Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

Sijaona alietembea humu , sisi tunatembea tumebeba na vyakula kabisa...Yani mnaanza safari jua alijatoka mnafika linazama ,ni usiku.
 
Nakumbuka siku moja nikiwa Msasani alitokea kijana mmoja akaniomba nimtembeze kwenye mtumbwi.

Ila kwa bahati nzuri kukawa na boti linaenda Kigamboni siku hiyo, basi bhana nikamuunganisha akaniambia tuende wote mpaka taifa tukaangalie na Mpira kati ya Yanga na Mbeya city.

Alifurahi sana tulipofika Kigamboni tukapanda panton tukavuka posts tukaenda kupanda magari ya rangi tatu, basi bhana tulipofika akaenda kukata ticket kwenye gari akakata ya kwake tu akaniambia nimsubiri, anaenda kutoa hela kwenye simu, nikamuamini poa tu japo nilishashtuka ila nikawa najipa moyo.

Mpaka Mpira unaanza hakutokda ila bidi nianze kupiga ado ado na mguu mpaka msasani.
Sinza Mori hadi Sinza Mapambano
 
ila Mbeya nishawahi tembea toka mwanjelwa hadi shuleni (Iyunga) nilikula nauli 200 tu form one hata kuomba kwa konda siwezi sitasahau
 
Palm beach hadi mwenge,kinondon manyanya hadi mwenge hizi nimezipiga sana kila mara yaani nikitoka xul ,ila kubwa kuliko ni kkoo to mwenge
 
Kariakoo - Kinondoni studio.
Buguruni - Mawenzi.
Buguruni - katakana.
Gomzi - Jitegemee.

Ni matunda ya kula nauli, kununua nguo/viatu..,
Hii ya mwisho Ilikua usiku na nikadakwa na wajeda wakati naruka ukuta, ila tulikua wengi.

Hio ya pili Ile nafika tuu nyumbani nahojiwa mbona umechelewa?? ile najibu tuu, nikarudisha chenchi seble nzima.
 
Humu sijaona ruti ndefu ya mtu hata moja, mimi nilikuwa natoka kibamba mpaka kibada na ni kila siku, nilikuwa natembea bila kujua kuwa ni mbali mpaka pale nilipozoea jiji zima nazunguka kwa miguu tu, sikuwahi kupanda daladala mpaka narudi kijijini kwetu Magera, Morogoro.

Kumbe na wewe ni wa moro.

Mimi nimekaa moro town miaka 3 na nimejenga kibanda changu hapo.

Mimi na uhaya wangu ila huniambii kitu moro napapenda sana
 
Mbezi beach high school mpaka wazo hill enzi za mgomo wa daladala kipindi cha jakaya hiyoo wazeee nililala siku mbili hom koz ilikuwa ijumaa hivi wakuuu
 
Nilikuwa natembea kutoka tabata shule mpka Ukonga Mombasa maeneo ya relini, nanyoosha mpaka buguruni kwa mnyamani kwa shortcut nakata mpka veta nanyoosha mpka Airport mpka home. kipindi kile nauli ilikuwa 20 Tsh

Nikiwa darasa la 4 na ni kwasababu tulikuwa tunakaa tabata sasa tukahamia kwetu ukonga na darasa la 4 ilikuwa ngumu kuhama kama mtu kasajiliwa mtihani kweny shule husika
 
Yale mabomu ya G/mboto[emoji23]

Kutoka g/mboto rada chuo hadi ubungo but sielewi nilifikaje na sitaki kukumbuka hii kitu.
 
Back
Top Bottom