Ummy Mwalimu: Ruksa Madaktari kutumia hospitali za Serikali kama private clinic baada ya muda wa kazi

Yaani watumie rasilimali za umma kwa matumizi yao binafsi duh
Amekwambia watalipia kama wanavyofanya sasa hili wala sio kitu kipya. sio kila jambo kipinga tu haya mambo yanafanyika toka zamani. Namuona Dr baada ya kazi clinic yake anakupata appointment labda kufanya upasuaji anakuelekeza Hosp ya kwenda kwa maana private Hosp anakuja huyo Dr anafanya service zake wewe unamlipa kama yeye na unalipa gharama za Hosp. wakati mwingine inakuwa lump sum yeye Dr anakuwa na maelewano na hiyo Hosp kuhusu charges. Hakuna jipya katika hili.
 
Safi sana, ikiwezekana tutafute hata madaktari kutoka Dubei waje kuendesha suala zima la matibabu nchini😄
Acheni gubu nyinyi, mbona wakija ma Dr bingwa kutoka nchi za nje kama India tunawapokea kwa mikono miwlili hatusemei hatutaki wageni. Kila jambo nongwa tu hata kama unaichukia serikali sio kila jambo mengine hata kama hutaki kusifia nyamaza tu.
 
Au kama vipi, Kila mtumishi atumie ofisi ya serikali kujiongezea kipato baada ya muda wa kazi uliopangwa kuisha...😊
Ndio huku tunako elekea na tumefika, Mashuleni nako, waalimu nao! wana lao jambo
 
Hapo mama yangu "umechemka"; tena umechemsha haswaa! Hospitali za Serikali zinakwenda kuharibika sasa. Kwa hiyo watumie vifaa na madawa ya Serikali kujinufaisha, Siyo?
Kumbukeni, madaktari wetu wamesomeshwa, wameajiriwa na wanalipwa na wananchi. Ni wajibu wao kuwatumikia wananchi usiku na mchana. Magonjwa hayana muda maalum. Tuige mfumo uendeshaji wa Sekta ya afya Botswana. Madaktari wa Nchi hii wanaogopwa na kusujudiwa kupita kiasi kwamba baadhi yao ni kama miungu watu wanafanyakazi wanavyotaka. Hapana.
 
Kwanza huyo Dokta kwenye hizo ‘after hours’ services, patients info anahifadhi wapi for medical history purposes; ni sawa na kufungua hospitali bubu na kuhatarisha maisha ya watu.

Only Ummy Mwalimu anaweza kuja na ubunifu kama huo.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hata walimu wanafundisha tuition tu shuleni. Sio kila kitu kipinga haya mambo hata hivi sasa yapo unaenda Hospital unataka fast track unalipia unataka kusubiri yapo tu, tusifanye mambo magumu na kuingiza ushabiki wa kisiasa kwa kila jambo.
Bora iwe sio halali, watu wafanye kwa kuibia, kuliko kuwapa uhuru sasa unawajua wabongoo vizuri lakini??
 
Bora iwe sio halali, watu wafanye kwa kuibia, kuliko kuwapa uhuru sasa unawajua wabongoo vizuri lakini??
Walikuwa hawafanyi kwa kuibia haya mambo yalikuwa wazi na kihalali kabisa. Ilikuwa unaenda kumuona Dr Hosp na anakuhudumia sio kwamba anafanya uzembe unapata huduma kama zote ila inajulikana baada ya kazi huyo huyo Dr ana clinic yake nje na anahudumia. Mimi binafsi sijawahi kuhudumiwa tofauti japo ukiwa Hosp ya serikali process zake ni tofauti. Lakini hata hizi Hosp za serikali ziko huduma za fast track ukitaka kuonana na Dr bingwa express bila foleni unalipa tu hutaki unapiga foleni haya mambo yapo kila siku.

Waziri nia yake ni nzuri kwamba hawa ma Dr nje ya kazi badala ya mfano kwenda kulipia xray nje wanaweza kutumia za Hosp na wakalipia mimi sidhani kama ni issue kubwa sababu tayari haya mambo yapo Hosp zote kubwa za serikali.
 
Basi tulichelewa sana wakanyage twende
 
Ukisoma comments nyingi humu watanzania wengi wana chuki na madaktari, they don't give a f*ck about doctors wellfare!!!
 
Tz ni nchi yenye viongozi wa hovyo kuwahi kutokea duniani
 
Huu uwamuzii bado hautotatua tatizo utaongeza tatizo wajomba watafanya sehemu ya biashara zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…