Ummy Mwalimu: Ruksa Madaktari kutumia hospitali za Serikali kama private clinic baada ya muda wa kazi

Ummy Mwalimu: Ruksa Madaktari kutumia hospitali za Serikali kama private clinic baada ya muda wa kazi

Hakuna siku mafuta na maji yaliwahi kuchanganyikana...[emoji2955]

Na sio siku nyingi serikali itakuja kujutia uamuzi wake huu...[emoji57]

Au kama vipi, Kila mtumishi atumie ofisi ya serikali kujiongezea kipato baada ya muda wa kazi uliopangwa kuisha...[emoji4]
Jambo hili nafikiri lingesubiri kwanza na lisifanyike kabisa katika ofisi na hospitali za umma. Kwa sababu Daktari ameajiliwa na kusaini mkataba wa kutumikia umma wa watanzania kwa muda wote atakaohitajika hospitalini kuhudumia wagonjwa.

Hatua hii na ruhusa hii ya Waziri ni hatari Sana kwa watanzania wanyonge wasio na uwezo wa kumuona daktari kwa muda huo wa ziada. Kwa kuwa hii inaweza kuwafanya madaktari na watumishi wa Afya kugeuza hospitali za umma Kama hospitali binafsi katika koti la hospitali ya umma, pia hatua hii itazolotesha utoaji wa huduma kwa watanzania wanyonge ili kuwalazimisha waje muda wa ziada ambapo gharama lazima ziwe za juu Sana

Watanzania wengi watapoteza maisha kwa kukosa huduma Bora na kukosa hela ya kumuona daktari muda huo ambao dactari atasema Ni wa ziada na anatakiwa alipwe hela kwa makubaliano binafsi,pia hatua hii itawafanya baadhi ya madaktari kupunguza ufanisi muda wa kazi ili wawavute wagonjwa wengi muda wa ziada wanaojuwa watajipatia pesa Yao binafsi.

Hospitali za umma zibaki kuwa hospitali za umma tu na siyo kufanya hivyo,Kama serikali inaona vipato vyao yaani mishahara na stahiki zingine haziwatoshi Basi iwaongezee mishahara zaidi,marupurupu, fedha za over time iwalipe kwa wakati,iboreshe mazingira ya hospitali kwa kuhakikisha vifaa Tiba,Dawa na wahudumu wa Afya wapo wa kutosha ili wasielemewa na mzigo wa kuhudumia wagonjwa.

Tunaweza kufanyia majaribio maeneo mengine lakini katu na kamwe hatupaswi kuleta mzaha Wala majaribio na Afya za watanzania wanyonge, hatupaswi kuweka maisha ya watanzania rehani,hatupaswi kuwatelekeza watanzania kwa kuweka hospitali ndani ya hospitali,mfumo ndani ya mfumo pasipo hata maandalizi ,hili nasema hapana Tena hapana.maisha yetu watanzania nayafahamu Sana na hata Mimi nikiona mzazi wangu anaumwa huwa Namuomba Mungu amponye maana hatuna uwezo wa kugharamia au kubeba gharama kubwa pale tutakapo hitajika kufanya hivyo.

Hospital za umma ziendelee kuboreshwa na kuwaboreshea maslahi watumishi wake ili kuongeza morali ya kazi lakini siyo kwa njia hiyo pendekezwa na mh Waziri ummy mwalimu, nasema jambo hili lisifanyike na pia viongozi wetu wa kisiasa yawapasa kuwa makini katika utoaji wa matamko kwa kuwa mengine yanaweza kuleta athari kubwa Sana hasa kwetu wa kipato Cha chini ambao hatuna uwezo wa kuwaona madaktari huo muda wa ziada.

Unafikiri Ni Daktari yupi ambaye hatapenda kuwekeza muda wa ziada kuhudumia wagonjwa? Unafikiri Daktari yupi ambaye hatawashawishi wagonjwa wake muda wa ziada? Unafikiri daktari atafanya kazi kwa juhudi muda wa kazi Kama ule wa ziada? Sasa Kama tunaruhusu hili kufanyika kulikuwa na kunakuwa na haja gani ya kupiga marufuku maduka ya watu binafsi kuwa karibu na hospitali za umma?

Mimi Nafikiri Kama serikali inalenga kuwaongezea vipato madaktari wetu ambao nami pia nawapenda ,Kuwaheshimu na kuthamini mchago wao Basi ingejikita katika kuwaongezea maslahi yao na kuboresha zaidi mazingira ya kazi.

Namshauri mh Waziri wangu kutengua kauli yake kabla haijaanza kufanyiwa kazi,.Nasema kuwa Afya za watanzania Ni muhimu Sana,sisi uwezo wetu wa kipato Ni mdogo Sana na ndio maana wengi Sana hatuna hata tu bima ya Afya Wala kuwa na uwezo wa kufanya vipimo binafsi vya Afya walau kila mwaka,chonde Sana serikali yangu nawaombeni Sana katika hili kutuonea huruma wanyonge nakutambua kuwa Afya ndio mtaji wetu.
Utaelewaaaaa tu

Ova
 
Mlipenda zama za ..... zinalejea kwa kasi-ile nidhamu aliyokuwa ameanza kuijenga Magufuli katika utoaji wa huduma ya afya sasa inakwenda kutoweka
The pharma Industry, wanatumia Kila njia kuhakikisha Kuna sustainable customers. Baadhi yetu ama kwa kujua ama kutojua tunafanya maamuzi ya kutimiza hii ajenda ya hii industry!!!

Jambo hili linatekelezeka kirahisi kwa sababu pesa inakuwa mbele zaidi ya utu!
 
Ambacho hamjaelewa wengi kama si wote ni kwamba hospital ya serikali ni saa 24 huduma, kwahiyo huduma zitendelea kama kawaida,

Aliyeruhusiwa ni daktari, yaani badala ya kuhangaika kwenda private basi aendelee tu hapo hapo, kwahiyo pataekwa mfumo na utaratibu mzuri kwa ajili lengo ni kuhudumia wananchi

Hivi daktari huyo huyo akitoka hapo si anakwenda private za wahindi huko? Si pia anaweza kukushauri umfate huko? Ndio maana ya hili
Acheni mihemko
 
🙄
 
Huyu yupo Sawa kichwani kweli? Yaani kazi binafsi zifanyikie kwenye hospitali ya umma. Hii imekaaje. Hizo dawa na vifaa tiba nani anawajibika?
Amekosea mno, ni heri wafanye hizo kazi nje ya hospitals za umma. Hapa anaua huduma za kiafya kwa hospitals za umma
Zina mtosha mwenyewe, halafu anaenda kabidhiwa uhai wa watu.
 
Ambacho hamjaelewa wengi kama si wote ni kwamba hospital ya serikali ni saa 24 huduma, kwahiyo huduma zitendelea kama kawaida,

Aliyeruhusiwa ni daktari, yaani badala ya kuhangaika kwenda private basi aendelee tu hapo hapo, kwahiyo pataekwa mfumo na utaratibu mzuri kwa ajili lengo ni kuhudumia wananchi

Hivi daktari huyo huyo akitoka hapo si anakwenda private za wahindi huko? Si pia anaweza kukushauri umfate huko? Ndio maana ya hili
Acheni mihemko
Tafakari unachoandika.
 
Vifaa atatumia vya kwake au hospital 🤔🤔 kama ni vya hospital daktari anaechukua zamu atatumia vya kutokea wapi🤔🤔 vipi kuhusu na vitanda vitatosha kweli 🤔🤔, alipaswa kuchukua tahadhali kubwa kutokana na waswahili kua ni watu wa Dili Sana wanaweza Waka chelewesha huduma ili wapige pesa baada ya muda wa kazi kuisha
 
Back
Top Bottom