Ummy Mwalimu: Ruksa Madaktari kutumia hospitali za Serikali kama private clinic baada ya muda wa kazi

Ummy Mwalimu: Ruksa Madaktari kutumia hospitali za Serikali kama private clinic baada ya muda wa kazi

Ambacho hamjaelewa wengi kama si wote ni kwamba hospital ya serikali ni saa 24 huduma, kwahiyo huduma zitendelea kama kawaida,

Aliyeruhusiwa ni daktari, yaani badala ya kuhangaika kwenda private basi aendelee tu hapo hapo, kwahiyo pataekwa mfumo na utaratibu mzuri kwa ajili lengo ni kuhudumia wananchi

Hivi daktari huyo huyo akitoka hapo si anakwenda private za wahindi huko? Si pia anaweza kukushauri umfate huko? Ndio maana ya hili
Acheni mihemko
Huo mfumo utafanya kazi vipi?

Vipimo maabara vya wagonjwa binafsi vitapewa kipaumbele ili wapewe majibu ya haraka?

Nani atalipia muda na matumizi ya vifaa vya maabara na gharama za kutunza sample.

Wakilazwa nani ata gharamia manesi watakao kuwa wakiwauguza hao wagonjwa wake, huyo dokta akitoka shift nani afanye maamuzi ya wagonjwa wake watakao lazwa.

Ata changia gharama za kutunza store za dawa.

Kwa kifupi ni wazo la kijinga mno.
 
ChoiceVariable Kumbe muda mwingine huwa unauwezo wa kujiongeza.

Leo ninakupongeza kwa mara ya kwanza.
We nyumbu ukiona naunga mkono jambo ujue Lina maslahi mapana Kwa Nchi kinyume chake Huwa napinga,mimi sio chawa Wala sio mwana ccm au Chadema na sitaki hayo mavyama yenu.
 
Huo mfumo utafanya kazi vipi?

Vipimo maabara vya wagonjwa binafsi vitapewa kipaumbele ili wapewe majibu ya haraka?

Nani atalipia muda na matumizi ya vifaa vya maabara na gharama za kutunza sample.

Wakilazwa nani ata gharamia manesi watakao kuwa wakiwauguza hao wagonjwa wake, huyo dokta akitoka shift nani afanye maamuzi ya wagonjwa wake watakao lazwa.

Ata changia gharama za kutunza store za dawa.

Kwa kifupi ni wazo la kijinga mno.
Nilivyoelewa mimi ni kliniki tu itafanyika hapo na huyo daktari, sasa sdhani kama kliniki ina mlolongo wote hui,

Ninavyojua kliniki ni kumuona daktari akupe ushauri then unaendelea either private hospital au government hospital kwa utaratibu uliowekwa
 
We nyumbu ukiona naunga mkono jambo ujue Lina maslahi mapana Kwa Nchi kinyume chake Huwa napinga,mimi sio chawa Wala sio mwana ccm au Chadema na sitaki hayo mavyama yenu.
 

Attachments

  • 9A6B14AB-18B6-4A3B-9FF0-EC486AF692D8.gif
    9A6B14AB-18B6-4A3B-9FF0-EC486AF692D8.gif
    69.7 KB · Views: 2
Very unpopular decision. Hapo ujue limekaa jopo la wataalam kufanya hayo maamuzi.

Terrible!
 
Nadhani kwa Nairobi - Kenya jambo hili limeshafanyika na linaendelea
 
Ni mwendo wa kubinafsisha kila kitu, waziri wa Elimu nae atoe maagizo haya kwa walimu.
Hata walimu wanafundisha tuition tu shuleni. Sio kila kitu kipinga haya mambo hata hivi sasa yapo unaenda Hospital unataka fast track unalipia unataka kusubiri yapo tu, tusifanye mambo magumu na kuingiza ushabiki wa kisiasa kwa kila jambo.
 
this has been happening since ever , hospital kabla ya clinic kuna private clinic na baada ya clinic kuna private clinic. sema waziri kaiweka wazi.na ruksa. aina shida sema aina foleni. ni direct kumuona doctor hasa doctor bingwa ni fast service sema unalipia more. ukitaka kawaida unaendelea na taratibu wa kawaida ambao upo. na pia doctor bingwa yupo mda wa clinic unamuona kama kawaida kwa bei Chee. no conflict of interest, hospital makes more money and the doctor too. win win
 
Nilivyoelewa mimi ni kliniki tu itafanyika hapo na huyo daktari, sasa sdhani kama kliniki ina mlolongo wote hui,

Ninavyojua kliniki ni kumuona daktari akupe ushauri then unaendelea either private hospital au government hospital kwa utaratibu uliowekwa
Kwa ivyo wagonjwa wake wakienda hapo wanaoihitaji further diagnosis atawapeleka wapi?

What’s the point kama ni consultation si wamfuate kwake, otherwise huduma ya afya inaenda sambamba na medical treatment. Ambazo huyo daktari awezi toa bila ya kutumia huduma zingine za serikali.

Au unataka kusema na yeye akishindwa atakuwa anaandika referrals za kurudi masaa ya kazi atakapokuwa na access ya huduma zote za hospitali. Si ndio tunarudi pale pale kuhudumia wagonjwa binafsi muda wa kazi.

Ni wazo la ovyoo mno, only Ummy Mwalimu can come up with something like that.

Hospitals should strive for standardisation of their services and upholding medics to perform at the best of their abilities always. Wewe unasema kuna watu awataki kusubiri ina maana una suggest hospitali zianze ku discriminate kwenye kutoa huduma kwa jinsi Dokta anavyolipwa na watu binafsi.

Huyo dada kama lazima awe msimuweke sehemu serious kama hizo.
 
Jambo hili nafikiri lingesubiri kwanza na lisifanyike kabisa katika ofisi na hospitali za umma. Kwa sababu Daktari ameajiliwa na kusaini mkataba wa kutumikia umma wa watanzania kwa muda wote atakaohitajika hospitalini kuhudumia wagonjwa.

Hatua hii na ruhusa hii ya Waziri ni hatari Sana kwa watanzania wanyonge wasio na uwezo wa kumuona daktari kwa muda huo wa ziada. Kwa kuwa hii inaweza kuwafanya madaktari na watumishi wa Afya kugeuza hospitali za umma Kama hospitali binafsi katika koti la hospitali ya umma, pia hatua hii itazolotesha utoaji wa huduma kwa watanzania wanyonge ili kuwalazimisha waje muda wa ziada ambapo gharama lazima ziwe za juu Sana

Watanzania wengi watapoteza maisha kwa kukosa huduma Bora na kukosa hela ya kumuona daktari muda huo ambao dactari atasema Ni wa ziada na anatakiwa alipwe hela kwa makubaliano binafsi,pia hatua hii itawafanya baadhi ya madaktari kupunguza ufanisi muda wa kazi ili wawavute wagonjwa wengi muda wa ziada wanaojuwa watajipatia pesa Yao binafsi.

Hospitali za umma zibaki kuwa hospitali za umma tu na siyo kufanya hivyo,Kama serikali inaona vipato vyao yaani mishahara na stahiki zingine haziwatoshi Basi iwaongezee mishahara zaidi,marupurupu, fedha za over time iwalipe kwa wakati,iboreshe mazingira ya hospitali kwa kuhakikisha vifaa Tiba,Dawa na wahudumu wa Afya wapo wa kutosha ili wasielemewa na mzigo wa kuhudumia wagonjwa.

Tunaweza kufanyia majaribio maeneo mengine lakini katu na kamwe hatupaswi kuleta mzaha Wala majaribio na Afya za watanzania wanyonge, hatupaswi kuweka maisha ya watanzania rehani,hatupaswi kuwatelekeza watanzania kwa kuweka hospitali ndani ya hospitali,mfumo ndani ya mfumo pasipo hata maandalizi ,hili nasema hapana Tena hapana.maisha yetu watanzania nayafahamu Sana na hata Mimi nikiona mzazi wangu anaumwa huwa Namuomba Mungu amponye maana hatuna uwezo wa kugharamia au kubeba gharama kubwa pale tutakapo hitajika kufanya hivyo.

Hospital za umma ziendelee kuboreshwa na kuwaboreshea maslahi watumishi wake ili kuongeza morali ya kazi lakini siyo kwa njia hiyo pendekezwa na mh Waziri ummy mwalimu, nasema jambo hili lisifanyike na pia viongozi wetu wa kisiasa yawapasa kuwa makini katika utoaji wa matamko kwa kuwa mengine yanaweza kuleta athari kubwa Sana hasa kwetu wa kipato Cha chini ambao hatuna uwezo wa kuwaona madaktari huo muda wa ziada.

Unafikiri Ni Daktari yupi ambaye hatapenda kuwekeza muda wa ziada kuhudumia wagonjwa? Unafikiri Daktari yupi ambaye hatawashawishi wagonjwa wake muda wa ziada? Unafikiri daktari atafanya kazi kwa juhudi muda wa kazi Kama ule wa ziada? Sasa Kama tunaruhusu hili kufanyika kulikuwa na kunakuwa na haja gani ya kupiga marufuku maduka ya watu binafsi kuwa karibu na hospitali za umma?

Mimi Nafikiri Kama serikali inalenga kuwaongezea vipato madaktari wetu ambao nami pia nawapenda ,Kuwaheshimu na kuthamini mchago wao Basi ingejikita katika kuwaongezea maslahi yao na kuboresha zaidi mazingira ya kazi.

Namshauri mh Waziri wangu kutengua kauli yake kabla haijaanza kufanyiwa kazi,.Nasema kuwa Afya za watanzania Ni muhimu Sana,sisi uwezo wetu wa kipato Ni mdogo Sana na ndio maana wengi Sana hatuna hata tu bima ya Afya Wala kuwa na uwezo wa kufanya vipimo binafsi vya Afya walau kila mwaka,chonde Sana serikali yangu nawaombeni Sana katika hili kutuonea huruma wanyonge nakutambua kuwa Afya ndio mtaji wetu.
Nadhani kama haya hujayaelewa, ma Dr wote wana clinic zao baada ya kazi wote na tuwajuwa sehemu za kuwapata baada ya kazi. Na nasema ma Dr wote kilafanyika sana ni kuongeza kipato Hosp ku charge gharama za private clinic. Hawa ma Dr hapa Dar unaenda kumuona akitoka Muhiumbili na anafanya operation hosp sio ya kwake ila wewe unalipia Hosp na yeye unamlipa kipato kinaenda clinic za nje sasa badala kwenda nje wape access Hosp itenegeze pesa pia.
 
Ushauri wangu, Katibu wa Wizara au Chief Medical Officer mmoja wao ajitokeza kuliweka sawa hili jambo. Sioni nia mbaya ya waziri au serikali, bali naona kuna utoaji wa message tofauti na iliyokusudiwa.
Wafanye mapema
 
Labda hujanielewa, au pengine mimi si mwandishi mzuri
Umeeleweka,yaani unasapoti daktari atumie chumba cha kutolea huduma kilekile hapo hospitalini kumpa huduma mgomjwa anayehitaji huduma binafsi kutoka kwa daktari husika,pia vifaa tiba hivyohivyo vitumike pia,kibinafsi n.k. Aisee...
 
Kadhalika Magari yana breki, yana mikanda, yana airbag.
 
Wala usishangae sie ndio tunaanzisha wengine wataiga
Hakuna atakae kuiga hospitali makini zipo busy kupambana na kuimarisha huduma zao siku zote, kujifunza makosa (hasa medical errors) na kutafuta namna ya kupunguza kwa kuweka process imara za kazi.

Huo muda wa kuruhusu hayo mambo ya kipuuzi hayapo, kwanza nani anakaguwa quality ya hizo services; you do know nchi nyingi zina health services watchdog ujitolei tu huduma.
 
Umeeleweka,yaani unasapoti daktari atumie chumba cha kutolea huduma kilekile hapo hospitalini kumpa huduma mgomjwa anayehitaji huduma binafsi kutoka kwa daktari husika,pia vifaa tiba hivyohivyo vitumike pia,kibinafsi n.k. Aisee...
Hapana ni daktari tu anatumika na fees yake atalipwa na huyo mgonjwa,hivyo vifaa na madawa menngine yote yakitumika vitalipiwa kwa serikali baada ya mfumo kuwekwa,
Vyumba vya ziada vitatumika kwa kuwa hospital ya serikali inafanya kazi saa 24
 
Kwanini hizo hospitali za serikali zisianzishe private klini badala ya hilo wazo la Mh Aaziri
 
Back
Top Bottom