new generation
JF-Expert Member
- Mar 14, 2012
- 817
- 1,687
Mafundi wapo...Umeaua kabisa, shida tunarudi pale pale hapa bongo wataalamu wa hizi gari, kwa ajili ya service za kawaida na maintance nyingine wapo?
Hybrid cars zipo na service costs ndogo kuliko conventional cars... Mfano na zenyewe zinatumia oil kwenye injini ila frequency ya kuchange engine oil si kubwa kama gari yakawaida kwakua Hybrid car injini huwaka mda mchache na kuzima... Tena ukiwa kwenye folen mfano na ac ipo on... Utaona injini inazimika baada kama dakika 4 utasikia inawaka kwa ajiri ya kuchaji battery then itaunguruma kama sekunde 20 itazimika but functions nyingine zote zitaendelea kufanya kazi kwakua kichafanya kazi ni umeme tu. Hapo hata oil aichoki haraka kama oil ya kwenye gari ambayo si hybrid..
Na kumbuka regular service ya gari ni oil changing pomoja na filter yake (oil ya hybrid car kama upo tz at least 5w-30 fully synthetic oil usiweke hizi oil za kawaida kama sae 40 au hizi wengi wamezoe ya 20w-50), airfilters changing (both engine and cabin-ile ya ac) na brake pads sasa kwa Hybrid hivi vyote vinachukua muda kubadirisha... Hasa brake unaweza kuta gari inafikisha hadi km 200,000 ujawah badiarisha brake pads kwakua brakea zake hazitumiki mara kwa mara(regenerative braking ndo ufanya kazi mara nyingi)
Vingine ni vya kawaida.. ishu kama plug, kubadiri betri ile ya volt12, kusafisha egr valves kama ikijaa carbon, shocks absorbers na buahing hizi zipo hapa bongo (kumbuka uzuri wq toyota vitu vingi vya gari zake vinakua standard ni kufanya kuweza kuingilia kwa baadhi ya vitu vya gar zake hasa huku kwenye suspension systems
And the other major components they are too reliable (vitu kama car computers, engines, hybrid batteries, both motors yaani MG1 na MG2 zito za patikana ingawa kwakua hizi ndo za tengeneza transmission system, ikitokea zimekufa wewe nunua gearbox mpya kama tunavofanya hizi gari za kawaida.
Na ikitokea issue ni battery ya Hybrid ndo imekufa kuna namna nyingi na cheap ya kurekebisha kama fundi anajua achofanya. Unless una replace battery pack nzima ambayo haichukui hata nusu saa kubirisha..
Zingatia maji yasiingie mahala battery inakaa... Unapokua na hybrid car jitahidi kujua location ya battery zote mbili ili ujui namna ya kuilinda na maji.. pia kuzingatia kusafisha filter ya hewa inayokaa kwenye hybrid battery (maana hii ndo chanzo kikuu cha kuharibika kwa hizi battery) hakikisha battery inapata hewa ya kutosha.. (hizi gari kuna ambazo zina battery ya lithium ion na nyingine ni nickel cadmium sasa kila battery ina advantagea na disadvantages zake ingawa zote zinatengeneza joto zinapokua zinafanya kazi kama vile betri za simu.. sasa zinahitaji hewa ya kutosha ili ziweze kufanya kazi na kudumu kwa muda mrefu... Na kwa namna toyota walivo design kila battery pack inayotengeza hybrid battery ina temperature sensor kwa ajili ya monitoring ya temperature for every individual battery pack.. hii inasaidia effective protection ya battery when subjected to high temperature beyond required range..na hii ndo utakuta kuna fan ambayo inakaa kwenye kiti cha abiria kwa chini (kwa Toyota Prius) ambapo rotation speed yake inabadirika kulingana na temperature level ya battery. (Kwa watu wa dsm kama una gari Hybrid tumia AC as much as possible unapotumia hii gari hii itasaidia feni ya battery ku suck in cool air ambayo itakwenda kupoza battery..
Pia hii gari ni rahisi kufanya diagnosis kwa kutumia diagnostic machines kwakua zinakutajia specific problem na hata kama nu battery unaweza zoom in kwakila battery pack individual na ukajua ni pack gan ubadirishe na kufanya charging balancing ili battery zote ziwe even kwenye charging na discharging.
Zingatia tu kua kwenye mfumo wa uzungushaji maji ya kupozea injini kuna ambazo zinakuja na electric water pump na kuna zinazokuja na non electric water pump-ambayo inazungushwa na timing chain..so kwa zinazokuja na electric water pump when check engine light is on haraka saana weka gari pembeni chunguza chanzo cha hiyo check engine light..kwakua kwa hii gari yenye electric water pump the only way kujua kua ni water pump ndio imekufa is through check engine light illumination.
Kitu kingine cha kujua hii gari unapata a very good gas mileage kwenye trip za mjini kwakua muda mwing regenerative braking system inafanya kazi(zile stop and go zinafanya regenerative braking ina jaza chaji battery wakati wa kusimamisha gari but for high driving kwa speed 90+ gas mileage inashuka kidogo kwakua muda mwingi injini inawaka ku keep up with driving needs za dereva..so hapa both engine na MG2 motor zitakua zafanya kazi kwa pomoja ili kutoa nguvu dereva anahitaji kwa ajili ya hiyo speed ya juu, the reduced fuel efficiency at high way speed isnt that much because of absence of regenerative braking....
Unless otherwise hii gari ni gari nzuri sana mkuu.. na huto jutia kuinunua..