Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

Way back 2008/9 hv from posta to gongo la mboto..nakumbuka nilienda posta then siku hiyo mvua ilinyesha sana..kukawa na foleni kubwa sana..magari yanatembea taratibu..nilipiga mguu hd k.koo bado foleni lipo..nikatembea hadi tazara bado..nikavuta hadi Airport hali ni ileile,gari zinaenda taratibu na watu wengi waliamua kutembea tu..basi nikapata kampani mpaka gongo la mboto
 
Sijui kulitokea shida gani ya Magari!!Sikuhiyo tulitembea kwa Miguu mimi nikianzia Posta Mpaka Kinyerezi Pale Mbuyuni..
 
Ubungo - mnazi mmoja - kivukoni - jangwani - ubungo via morogoro road. Nilikuwa nainjoi tu kunyoosha miguu sikuwa na shida yoyote, mfukoni nilikuwa na hela ya kutosha tuu
 
[emoji3][emoji3][emoji3]taifa mpaka chanika

Kuna mwanangu mmoja baba yake alitupeleka kuangalia game ya Simba na yañga na tiketi akalipa Sasa yanga alivopigwa tu yule mzee alitukacha afu mfukoni Nina mia Saba ikabidi tule kashata za mia sita na maji ya kandoro ya hamsini hamsini kipindi hicho. Kisha tuanze kugonga one two
Nchi ii ina wazee wa ovyo sana [emoji22] [emoji17]
Ila nimecheka sio pw mkuu
 
Mbagara rangi tatu mpaka keko

Siku iyo nilienda kumsalimia bamdogo kibulugwa sasa jioni nikagewa elfu moja yanauli nanakumbuka nauli ilikuwa 100 kwawanafu hivyo nikapiga esabu mia nane ii natamba shule nanilikuwa primary' saa ile nafika zakhiem si ndo nikawakuta wale jamaa wanaozungusha mkanda alafu kati kunakuwa namatundu mawili wanakupa peni ubaatishe

basi si ndio nikasogea ili nione inakuwaje watu wanakosa wakati jamaa anazungusha tu mkanda taratibu' aaaaaaaa asalaleeeee ile nasogea tu nikashangaa watu walikuwa wengiiiii mpaka sioni ila ghafla nikakuta nimeachiwa njia naile nimelisogelea boksi tu nikajikuta nipo kat kat uku nimezungukwa nawatu pande zote alafu mchezeshaji anavyochezesha amenilenga mm direct

heeee nikaambiwa dogo kujaribu bule naukiweka elfu tatu unapata elfu sita kabla sijaongea chochote nikashikishwa peni nijaribu bule nisitoe ela' ile najalibu nikapata nanikaskia watu wanashangilia eeeeee kapata nawadada walikuwepo wanasema we mkaka mpe dogo elfu sita yake, wale wengine wakasema uyu dogo fala kaambiwa aweke ela hajaweka angekuwa na elfu sita mda uu' sasa ikatokea njemba moja ina kipala kinang'aa atari cjui kapaka namafuta yavitumbua

akaniuliza kwani we dogo mfukoni una bei gani? nikamjibu nina elfu moja nakumbuka iyo ela ndo yanauli ujue' daaaah bas ile njemba ikanambia saa siuweke ilo buku uchukue elfu mbili, bas chap nikasema shuleni kesho watanikoma vishet vya shilingi tano tano nakula namasela vyakubuku mbili' nikashikishwa peni jamaa kazungusha mkanda mimi jicho limenitoka kwenye mkanda kama nimedondosha nati ya simu nipo makini sio powa nikachomeka daaaah
 
Back
Top Bottom