Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

Tupe kidogo Mikasa ya huko barabarani mkuu mkutembea kwa miguu toka Moro - Dar simchezo,,,

maana hii hali iliwahi kukaribia kunitokea siku moja, bado kidogo sana nitembee kwa miguu kutoka msavu hadi ubungo!

Bahati njema alitokea msamaria mmoja nisiye mjua akanisaidia nauli 5000 wakati huo nauli ya Moro - Dar ni 2500 , nilikaa stand ya msavu toka asubhi mpaka jioni bila bila,,, msamaria huyo alinipa nauli imeshakuwa jioni sana karibu saa moja na dakika zake usiku!

Nikapanda coaster ya mwisho kabisa kuja ubungo! Tukafika Ubungo mida ya saa tano usiku! Kisha nikachukua daladala hadi k/koo then nikachukua lingine la kuja home Kurasini, nilifika home saa saba usiku!

Sitasahau! Yule msamaria Mungu ambariki sana kokote aliko!
Sasa ungetembeaje Dar hadi Moro kwa mguu jombaa wakati kuna kipindi flani ubena Zomozi kulikuwaga na wanyama kabisa Chui unawaona Road kabisa. 🤣🤣🤣
 
Enzi za kwenda kuogelea Coco Beach unatoka Magomeni unapitia rafiki Kinondoni mnatembea mpaka Coco Beach, mnaogelea kisha mnasogea kwa kutembea mpaka Dar Yatch kushangaa Boti, Slip Way mkifika Msasani Fish Market hapo ni kutembea kando ya Bahari ufukweni mnapita kwa Nyerere nyuma ya nyumba, Dar Independent School, Mbalamwezi Beach, Kwa Mzee Bomani, Mzee George Kahama, Escape One Beach Mpaka Kawe Beach hiyo jioni mpo hoi.

mnarudi kwa njia za chochoro Mikocheni B, Wastaafu street, Warioba mnapita barabara ya Lucy Lameck nyuma nyuma mpaka mitaa ya Kairuki kuitafuta Morroco na Kinondoni unafika Magomeni hoi nguo zina mchanga kichwani mchanga.

Saizi kuipita route hizo kasheshe
Hahahahah kwa hili jua la milenia ukiweza tembea kilometre moja tu hapa Dar wewe ni mwamba
 
G/Mboto from Mzambarauni via Jet via Buguruni via Tabata Relini, nikatokea Ubungo, nikanyooka hadi Shekilango hadi Sinza Vatcan..... hii ilikua 1994, na mwisho wa daladala toka K/Koo, Posta nk ilikua ni pale G/Mboto Mzambarauni kabla ya Scolla House haijajengwa kmmk walahi...
Baharia ulikuwa unafata kisamaki kwa Ng'ondi kudadadeki
 
Nakumbuka siku moja nikiwa Msasani alitokea kijana mmoja akaniomba nimtembeze kwenye mtumbwi.

Ila kwa bahati nzuri kukawa na boti linaenda Kigamboni siku hiyo, basi bhana nikamuunganisha akaniambia tuende wote mpaka taifa tukaangalie na Mpira kati ya Yanga na Mbeya city.

Alifurahi sana tulipofika Kigamboni tukapanda panton tukavuka posts tukaenda kupanda magari ya rangi tatu, basi bhana tulipofika akaenda kukata ticket kwenye gari akakata ya kwake tu akaniambia nimsubiri, anaenda kutoa hela kwenye simu, nikamuamini poa tu japo nilishashtuka ila nikawa najipa moyo.

Mpaka Mpira unaanza hakutokda ila bidi nianze kupiga ado ado na mguu mpaka msasani.
Kutoka Coco beach hadi kurasini, hiyo siku ilikuwa Boxing day ya Christmass nikiwa na wanangu wa damu tulipiga "pedeli" kutoka Coco beach hadi mitaa ya kurasini baada ya kukosa usafiri ilibidi tufanye maamuzi magumu.
Picha limeanza tumemaliza kuogelea tukasema twende tukachukue gari za kurudi kitaa, bahati mbaya kule ushuani hakuna daladala za kuja kurasini moja kwa moja na zote zilizokuwa zinakuja zilikuwa zinajipangia nauli ambayo mimi na watoto wa mbwa wenzangu tuliona haiko fair (tulikuwa na misimamo ile ya kijamaa).

AZIMIO LA COCO BEACH:
Basi tulikubaliana na wana tupige "pedeli" kutoka Coco beach mpaka posta ambapo kipindi hicho kulikuwa na hiace za Tandika-Posta. Kufika Posta gari hakuna, kumbuka miaka hiyo kuna ile michezo ya watu kukodi gari kuwapeleka beach hivyo ikapelekea uhaba wa usafiri. Kamati ikakaa na kuja na azimio dogo baada ya lile la awali kugonga mwamba.

AZIMIO LA POSTA:
Basi kamati ya Wazalendo ikiongozwa na mimi tukakubaliana tusogee mpaka hapo Stesheni maana kulikuwa na hiace za Temeke-Stesheni kupitia barabara ya kilwa zingetufaa sana kama tukishukia Police ufundi au Jkt basi kurasini sio mbali kabisa.
Tulianza mdogo mdogo kuelekea Stesheni lakini kwa bahati mbaya au nzuri hiyo siku ilipangwa tufanye matembezi ya hisani bila kuwa na ajenda yoyote ile.
Baada ya kufika Stesheni hali ilikuwa ni ile ile tu kama ya Posta ikabidi kamati iende "chemba" kidogo.

AZIMIO LA STESHENI:
Baada ya wataalamu wa kusoma ramani na kutafsiri picha (MAP READING AND PHOTOGRAPH INTERPRETATION) kumaliza kikao kidogo likazaliwa Azimio la Stesheni.
Wataalamu walibaini kuna njia za mkato nyingi ambazo tunaweza kuzitumia kama askari wa miguu kuweza kufikia target bila kuchoma nauli kwa kutumia usafiri usiohitaji nishati ya Mwarabu.
Basi tulianza mdogo mdogo story nyingi sana na kujipa moyo kwamba palipoaki ni padogo sana ukilinganisha na tulipotoka.
Ukizingatia kipindi hicho tulikuwa tumeshaanza kupita Dojo na kupikwa vilivyo huo umbali ulikuwa wa kawaida sana na kuona kama mazoezi tu ya ukakamavu.
Tulifika kurasini kwa wakati kabisa japo kigiza kilikuwa kimeshaanza kuingia lakini hakuna aliyejua kuwa tulipitia changamoto gani siku hiyo.
Ile kamati hakika ilitoa wazalendo wa kweli ambapo kwasasa wanalitumikia Taifa mikoa mbalimbali hapa nchini
 
42km kwa mkimbiaji nzuri na kimashindano ni masaa 2+
Weweeee 59km kwa masaa 10 ilikuwa n milima gani hiyooo ulipanda mkuu
Usichukulie poa hiyo pace ya marathon runners, years of training
 
Sasa ungetembeaje Dar hadi Moro kwa mguu jombaa wakati kuna kipindi flani ubena Zomozi kulikuwaga na wanyama kabisa Chui unawaona Road kabisa. 🤣🤣🤣
Kwani vijijini watu wanatembeaje? Mfano ukiwa Vuma lodge IPO ndani ya mbuga ya mikumi, kutoka restaurant mpaka kota za wafanyakazi kuna distance halafu usiku Giza na generator inazimwa SAA 4 usiku.

Pia nakumbuka kitambo Nilikuwa na jamaa yangu ni marehemu sasa hivi tulichelewa usafiri tulitembea kwa mguu kutoka Bagamoyo mpaka Bunju, na kipindi hicho Mapinga kuna Simba.

Bunju tulifika usiku mkubwa tukakaa stand mpaka alfajiri Daladala za kwanza za kariakoo ndio tukapata usafiri.

Mungu ni mkubwa sana.
 
Kwani vijijini watu wanatembeaje? Mfano ukiwa Vuma lodge IPO ndani ya mbuga ya mikumi, kutoka restaurant mpaka kota za wafanyakazi kuna distance halafu usiku Giza na generator inazimwa SAA 4 usiku.

Pia nakumbuka kitambo Nilikuwa na jamaa yangu ni marehemu sasa hivi tulichelewa usafiri tulitembea kwa mguu kutoka Bagamoyo mpaka Bunju, na kipindi hicho Mapinga kuna Simba.

Bunju tulifika usiku mkubwa tukakaa stand mpaka alfajiri Daladala za kwanza za kariakoo ndio tukapata usafiri.

Mungu ni mkubwa sana.
Hahahhahaha mlikuwa mnakaza mno mafuvu🤣
 
Na sisi machinga tunaruhusiwa kuchangia
Yaani wewe ndio umemaliza katika wote,ujue kutembea umbali flani kuna sababu tofauti na inategemea na hali ya kiuchumi kwa wakati husika mfano huyu mtu aliyeuliza je sisi machinga tunaruhusiwa kuchangia? Kiukweli hawa jamaa wanatembea sana na kwa ukaazi wangu nishawashuhudia wamachinga ambao wanauza bidhaa maeneo ya mbali sana mfano kuna mmoja alikuwa namkuta sana maeneo ya tmk sasa siku hyo nikamkuta maeneo ya Bonyokwa tena kabeba yale majiko ya mkaa yale yenye udongo ndani,ebu fikiria lilivyo zito tena na pima tmk to bonyokwa na hapo anapita kuelekea kimara!
 
Back
Top Bottom