Ndugu yangu
Ngoja nikueleze kitu uhusu takwimu,
Kiufupi hali ni mbaya sana kwenye swala la watoto wanaozaliwa na maambukizi ya HIV kutoka kwa mama zao. Japo ina nafuu kidogo ukilinganisha na miaka ya 2000-2015.
Na hii ni kutokana na watu kuwa na elimu juu janga la ukimwi na serikali kuwa na mikakakati na kuwa zahanati katika kalibia kila kijiji hii imepelekea wazazi wengi kujifungulia katika vituo vya afya. Hali iliyopelekea kutokea kupungua kidogo kwa kasi ya watoto wanaozaliwa na maambukizi ya HIV.
Japo ki takwimu namba ni nyingi. Sio utani.
Vijijini hata na mijini hali ni mabaya sana.. kama utaamua kuwapima wanafunzi wa darasa la kwanza katika kila shule basi kwa vijijini utapata hata 10 au 20 kutegemea na wingi wa watoto katika kila darasa.
Ni wastani wa asilimia 13.5 katika kila darasa.
Hivyo basi bado elimu kubwa inahitajika kwa wazazi, jamii na hata watoaji huduma ya afya.
Hatuwezi kufanikiwa kupambana na watoto wanaozaliwa na HIV ikiwa bado tunaendelea kujificha ukiwa na maambukizi. Ifike hatua wenye maambukizi iwe ni wazi kujieleza tu kwenye jamii kuwa nina hiv na hata mwanangu pia.
Tukifika katika hatua hii tutakuwa tayari tumepiga hatua kubwa kwenye maambukizi mapya.
Maana siraha kubwa ya HIV ni kujificha na kujichukulia tatizo lako ni siri yako.