Ummy Mwalimu: Wachangiaji damu, kupewa kipaumbele wanapohitaji damu hospitalini. Watapewa kadi Maalum

Serikali kupitia wizara ya Afya imejipanga kutoa kadi za kieletroniki kwa wachangiaji damu wanaojitolea mara kwa mara angalau mara tatu kwa mwaka.

Hayo yamesemwa leo Februari 25, 2022 na Waziri wa afya Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa katika ziara ya kutembelea makao kuu ya mpango wa taifa wa damu salama jijini Dar es Salaam
.
Waziri Ummy amesema Kadi za kieletroniki zitaepusha usumbufu kwa wachangia damu endapo watahitaji huduma ya damu kwani kadi hizo zitaonesha jina la mchangiaji damu, kundi la damu yake na namba ya kadi, na mchangiaji huyu atapewa kipaumbele akiwa na mgonjwa hata yeye mwenyewe.

"Kila Mtanzania ana haki ya kupata damu lakini kwa wale ambao watakaokuwa na kadi watapewa kipaumbele cha kwanza". Amesema Waziri Ummy.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeamua kutoa bure mifuko ya kukusanyia damu salama pamoja na vifaa vya ukusanyaji kwa Halmashauri zote nchini 184 ili kwenda kumaliza changamoto ya ukusanyaji ambayo imejitokeza nchini hivi sasa na kusababisha uhaba wa damu katika vituo vya kutolea huduma za afya.

"Nitoe wito kwa waganga wakuu wa mikoa yote nchini kuhakikisha wanapokea vifaa hivyo vya kuchangia damu na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kutatua changamoto ya upatikanaji damu kwa kuwa damu inahitajika sana na mama wajawazito, watoto, watu waliopata ajali pamoja na wanaofanyiwa upasuaji". Amesema Waziri Ummy.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume amesema vifo vingi vya kina mama wajawazito hutokana na ukosefu wa damu salama na hivyo kuitaka jamii iweze kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha kwa wenye uhitaji huku akieleza kuhamasisha vikundi mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya uchangiaji.

Nae, Meneja mpango wa Taifa damu salama Dkt. Magdalena Lyimo ameishukuru Serikali kwa hatua inayochukua juu ya upatikanaji damu salama kwa urahisi.

"Sasa kazi ni kwetu kuhakikisha damu salama inapatikana kwa kuungana na wananchi juu ya uchangiaji damu na naamini tukishirikiana tutaokoa vifo vingi". Amesema Dkt. Lyimo.
 
Nimemkejeli Hana lolote huyo wa hovyo kuliko, anyways no comparison

Kuna namna kweli unajua mambo mengi, ila Sasa wewe ndugu yangu, ni kama una malengo fulani ya nakuwa kama yanakupofusha hivi!
Besides everything, mimi pia ni kada wa CCM, hivyo ukiwa kada, lazima kuna baadhi ya maeneo lazima nita side na chama changu, mfano kwenye uchaguzi mkuu, uliopita, licha ya uwepo wa dosari ndogo ndogo, lakini uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, ulioendeshwa na Tume huru ya uchaguzi, hivyo CCM imeshinda kwa haki, wapinzani wamekataliwa!.
P
 
Thread[emoji116][emoji116][emoji116]

Serikali kupitia wizara ya Afya imejipanga kutoa kadi za kieletroniki kwa wachangiaji damu wanaojitolea mara kwa mara angalau mara tatu kwa mwaka.

Hayo yamesemwa leo Februari 25, 2022 na Waziri wa afya Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa katika ziara ya kutembelea makao kuu ya mpango wa taifa wa damu salama jijini Dar es Salaam
.

Waziri Ummy amesema Kadi za kieletroniki zitaepusha usumbufu kwa wachangia damu endapo watahitaji huduma ya damu kwani kadi hizo zitaonesha jina la mchangiaji damu, kundi la damu yake na namba ya kadi, na mchangiaji huyu atapewa kipaumbele akiwa na mgonjwa hata yeye mwenyewe.

"Kila Mtanzania ana haki ya kupata damu lakini kwa wale ambao watakaokuwa na kadi watapewa kipaumbele cha kwanza". Amesema Waziri Ummy.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeamua kutoa bure mifuko ya kukusanyia damu salama pamoja na vifaa vya ukusanyaji kwa Halmashauri zote nchini 184 ili kwenda kumaliza changamoto ya ukusanyaji ambayo imejitokeza nchini hivi sasa na kusababisha uhaba wa damu katika vituo vya kutolea huduma za afya.

"Nitoe wito kwa waganga wakuu wa mikoa yote nchini kuhakikisha wanapokea vifaa hivyo vya kuchangia damu na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kutatua changamoto ya upatikanaji damu kwa kuwa damu inahitajika sana na mama wajawazito, watoto, watu waliopata ajali pamoja na wanaofanyiwa upasuaji". Amesema Waziri Ummy.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume amesema vifo vingi vya kina mama wajawazito hutokana na ukosefu wa damu salama na hivyo kuitaka jamii iweze kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha kwa wenye uhitaji huku akieleza kuhamasisha vikundi mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya uchangiaji.

Nae, Meneja mpango wa Taifa damu salama Dkt. Magdalena Lyimo ameishukuru Serikali kwa hatua inayochukua juu ya upatikanaji damu salama kwa urahisi.

"Sasa kazi ni kwetu kuhakikisha damu salama inapatikana kwa kuungana na wananchi juu ya uchangiaji damu na naamini tukishirikiana tutaokoa vifo vingi". Amesema Dkt. Lyimo.
 
na kuna watu wanaunga mkono hii mambo. urasimu unapozidi, huzaa rushwa. baada ya hapo sasa wasio na hivyo vitambulisho, bila rushwa, hakuna damu!
ati watu wajitokeze kwa wingi kuchangia damu! kasahau kbs kuwa kuna watu, hususan wazee na wenye magonjwa kadhaa hawachangii damu kwa sababu mblmbl - hivyo wakiugua waachwe wafe kwa kuwa Ummy kasema!? au watoe rushwa!
kasahau kbs kuna maeneo mengi hususan vijjn hakuna hizo huduma!? lkn tunatoa wp viongozi wa aina hii?
katoka Dom anazingirwa na wanahabari akizunguka huku na huko akitumbua! hakuna mfumo sahihi wa kuwajibishana mtumishi anapokosea? kazi za mawaziri ndo hizo tu? hana nyingine?
kwa sasa mfumo wetu wa uongozi ndo umefika hapo. mnachagua watumishi kw vigezo mnavovijua wenyewe wanaofanya kw staili zenu wenyewe hadi panapotokea mabadiliko ya kisiasa ndiposa mnagundua madudu na kuanza kutumbuana, halafu kuna watu wanaimba mapambio ya kupongeza!
ni lini Tz tutakapobadili mfumo huu wa kutatua matatizo ya ki-menejiment kw solution za kisiasa za "Utumbuzi". ni kwamba ktk mfumo wetu wa ajira hatuna wataalamu wa hiyo fani au wote ni siasa tu!! ...dah!
acheni kuingiza siasa kila mahali. mambo ya kitaalam waachieni wenyewe, hayawahusu wanasiasa
 
Mnajua wazi damu haiuzwi. Halafu kuna binadamu mmoja anajitolea mara tatu kwa mwaka kuchangia damu kwa hiyari na utashi wake. Kwa nini asipatiwe kipaumbele? To hell with ethics.

Mnajua yale masindano yanavyouma? Sasa kwa hiyari yake mtu huyu anatobewa mara tatu/nne kwa mwaka akichangia damu kwa watu asiowajua.

Nyie wengine wakati huyu anajiamsha kwenda kituo cha damu salama huwa mnakuwa wapi? Mnaogopa yale masindano, au mnaogopa kuambiwa damu yako si salama?
Mkitaka pasiwepo na upendeleo nanyi mkachangie.
 
Hii wizara kila akipewa mtu wa fani ya Afya, akina Kigwangala na Gwajima dada jahazi linaenda mrama.... wakipewa ngwini kama Anna Abdallah wanaweza! Kuna tatizo kwa hawa madaktari...
Simple answer hawa watu wa fani wengi ni viburi vya ujuaji niliwai kumskia gwajima akisema anaijua hiyo sekta ya afya nje ndani miaka mingapi sijui mtu kama huyu atashaurika,
But watu dizain ya ummy,anna huwa wanakubali hawana iyo taaluma na always wanafuata ushauri wa wataalam wabobevu wa kada husika thus why mambo yanaenda..
 
Unaonaje kama waganga wakuu wa Wilaya, Mkoa, nk wawe ni watu aliosomea utawala/ uongozi na sio MD's?
 
Simple answer hawa watu wa fani wengi ni viburi vya ujuaji niliwai kumskia gwajima akisema anaijua hiyo sekta ya afya nje ndani miaka mingapi sijui mtu kama huyu atashaurika,
But watu dizain ya ummy,anna huwa wanakubali hawana iyo taaluma na always wanafuata ushauri wa wataalam wabobevu wa kada husika thus why mambo yanaenda..
Ushauri mzuri kwako ni waziri kuja hadharani na kutuambia kutakuwa na ubaguzi wa kupewa huduma kama uchangii damu.

Kila disciplines ina kanuni zake za kufanya kazi inabidi azijue kwanza kabla ya kuleta ubinifu unaokwenda tofauti na ethics za taaluma.

Jukumu la ku mobilise mikakati ya kukusanya damu ni lao, wakishindwa mbinu za kufanya kazi zao wanakuja na solution za ovyo kama hizi.

Muhimbili inatoa huduma za kimataifa akija mgeni kutibiwa anakuja na damu yake?

Watu wanaropoka mambo ya ovyo mnatetea. Hiyo ndio sababu wanampenda huyo hayo dada hapo afya ni kama gari bovu wanalisukuma wanavyotaka.
 
Mnajua wazi damu haiuzwi. Halafu kuna binadamu mmoja anajitolea mara tatu kwa mwaka kuchangia damu kwa hiyari na utashi wake. Kwa nini asipatiwe kipaumbele? To hell with ethics.

Mnajua yale masindano yanavyouma? Sasa kwa hiyari yake mtu huyu anatobewa mara tatu/nne kwa mwaka akichangia damu kwa watu asiowajua.

Nyie wengine wakati huyu anajiamsha kwenda kituo cha salama huwa mnakuwa wapi? Mnaogopa yale masindano, au mnaogopa kuambiwa damu yako si salama?
Mkitaka pasiwepo na upendeleo nanyi mkachangie.
Umeshawahi kuona public health campaign ya kuhamasisha watu kuchangia damu recently. Au unadhani wananchi watajuaje inventory iliyopo kwenye blood bank.

Wahusika ndio wenye kuja inventory waliyonayo, wao ndio wanapanga muda wa kuongeza damu based on reserve limit and so forth.

Kutoka kulaumu watu wasiojua ata kama wanatakiwa kuchangia damu ni ufinyu wa fikra.
 
Hivi huyu mtu anafahamu hata Medical Ethics?

Waziri wa afya jifunze ‘medical ethics’ under the concept of ‘non malificence’ you can’t do harm to a patience.

Hakuna priority kwenye afya who deserve the resources than another. It’s either first come first served or who needs it the most based on their poor medical condition.

Lakini hakuna sera ya kuchangia, upendelewe. Ni jukumu la wizara ya afya kukusanya damu na watu wana mbinu za kufanya hiyo shughuli.

Wanakupenda huko kwa sababu siyo mtaalamu unaeongea ujinga mtupu na aliekupa hayo mapendekezo ni mjinga vile vile.

=====

Na. WAF - Dar Es Salaam
View attachment 2131495
Serikali kupitia wizara ya Afya imejipanga kutoa kadi za kieletroniki kwa wachangiaji damu wanaojitolea mara kwa mara angalau mara tatu kwa mwaka.

Hayo yamesemwa leo Februari 25, 2022 na Waziri wa afya Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa katika ziara ya kutembelea makao kuu ya mpango wa taifa wa damu salama jijini Dar es Salaam.

Waziri Ummy amesema Kadi za kieletroniki zitaepusha usumbufu kwa wachangia damu endapo watahitaji huduma ya damu kwani kadi hizo zitaonesha jina la mchangiaji damu, kundi la damu yake na namba ya kadi, na mchangiaji huyu atapewa kipaumbele akiwa na mgonjwa hata yeye mwenyewe.

"Kila Mtanzania ana haki ya kupata damu lakini kwa wale ambao watakaokuwa na kadi watapewa kipaumbele cha kwanza". Amesema Waziri Ummy.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeamua kutoa bure mifuko ya kukusanyia damu salama pamoja na vifaa vya ukusanyaji kwa Halmashauri zote nchini 184 ili kwenda kumaliza changamoto ya ukusanyaji ambayo imejitokeza nchini hivi sasa na kusababisha uhaba wa damu katika vituo vya kutolea huduma za afya.

"Nitoe wito kwa waganga wakuu wa mikoa yote nchini kuhakikisha wanapokea vifaa hivyo vya kuchangia damu na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kutatua changamoto ya upatikanaji damu kwa kuwa damu inahitajika sana na mama wajawazito, watoto, watu waliopata ajali pamoja na wanaofanyiwa upasuaji". Amesema Waziri Ummy.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume amesema vifo vingi vya kina mama wajawazito hutokana na ukosefu wa damu salama na hivyo kuitaka jamii iweze kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha kwa wenye uhitaji huku akieleza kuhamasisha vikundi mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya uchangiaji.

Nae, Meneja mpango wa Taifa damu salama Dkt. Magdalena Lyimo ameishukuru Serikali kwa hatua inayochukua juu ya upatikanaji damu salama kwa urahisi.

"Sasa kazi ni kwetu kuhakikisha damu salama inapatikana kwa kuungana na wananchi juu ya uchangiaji damu na naamini tukishirikiana tutaokoa vifo vingi". Amesema Dkt. Lyimo.

Wanaojifungua watakufa kutokana na sera ya waziri mpuuzi.
 
n watakufa kutokana na sera ya waziri mpuuzi.
Ndio maana wanampenda afya, kwa sababu hajui lolote upande wa management za afya wala taaluma za kazi.

Wakipelekewa mtaalamu wizara ya afya wanakuwa wakali na majungu; hii nchi watu wanamazoea awataki kubadilika ukiwapa mtu kama Ummy shangwe.

Imagine ‘Accident and Emergency’ watu wamepata ajali huko, mtu kapigwa risasi au kachomwa kisu na majambazi. Madaktari baada ya kufikiria kuokoa maisha waanze kuchunguza kama mgonjwa alikuwa mchangiaji damu si unakufa.
 
Sijaona kosa la waziri. Toka uchangie damu hili na wewe ukiitaji damu salama uipate kirahisi.
Na pia alichosema ndio kinatekelezwa hata kabla hajawa waziri wa Afya.
N.B. Zile sindano ziongezwe makali, sometimes ni butu, kimbembe ukutne na anayechoma hana weledi. Dah!
 
Ushauri mzuri kwako ni waziri kuja hadharani na kutuambia kutakuwa na ubaguzi wa kupewa huduma kama uchangii damu.

Kila disciplines ina kanuni zake za kufanya kazi inabidi azijue kwanza kabla ya kuleta ubinifu unaokwenda tofauti na ethics za taaluma.

Jukumu la ku mobilise mikakati ya kukusanya damu ni lao, wakishindwa mbinu za kufanya kazi zao wanakuja na solution za ovyo kama hizi.

Muhimbili inatoa huduma za kimataifa akija mgeni kutibiwa anakuja na damu yake?

Watu wanaropoka mambo ya ovyo mnatetea. Hiyo ndio sababu wanampenda huyo hayo dada hapo afya ni kama gari bovu wanalisukuma wanavyotaka.
Mkuu inawezekana una point but umekaza kichwa sana kwa ummy sijui kwa nini ..
Hili jambo mbona halijaanza na ummy ..
Hii kampeni ni ya muda sana hawa watu wa damu salama miaka mingi tu uko nyuma hii ndo njia yao yakuhamasisha ,
utakapochangia damu siku ya siku likitokea la kutokea utapewa kipaumbele..
Why ummy kakufanya nini huyu mama mkuu..
 
Sijamzungumzia at personal level nimezungumza policy anayoinadi, mbona huwa namsifia pia katika viongozi wanao behave sahihi yeye number 1.

Utaki azungumziwe basi mueleze awe anafahamu lines of reasoning katika sector husika kabla ya kuja na kauli za ovyo.

Hiyo policy kama ipo tangia zamani ni mbovu na inalea uzembe badala ya ubunifu huko damu salamu and unethical too.

There are better methods to gather blood inventory na fikra za huduma ya upendeleo katika kuamasisha sio njia mojawapo.

Yeye majungu aliyokuwa akimfanyia mwenzake mpaka akarudishwa ulikuwa uyaoni.

Interest yangu katika afya ni kuimarishwa kwa quality of services kuna watu wazembe sana kwenye health delivery, too much medical errors, negligence, culture ya kukosa sympathy kwa watumia huduma and so forth.

Anahitajika mtaalamu wa kuwanyoosha wale watu, wakikosolewa utasikia watu humu madokta watasusa, sijui watakadhuru; kuwapa vichwa. Tunataka mtu ambae anaelewa procedures kama ni kosa la makusudi muhusika rumande imuhusu na kuvuliwa practice licence.

Binafsi nimepoteza wazazi wangu wote wawili because of poor medical intervention (errors) so ningependa kuona mtu mwenye uwezo wa kuwanyoosha kama Gwajima hao wazembe mahospitalini. Maza mchana katoka hospitali wanadai yupo poa mtu unamwona dhaifu badala ya kumweka undersupervision mtu ana pressure wanamuacha harudi nyumbani usiku ana angalia TV pressure imepanda safari. Baba nae operation ya kisukari kidonda cha mguu, kwenye operation ya kawaida kabisa akuamka tena.

Majuzi tumeona Dr Gwajima akiingia maabara na kukutana na sample za wagonjwa zimepita muda wa kuchukua na kwenda katika vipimo hao watu wanasubiri results wapangiwe matibabu sahihi; si mtu anapoteza maisha kizembe. Wakifokewa hoo huyu Gwajima mropokaji.

Wampeleke Ummy Mwalimu mazingira, sijui ofisi gani ya waziri mkuu, sheria au kwingine uone kama nitamzungumzia; lakini huku kwenye maisha ya watu hapana.
 
Sijamzungumzia at personal level nimezungumza policy anayoinadi.

Utaki azungumziwe basi mueleze awe anafahamu lines of reasoning katika sector husika kabla ya kuja na kauli za ovyo.

Hiyo policy kama ipo tangia zamani ni mbovu na inalea uzembe badala ya ubunifu huko damu salamu and unethical too.

There are better methods to gather blood inventory na fikra za huduma ya upendeleo katika kuamasisha sio njia mojawapo.

Yeye majungu aliyokuwa akimfanyia mwenzake mpaka akarudishwa ulikuwa uyaoni.

Interest yangu katika afya ni kuimarishwa kwa quality of services kuna watu wazembe sana kwenye health delivery, too much medical errors, negligence, culture ya kukosa sympathy kwa watumia huduma and so forth.

Anahitajika mtaalamu wa kuwanyoosha wale watu, wakikosolewa utasikia watu humu madokta watasusa, sijui watakadhuru; kuwapa vichwa. Tunataka mtu ambae anaelewa procedures kama ni kosa la makusudi muhusika rumande imuhusu na kuvuliwa practice licence.

Binafsi nimepoteza wazazi wangu wote wawili because of poor medical intervention, so ningependa kuona mtu mwenye uwezo wa kuwanyoosha kama Gwajima hao wazembe mahospitalini.

Wampeleke Ummy Mwalimu mazingira, sijui ofisi gani ya waziri mkuu, sheria au kwingine uone kama nitamzungumzia.
Mkuu una mixed feeling kwenye hili kubali ukatae shida yako ni sera na ummy pia ..
But So sorry kupoteza wazazi wako wote wawili.
 
Shida yangu sio Ummy; shida yangu ni uzembe uliokithiri kwenye afya.

Someone needs to sort that mess and it’s too technical for her.
 
Na pia alichosema ndio kinatekelezwa hata kabla hajawa waziri wa Afya.
N.B. Zile sindano ziongezwe makali, sometimes ni butu, kimbembe ukutne na anayechoma hana weledi. Dah!
Siyo kila mtu anaweza kuchangia damu, wengine damu yao baada ya kupimwa haikubaliki, sasa huyu ana kosa gani!
 
Shida yangu sio Ummy; shida yangu ni uzembe uliokithiri kwenye afya.

Someone needs to sort that mess and it’s too technical for her.
Ndugu Kilatha, mimi nadhani unasumbuliwa na chuki tu. Kiuhalisia hata huyo aliyejitolea damu akipatwa na tatizo ambalo litahitaji kuongezewa damu, ndugu na jamaa wanaweza kumchangia damu. Na sidhani kama kuna mtu anajitolea damu ili akipata tatizo apewe kipaumbele. Huko ni kujiombea matatizo, kitu ambacho sidhani kama kuna mtu anaweza kufanya hivyo.

Naamini unasoma michango mbali mbali inayotumwa hapa kujaribu kukuelewesha. Tatizo lako ni kwamba unajifanya unajua kuliko watu wengine. Lakini bahati mbaya huelekei kama unajua kama ambavyo unavyotaka watu wakuchukuliye. Ndugu yangu hata maneno tu ya kitaalamu yanakushinda kuandika! Na bado umeng'ang'ana hapa kutuaminisha kuwa u mjuzi. Au unataka cheo?

Nakushauri pumzika ndugu yangu maana unazidi "kujivua nguo".
 
Back
Top Bottom