Ummy Mwalimu awatumbua Mkurugenzi wa Temeke (Mwakabibi) na Mkurugenzi wa Sumbawanga (Msemakweli)

Ummy Mwalimu awatumbua Mkurugenzi wa Temeke (Mwakabibi) na Mkurugenzi wa Sumbawanga (Msemakweli)

Aliemteua alipenda style yake .....ikampa jeuri zaidi ...asubiri uchunguzi
Hakika kiongozi maana jamaa alikuwa na kiburi. Nasikia watumishi wa halmashauri ya Temeke walikuwa wanamuogopa kuliko waziri mkuu.
 
Ni jambo jema

Huyu jamaa Jaffo alikuwa anamuogopa sana.

Nimeamini Wanawake wakiwezeshana wao kwa wao Wanaweza!
Wanacheza ngoma ya bosi wao tu, hata Jaffo angefanya hivyo kama bosi angependa, tatizo wakati wa Jaffo bosi alikuwa hapendi.
 
Mabega yalimpanda sana hadi yakapitiliza kiasi kwamba hata mwananchi aliye mbali naye aliweza kuyaona jinsi yalivyompanda!

Huenda swala la kuwa “Mtumishi wa Umma halijaeleweka vyema miongoni mwa wengi”
 
Huyu alikuwa Kakonko kabla ya kepelekwa Temeke. Yupo hovyo mno. Uchunguzi inafaa uanzie Kakonko.
Duh kumbe jamaa kitambo na mambo ya hovyo. Tena alivyoletwa ndani ya jiji akaona yupo peponi hakuna wa kumchezea.
 
Mwakibibi Mwakibumbu,nimekumbuka maneno ya Mwalimu wa Kyle.Kigoma aliyejinyonga kiss Mwakibibi kisha akaacha ujumbe kuwa huyu Mwakibibi ataua wengi.
 
Naona Ummy yuko vizuri sana. Kila mtu anakuwa na shida za hapa na pale ila nampongezani hatua nzuri sana
 
Huyo wa TEMEKE ndiye aliyekuwa anawajibu vibaya waandishi wa habari, mara awaweke ndani.. Huyo DED alikuwa na jeuri na kiburi.
Hii jeuri alikuwa nayo sababu ya jiwe. Alifanikisha kuiba uchaguzi wa ubunge kule Kibondo alipofariki Eng. Chiza akapata zawadi ya kuhamishiwa mjini na akaota mapembe. Visa vyote alivyofanya akiwa DED ni sababu ya backup ya uhakika aliyokuwa nayo toka kwa jiwe
 
Wanacheza ngoma ya bosi wao tu, hata Jaffo angefanya hivyo kama bosi angependa, tatizo wakati wa Jaffo bosi alikuwa hapendi.
Sema napenda Sana namna Mwakabibi anajiamini ...tatizo strength hii Kuna muda anaitumia vibaya
 
Wengine wakishahakikishiwa na waganga wao kuwa “hakuna wa kukung’oa” basi huzani ni kweli na kuanza kupandisha mabega! [emoji57][emoji57]

Madam Ummy kamatia hapohapo [emoji108]

Wanyooshe wanoko woote!
 
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi Wakurugenzi wawili.

Wa kwanza ni Nyangi Msemakweli wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Huyu katumbuliwa kwa ubadhirifu wake na usimamizi mbovu wa miradi ya Maendeleo pia alikuwa hana maelewano na Madiwani.

Wa pili ni Lusubilo Mwakabibi, Mkurugenzi wa Manispaa ya temeke. Huyu yeye katumbuliwa kutokana na kuwa na mwenendo usiofaa na matumizi mabaya ya Madaraka.

Mwakabibi ametumbuliwa kutokana na watu kumlalamikia kwa mwenendo usiofaa na matumizi Mabaya ya Madaraka, Ubadhirifu, usimamizi mbovu wa miradi ya Maendeleo Katika Manispaa ya Temeke.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewataka Wakurugenzi wote Nchini kuzingatia Mipaka yao ya kazi.

Soma hizi:
1) Mkurugenzi wa Temeke, Mwakabibi awasweka ndani waandishi wa habari ili wasihudhurie kikao chake na wafanyabiashara

2) Wizara ya habari kuchunguza tukio la DED wa Temeke kuwaweka chini ya ulinzi waandishi kwa kufika kwenye kikao chake bila mwaliko

3) Wito: ITV isusie kutangaza taarifa zote za Manispaa ya Temeke mpaka pale DED Mwakabibi atakapotimuliwa

4) Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke aache kutisha na kufedhehesha Waandishi wa Habari

View attachment 1763482
View attachment 1763546
Huyu wa Temeke ilikuwa suala la muda tu ,amekuwa akilalamikiwa sana....hata waandishi amekuwa akiwatukana
 
duh haya majina yanachanganya sana bila kuona hiyo picha siku zote nilikuwa nikisikia hilo jina najua ni mwanamama btn watu wasifanye kazi kwa mazoea
 
Back
Top Bottom