Umewahi ziona hybrid cars hapa bongo? Je, zinastahimili changamoto mbalimbali? Wataalamu karibuni!

Umeaua kabisa, shida tunarudi pale pale hapa bongo wataalamu wa hizi gari, kwa ajili ya service za kawaida na maintance nyingine wapo?
Mafundi wapo...

Hybrid cars zipo na service costs ndogo kuliko conventional cars... Mfano na zenyewe zinatumia oil kwenye injini ila frequency ya kuchange engine oil si kubwa kama gari yakawaida kwakua Hybrid car injini huwaka mda mchache na kuzima... Tena ukiwa kwenye folen mfano na ac ipo on... Utaona injini inazimika baada kama dakika 4 utasikia inawaka kwa ajiri ya kuchaji battery then itaunguruma kama sekunde 20 itazimika but functions nyingine zote zitaendelea kufanya kazi kwakua kichafanya kazi ni umeme tu. Hapo hata oil aichoki haraka kama oil ya kwenye gari ambayo si hybrid..

Na kumbuka regular service ya gari ni oil changing pomoja na filter yake (oil ya hybrid car kama upo tz at least 5w-30 fully synthetic oil usiweke hizi oil za kawaida kama sae 40 au hizi wengi wamezoe ya 20w-50), airfilters changing (both engine and cabin-ile ya ac) na brake pads sasa kwa Hybrid hivi vyote vinachukua muda kubadirisha... Hasa brake unaweza kuta gari inafikisha hadi km 200,000 ujawah badiarisha brake pads kwakua brakea zake hazitumiki mara kwa mara(regenerative braking ndo ufanya kazi mara nyingi)

Vingine ni vya kawaida.. ishu kama plug, kubadiri betri ile ya volt12, kusafisha egr valves kama ikijaa carbon, shocks absorbers na buahing hizi zipo hapa bongo (kumbuka uzuri wq toyota vitu vingi vya gari zake vinakua standard ni kufanya kuweza kuingilia kwa baadhi ya vitu vya gar zake hasa huku kwenye suspension systems

And the other major components they are too reliable (vitu kama car computers, engines, hybrid batteries, both motors yaani MG1 na MG2 zito za patikana ingawa kwakua hizi ndo za tengeneza transmission system, ikitokea zimekufa wewe nunua gearbox mpya kama tunavofanya hizi gari za kawaida.

Na ikitokea issue ni battery ya Hybrid ndo imekufa kuna namna nyingi na cheap ya kurekebisha kama fundi anajua achofanya. Unless una replace battery pack nzima ambayo haichukui hata nusu saa kubirisha..

Zingatia maji yasiingie mahala battery inakaa... Unapokua na hybrid car jitahidi kujua location ya battery zote mbili ili ujui namna ya kuilinda na maji.. pia kuzingatia kusafisha filter ya hewa inayokaa kwenye hybrid battery (maana hii ndo chanzo kikuu cha kuharibika kwa hizi battery) hakikisha battery inapata hewa ya kutosha.. (hizi gari kuna ambazo zina battery ya lithium ion na nyingine ni nickel cadmium sasa kila battery ina advantagea na disadvantages zake ingawa zote zinatengeneza joto zinapokua zinafanya kazi kama vile betri za simu.. sasa zinahitaji hewa ya kutosha ili ziweze kufanya kazi na kudumu kwa muda mrefu... Na kwa namna toyota walivo design kila battery pack inayotengeza hybrid battery ina temperature sensor kwa ajili ya monitoring ya temperature for every individual battery pack.. hii inasaidia effective protection ya battery when subjected to high temperature beyond required range..na hii ndo utakuta kuna fan ambayo inakaa kwenye kiti cha abiria kwa chini (kwa Toyota Prius) ambapo rotation speed yake inabadirika kulingana na temperature level ya battery. (Kwa watu wa dsm kama una gari Hybrid tumia AC as much as possible unapotumia hii gari hii itasaidia feni ya battery ku suck in cool air ambayo itakwenda kupoza battery..

Pia hii gari ni rahisi kufanya diagnosis kwa kutumia diagnostic machines kwakua zinakutajia specific problem na hata kama nu battery unaweza zoom in kwakila battery pack individual na ukajua ni pack gan ubadirishe na kufanya charging balancing ili battery zote ziwe even kwenye charging na discharging.

Zingatia tu kua kwenye mfumo wa uzungushaji maji ya kupozea injini kuna ambazo zinakuja na electric water pump na kuna zinazokuja na non electric water pump-ambayo inazungushwa na timing chain..so kwa zinazokuja na electric water pump when check engine light is on haraka saana weka gari pembeni chunguza chanzo cha hiyo check engine light..kwakua kwa hii gari yenye electric water pump the only way kujua kua ni water pump ndio imekufa is through check engine light illumination.

Kitu kingine cha kujua hii gari unapata a very good gas mileage kwenye trip za mjini kwakua muda mwing regenerative braking system inafanya kazi(zile stop and go zinafanya regenerative braking ina jaza chaji battery wakati wa kusimamisha gari but for high driving kwa speed 90+ gas mileage inashuka kidogo kwakua muda mwingi injini inawaka ku keep up with driving needs za dereva..so hapa both engine na MG2 motor zitakua zafanya kazi kwa pomoja ili kutoa nguvu dereva anahitaji kwa ajili ya hiyo speed ya juu, the reduced fuel efficiency at high way speed isnt that much because of absence of regenerative braking....

Unless otherwise hii gari ni gari nzuri sana mkuu.. na huto jutia kuinunua..
 
Maelezo yameshehen content safi!
 
Uko sahihi ila kwenye categories za hybrid kuna aina 2.
1.Convetional hybrids (Traditional)
2.Plug-in hybrids electric vehicles (PHEV)

Hapo kwenye conventional ndio penye hizi gari mithili ya Prius. Zinatumia Engine na Motors kutengeneza motion ya gari! Battery inachajiwa through generative braking tu!

Ukija kwenye PHEV hizi ni advanced ambazo battery inapokea charge kupitia regenerative braking pamoja na power outlets za majumbani! Hizi ni hybrid ambazo unaweza kuzichaji na zikatembea in isolation ya Engine kwa umbali flani then charge ikiisha engine ina kick in!

Kwa advancement zilizopo kwa sasa tunaenda kwenye aina ya 3 ya gari ambazo zinaitwa BEV ambayo ni kifupisho cha Battery Powered Electric Vehicle. Katika kundi hili ndipo wapo wakina Tesla ambao gari zao zina motor tu pekee bila engine. Wako wengine sana wameingia katika hili kundi ikiwamo kampuni za kichina ambazo zinachuana na tesla na almost kila kampuni kubwa wana gari ya BEV kwa mwaka huu! Toyota ana plan kutuletea hii gari mwaka 2022 akiwa ame patner na subaru! Inaitwa Toyota BZ (Beyond Zero) huku Lexus wakija na LF-1 (Limitless Electrified).
 
Nikweli Ukisoma kwa andiko langu nimeandika hybrid cars zipo za aina mbili... Wewe umeziita conventional Hybrid.... Mimi nkaita non plug-in hybrid car...

Ipo hivi Toyota wame opt hybrid kwakua ni gari ambazo ni self charging.. hata kama ni plug-in..

Tofauti hizo ambazo ni pure electric cars ambazo zinatumia battery tu... Disadvantages ya hii gari inayotumia battery peke yake ni kwamba unahitaji kipita kwenye charging points kuijachaji (fast charging infrastructures si nyingi dunianu hivo ukinunua gari kama tesla, nisssan leaf ukaja nayo bongo ina maana huwezi safari nayo toka dar kwenda mwanza kwakua betri itaisha charge na utahitaji kuichaji sasa shida itakuaja hapa yes unaweza ichaji kwenye socket ya nyumban but it will take days to have it full charged na ndo maana tesla ka install high voltage fast chargers kwa ajili ya gari zake, but with hybrid car (yaan ina umeme na injini ya kawaida) huta kutana na haya majanga ya kushiwa chaji ya betr then unabaki stranded njiani kwakua ilivokua designed hybrid car ni kwamba battery ikiwa imepungua charge below a certain level, engine kick-in to charge the battery after few seconds injini inazima na hata ukiwa na plug-in Hybrid car battery ikiisha injini itawaka ku charge huku unaendelea na safari (talking from experience)

Utofauti wa hybrid car na pure full electric car ni ukubwa wa battery.. Hybrid inakua na battery si kubwa sana kama pure electric car.. na ndo maana distance coverage in electric mode (EV mode) ya gari ambayo ni pure electric na ambayo ni hybrid ni tofauti... Mfano tesla anaweza kwenda umbali wa km 400 kwa umeme tu wakati Hybrid cars tena hizi latest ambazo ni plug-in ndo zaweza fika umbali wa 50km kwa umeme bila injini kuwaka (na hapa nu kama watembea speed ya kawaida)

So kifupi toyota wame opt Hybrid car kwakua hawa-limit kwenye kuuza magari yao .. tofauti na tesla ambapo ukinunua tesla unakuwa unawaza namna ya kuichaji ili utumie while with hybrid huna hizo stress.
 
But ndio maana nikasema tunaenda advancement ya pure electric kwa sasa soko limechangamka kaka!

Toyota analeta kitu pure electric mwakani hapo! Kitakuwa na solid state battery ambalo linaweza kuwa 80% charged ndani ya dakika 10! Very durable compared na hizi Li-ion batteries zilizopo sokoni! Wame patner na Panasonic kuhakikisha hilo linawezekana.

Mercedes ana EQS full electric!
Audi ana E-Tron full electric
BMW nae ana yake
VW pia anacho cha kwake

Inshort Tesla anakwenda kukumbana na ushindani wa hali ya juu. Future is electric kwa wenzetu huko! Nawaza kama ningekuwa Mo au mtu mwengine mwenye hela ningeanza kuwekeza Fast Charging points Around Town najua baada ya miaka 5 mbele watu wengi watakuwa wameanza kununua Plug-ins na ku abandon mafuta!
 
Usemacho ni kweli kabisa tec ya battery inaenda ina improve sana with time... Na kwa nature ya uchumi wetu kuhamia kwenye pure electrified cars may take decades kwakua vipato vyetu wengi ni wa kukunua gari za zamani, yaan mpaka circle ifike ya sisi kununua hizo gari technologia ilisha pitaga zaman, we imagine hata mifumo yetu ya tax assessment sijui kama hata tra tax calculator ipo configured kuweza hata kumsaidia mtu mwenye intention ya ku import electric car inaweza msaidia kupata hata indicative tax rate tu anayotarajia kulipa endapo ataagiza hilo gari (just out of curiosity)

So investment in fast charging infrastructures it has to be long term investment ambayo iko properly assessed na executed ili ije kukulipa in long run basing na mazingira yetu ya kibongo.. ila dah technology inakimbia sana na sie tupo nyuma.
 
Si tuko zama za mawe! Unajua Prius Hybrid tech has two decades mpaka sasa! Ilianzaga early 2000’s kwa wenzetu huko leo sisi 18- 20 years ahead ndio tumeweza afford!

Sema kwa mujibu wa Toyota wakifanikisha wanasema gari zao zinaenda kufanya mapinduzi hata bei ya EV’s itakuwa chini compared na ICE’s
 
Changamoto kubwa za convectional hybrid na PHEV cars ni zipi hasa?
 
Toyota Auris hybrif zinateleza mtaani kwetu kama panya wa kariakoo shimoni
 
Changamoto kubwa za convectional hybrid na PHEV cars ni zipi hasa?
Usipo jua namna ya kuitunza battery ya high voltage inaweza ika fail prematurely (mfano kuobadirisha air filter ya battery/uki interfere cooling mechanisms ya Hybrid battery.

Running car out of fuel hii ni shida kidogo..ukiishuwa mafuta na ukaendesha gari mpaka battery ikaisha kabisa kiasi kwamba computer itapo command injini iwake lakini kwakua hakuna mafuta injini ikashindwa kuwaka huwa inaleta shida...gari inaweza kukulete DTC (diagnostic trouble codes) ambazo itakulazimu kutumia scanner ili uzi clean ndo gari iwake

HID headlights zake uungua (kwa generation 2 na 3 sina uhakika na hizi generations nyingine...but uki install led bulb problem inakwisha,

Not every driving situations gari itakunali kwenda kwenye EV mode.

But all these ni issues ndogo ambazo kutokona na ubora wa gari si vitu vikubwa vya kukufanya usinunue hizi gari hasa toyota( note: kumbuka haya yote na ongelea Toyota Prius kwakua ndo nauzoefu nayo) yawezekana hizi issues zikawa chache zaidi kwa Toyota nyingine
 
Okay kwa uzoefu wako tutajie hybrid nzuri kwa hali ya mbongo ambazo ni rahisi kuishi nazo kwenye mazingira ya kwetu
 
Harrier hybrid inaenda kilometer ngapi
 
Ndugu....samahanisana, nina shida nawe, kuna jambo naomba ushauri, tafadhali naomba uniruhusu kupata namba yako kwa mawasiliano zaidi
Mkuu....nina shida nawe, nimekutext inbox
 
M

Hiyo Auris Hybrid ninayo haijawahi kusumbua nilienda nayo moshi kupitia bagamoyo nilitumia lita 25
Mkuu huwa unaicharge wapi ? Ningependa pia kuona picha zake zaidi ,na bei ni kiasi gani ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…