Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi ninayo barrier hybrid hivyo nadhani msaada nitauhitaji siku ikifika
Kwa ushauri wangu achana nayo mkuu kama unapesa za kuunga unga hasa kipindi hichi cha anko magu..nakwambia hivyo coz ugonjwa mkubwa na hata wao huko nje wanaziuza kwasababu ya betri yaani shida sio kucharge ishu ni kwamba betri zinakufa .yaani zikishafikia kipindi haziwezi kuhifadhi sana moto ndio basi tena za kubadilisha na ujinga wake kwa wastani betri moja complete huwa na betri 30 zilizounganishwa series hapo betri moja au mbili zikuwa mbovu basi zinatia ubovu betri yote yakupasa ubadilishi hizo zilizokuwa majanga...
Hahahahaha mkuu mm siwatishi nasema ukweli wa lile ninalolifaham..toyota ni wauza spare niamini mm mzee ..nishafika kote huko toyota na cifao hakuna motor mafundi wote wa umeme wa toyota nawafaham na namba zao ninazo kuna kipindi nilikuwa natafuta sana chargi yakuchajia hizo betri nilikosa ikabidi niyengeneze ya kwangu yakienyeji nikafanikisha nilichokuwa nahitaji kukifanya gari ikawaka fresh tuu..
Nikakutana na gari ya pili ikiwa down kabisa ikanibidi niagize charger ya kuchajia ..
Ugonjwa mkubwa wa hizo gari ni betri maana hybrid battery zipo 30 zimeunganishwa series na moja inakuwa na 7.5 mpaka 9.kadhaaa hapo inategemeana na aina ya gari.ambazo ukijumlisha unapata kuanzia 260 kwenda juuu..
Sasa kama betri moja ina 7.5V unshindwaje kuchaji??.
Ugonjwa mwingine mkubwa ni inverter cooling motor ikifa hiyo gari inazingua sana mwishowe betry zinakwenda down..
HYBRID IPI BORA KATI YA YA UMEME AU YA MAFUTA?
Mkuu twende taratibu ..najibu kwa kile ninachokifaham labda nikuulize gari nyingi za toyota hazina plug IN hasa zile zitumiazo mafuta na umeme lk. Kwa gari itumiayo umeme tuu lazima iwe na plug in na hata nyingi zenye umeme na mafuta zina plug in pia.wew unabisha kuwa betri hazichajiwi labda nikuulize je ikitokea cell moja ya betri imekufa na kusababisha nyingine kwenda down itakuwaje?? Gari ndio imekufa?? Kwasababu gari haina plug in??.jibu ni hapana...
Ukweli ni kwamba hybrid cars ni gari bora zaidi na tunapoelekea miaka michache ijayo hizi ndizo gari zitakazotawala soko la dunia. Mfano, mwaka ujao Toyota watayoa Landcruiser V8 hybrid.Aha niljua tu ..sasa hiyo si battery moja kama ni hizo ndo umepima ukapata volt 7 sijui 9 basi jua humo ndan yake kuna battery kadhaa tena sababu hama single battery yenye volt hizo
Tatizo siyo hali zetu. Siwezi kupata uwezo wa kuagiza gari ya zaidi ya $10000 afu nikashindwa kuagiza spare ya $2000. Dunia ameishakuwa kijiji, tunanuna online, cash kupitia makampuni kama Beforward nk.Gari nyingi moya zikitoka mafundi wa nchi utukatisha tamaa eti hazifa lkn mwisho wake uja kuwa gari bora zaidi ktk sokoHahahaha mkuu maintanance ya hybrid car nigarama sana..hata kama zinatibika kwanza changamoto kubwa zaidi ni spare..hapa bongo hakuna spare kabisaa za hybrid car..hasa zikiharibika upande wa hybrid ingawa uhalibikaji wake mkubwa ni betri na betri sio yote bali ni piec chache..
Nasema watu wasiagize coz hali zetu zinafahamika coz hata magari 80% tunaagiza magari chakavu toka nje na hayo magari mengi yanakuwa yashaharibika au fikia kwenye kuharibika ndio maana wanaziuza..lkn kama mtu unanunua 0km haina shida sana.
Inakupa kms ngap kwa litaUkweli ni kwamba hybrid cars ni gari bora zaidi na tunapoelekea miaka michache ijayo hizi ndizo gari zitakazotawala soko la dunia. Mfano, mwaka ujao Toyota watayoa Landcruiser V8 hybrid. Mafundi wetu wa Tanzania wanapashwa kubadilika, wajifunze kuendana na Tecnolojia kuliko kuipinga kwa kutukatisha tamaa eti tusinunue gari za kisasa. Mimi nina Harrier hybrid sijaona tatizo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli zina battery mbili, ya mbele naya nyuma? Maana najipanga hapa nichukue toyota aqua ya 2014![]()
![]()
Hiyo Auris Hybrid ninayo haijawahi kusumbua nilienda nayo moshi kupitia bagamoyo nilitumia lita 25
Ni kweli zina battery mbili, ya mbele naya nyuma? Maana najipanga hapa nichukue toyota aqua ya 2014
Prius inafika sababu on low speed haitumii mafuta kabisa mpaka kuanzia 80KPH40km kwa 1liter?? Hata boxer za wahindi hapa bongo hazitumii hivyo.
Battery mpya ni ghali ila kwa kudumu yanadumu sababu ni Toyota hilo sina shaka nalo!hizi gari ni nzuri kwa fuel consumption baadhi 1L inaenda mpaka 56km, inategemea na jinsi unavyoliendesha kwasababu kama unaendelesha below 60 or 40km/h (sina uhakika) linatumia umeme hivyo una save fuel lakini sijajua gharama ya maintanance ya huo mfumo especially durability and cost of repalacing new battery.
Hio ni ngumu kweli hata siti zake ni ngumu kama jiweJamani mimi ni SUZUKI KEI (Kaitazame Google) ina 650cc na haina shida kabisa na ni kagumu balaa kamefanana na SWIFT
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu inategemea generation gan.. plug in prius ndo ina high mileage on EV modePrius inafika sababu on low speed haitumii mafuta kabisa mpaka kuanzia 80KPH
Umeaua kabisa, shida tunarudi pale pale hapa bongo wataalamu wa hizi gari, kwa ajili ya service za kawaida na maintance nyingine wapo?Naomba ntoe elimu kuhusu hybrid car.
Gari hybrid kuna za aina mbili. Kuna ambayo ina mpaka mfumo wa kucharge kama simu(plug-in hybrid) na hybrid car isiyo kua na sehemu ya kucharge kwenye soketi ya umeme(non plug-in hybrid car)
Sasa for car to qualify to be hybrid car ni kwamba inakua na injini na high voltage battery (lakini pia inakua na betri ndogo ya gari kama hizi tulizozoea)
Na inakua na mota mbili (MG1 na MG 2) hizi mota moja MG2 ndio inayopeleka nguvu kwenye matairi na hii mota pia huwa. Imeungwa kwenye injini ambapo wakati nguvu nyingi za kupush gari zinapo hitajika basi injini uingia kati na kusaidiana na mota (MG2) kutembeza gari.
Mota ya (MG1) kazi yake yake ni kuchaji hy voltage battery wakati injini inapokua inawaka na pia hii ndio mota inayo washa injini pia. (Kumbuka hybrid car haina starter.
Kazi ya high voltage battery ni ku power MG1 mota, ku power ac compressor (kumbuka compressor ya hybrid car hizungushwi na belt kama conventional car, na pia hii hybrid battery (high voltage battery) ndio inayo charge ile betri ya v 12 kupitia mfumo wa DC to DC inverter (hii betri ya volt12 ni ku kupower all 12v electric equipments kama radio,taa za gari ntc
Sasa hybrid car inavofanya kazi ni kuna kitu kinaitwa hybrid management system kipo pale mbele ya engine compartment (primary computer for hybrid car).. kazi ni kumanage mfumo mzima wa high voltage na hybrid. Hapa ni kwamba injini inafanya kazi kama jenerata inachaji betri. Then betri ikifika level ambapo kumpyuta itaona inafaa injini inazima ila vitu vingine vinaendelea kama ac operation, car movement pale betri ikienda low voltage utasikia injini inawaka yenyewe kucharge betri tena.. hapa ndo fuel efficiency ya hybrid cars inapotokea..
kwa hybrid ambayo unachaji pia kama tesla yenye inakua imeongezea source moja ya kucharge hybrid battery.. ambapo unaweza toka nyumban battery imejaa charge baada ya kucharge usiku kucha, gari ikatembea,, sasa charge ya betr ikikaribia kuisha automatically engine itawaka kuichaji betri huku gari inatembea badae kama sekunde 3 kama gari ipo stationary ijini itazima ila kama gari inatembea injini inaweza waka dakika moja then ikazima yenye ukaendelea na umeme( kuifupi driving circumstances ndo zina determine frequency ya injini kuwa na kizima)
Hybrid car zinakitu kinaitwa regenerative braking. (Unapofunga brake badala ya gari kutumia brake calipers kufunga brake ni MG1 mota ita engage na injini inazima alafu tairi zinaizungusha MG1 mota kwa ajiri ya kucharge hybrid battery. Na ndo maana ukiwa unaendesha hybrid car ukifungu brake utaona bars za battery zinaongezeka. Na pia kwakua brake hazitumiki sana, brake za hybrid cars hudumu muda mrefu sana kuliko gari za kawaida.
Hybrid car zipo na mode kadhaa za kuendesha gari(driving mode) 1 kuna EV(yaan electric mode only) 2 (Hybrid mode-yaan injini na mota vinafanya kazi kwa wakati mmoja kuendesha gari 3 ECOMode yaaan hapa gari ino- monitor inputs zake kwenye throttle pressings zako na yenye ku respond taratibu mpaka una gain moment ya ku accelerate fast. Pia kuna power mode hii sasa kama unataka drive aggressively. (Every driving mode has its own impact kwenya fuel consumption)
Now how to maintain hybrid cars (ishu kubwa najua ni betri) Hybrid cars are supper reliable (Toyota tu maana ndo wapo kwenye game mrefu) shida kubwa kinacho ua betri na joto.. like any other batteries, betri za hybrid cars zina ventilation mechanisms Ambapo zina hitaji proper air circulation kwa ajili ya cooling(ukiwa na hybrid car mfano toyota Prius kwenye kiti cha nyuma kuna mahala utakuta kuna vents, hizi vents ni for fan to suck in air for cooling battery sasa huwa kuna filter ambayo with time hujaa vumbi na kua affect airflow volume na hatima battery kuchemka na kuanza kupoteza storage capacity, ila ukizingatia kusafisha filters gari inakaa muda mrefu sana. Imagine prius zinafika mpaka km400,000 with original battery..
Pia hizi battery huwa zinakua na pack za betri za volt kama 1.5 ambazo zina pangwa in series mpaka zinafika volts 300+ sasa kuna kua na battery modules zinazo monitor every single cell ya kwenye hybrid battery, so kukitokea kuna variation kubwa ya voltage discharge hata kwa cell moja, red triangle itawaka kiashiria kuna tatizo kwenye hybrid battery. So ukichomeka scanning machine ambayo ni advance itakuonyesha ni cell zipi zinashida.. so badala ya kununua hybrid battery yote fund anaweza fungua battery backs na ku replace pack ilio nashida akafanya battery balancing akarudisha maisha yakaendelea (note: hybrid system involves high voltage DC and AC na wire zake utazitambua kwa rangi zinakua na rangi ya orange hivo fundi wakutengeneza hii gari should be professional person who knows how hybrid system works lasivo mtu anaweza poteza maisha)
Ila msi site nunua Hybrid cars.. tena ukiwa ni mtundu hybrid car can be used as generator to power a house-using dc to ac inverter. Ambapo dc cables zinatika kwenye betri ya v12 unazipeleka kwenye inverter, then inverter ina convert ile v12 to Ac 220v na watt 2000 kama inverter yako ni ya watt 2000 baada ya hapo you have proper off grid electricity to power your various electric equipments. Angalia wazungu wanavo fanya camping na toyota Prius hadi uta enjoy..
Naomba niishie hapa.