula majani" popote pale ambapo ningeweza kufika.
A passport, was that important to me.
Kulingana na vigezo vya kuipata nyaraka hiyo ya kusafiria kuwa vingi, basi nilikumbana na "nenda rudi" nyingi sana hadi namaliza chuo sikufanikiwa kabisa kuipata hati hiyo.
Michakato hiyo (nenda rudi zisizozaa matunda) ilipelekea kupoteza pesa, kupoteza matumaini na furaha yangu.
Baada ya kupita kama mwaka mmoja na nusu hivi,
kwa mbinde sana nilitimiza vigezo vya kuomba passport (japokua nilikua sina uhakika navyo sana kama "vitanivusha") na
kwa mbinde zaidi nikapata pesa ya kugharamia mchakato huo.
Siku hiyo nimeenda pale uhamiaji makao makuu Kurasini, baada ya foleni kubwa, hatimaye nilifanikiwa kuhudumiwa majira ya saa saba mchana.
Nyaraka zangu zilipokelewa, zikakaguliwa, nikaambiwa nilipie, nikachukuliwa maelezo, nikapigwa picha na kuchukuliwa alama zangu za vidole na hatimaye nikaambiwa hati yangu itakua tayari baada ya siku 14.
Wakuu sikuamini, nilipata
WEPESI WA AJABU. Yaani mwili ulikua soft, light and energetic. Namtabasamia kila mtu aliye mbele yangu.
Nikaanza tu kutembea, a joyful walk, napita tu vituo vya daladala sina habari, yaani nilikua ni kama kichaa mpya mjini. Juakali la saa saba kuelekea saa nane, saa tisa linaniwakia sina habari mimi.
Nilienda kusimama Mlimani City, Samaki Samaki kwa kaka mkubwa Carlito nilipoagiza Pepsi bariiiiiidi inayoambatana na glasi zenye mabarafu na vipande vya malimao.
Moral of the strory;-
Kufanikisha jambo (lolote lile) mara baada ya kulipambania kwa muda mrafu, kunaambatana na RAHA FULANI ambayo haielezeki.
Asanteni.
Pia aione
Mwifwa