Ummy Mwalimu awatumbua Mkurugenzi wa Temeke (Mwakabibi) na Mkurugenzi wa Sumbawanga (Msemakweli)

Ummy Mwalimu awatumbua Mkurugenzi wa Temeke (Mwakabibi) na Mkurugenzi wa Sumbawanga (Msemakweli)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi Wakurugenzi wawili.

Wa kwanza ni Nyangi Msemakweli wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Huyu katumbuliwa kwa ubadhirifu wake na usimamizi mbovu wa miradi ya Maendeleo pia alikuwa hana maelewano na Madiwani.

Wa pili ni Lusubilo Mwakabibi, Mkurugenzi wa Manispaa ya temeke. Huyu yeye katumbuliwa kutokana na kuwa na mwenendo usiofaa na matumizi mabaya ya Madaraka.

Mwakabibi ametumbuliwa kutokana na watu kumlalamikia kwa mwenendo usiofaa na matumizi Mabaya ya Madaraka, Ubadhirifu, usimamizi mbovu wa miradi ya Maendeleo Katika Manispaa ya Temeke.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewataka Wakurugenzi wote Nchini kuzingatia Mipaka yao ya kazi.

Pia soma hizi:
1) Mkurugenzi wa Temeke, Mwakabibi awasweka ndani waandishi wa habari ili wasihudhurie kikao chake na wafanyabiashara

2) Wizara ya habari kuchunguza tukio la DED wa Temeke kuwaweka chini ya ulinzi waandishi kwa kufika kwenye kikao chake bila mwaliko

3) Wito: ITV isusie kutangaza taarifa zote za Manispaa ya Temeke mpaka pale DED Mwakabibi atakapotimuliwa

4) Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke aache kutisha na kufedhehesha Waandishi wa Habari

5) Mkurugenzi TEMEKE naye akamatwe na ahojiwe



Screenshot_20210425-102914.png

20210425_111400.jpg
 

Attachments

Waziri wa Tamisemi, Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi Wakurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na Manispaa ya Temeke

Mwakabibi ametumbuliwa kutokana na watu kumlalamikia kwa mwenendo usiofaa na matumizi Mabaya ya Madaraka.


View attachment 1763482
Daah maisha ni kutafuta na siyo kutafutana, huyo Mwakabibi alikuwa jeuri mno mpaka kajisahau kuwa yeye siyo mtumishi.
 
Na Yule aliejenga nyumba ya milioni 800 mbona bado yupo??

Na wa Tanga mjini?
 
Huyu DED machachali mwenye kelele nyingi za kujifisia hatimae amesimamishwa kazi kwa kushindwa majukumu na ufisadi .

Mwakibinga ambaye alikuwa shabiki mkubwa wa jpm kiasi yeye na mkewe wote kupewa u-DED alijaa tuhumu za ufisadi na ulevi was madaraka huku akionekana kupambana zaidi na DC Gondwe muda wote
IMG-20210425-WA0016.jpg
 
Huyu DED machachali mwenye kelele nyingi za kujifisia hatimae amesimamishwa kazi kwa kushindwa majukumu na ufisadi .

Mwakibinga ambaye alikuwa shabiki mkubwa wa jpm kiasi yeye na mkewe wote kupewa u-DED alijaa tuhumu za ufisadi na ulevi was madaraka huku akionekana kupambana zaidi na DC Gondwe muda wote
View attachment 1763510
Kichwa cha habari Mwakibinga……… barua Mwakabibi ni mtu mmoja huyo?
 
Back
Top Bottom